Tofauti ya neno "Fahamu" na "Kujua"

Troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
19,882
38,512
Linaweza kuonekana swali la kipuuzi lakini haya maneno kama huwa yanatatiza.

Hivi mtu akisema ananifahamu na mwingine akasema ananijua. Wanaweza kuwa na maana sawa? Au yanatofautiana wapi. Je, lipi lipaswa kutumiwa wapi na lisitumiwe wapi.
Je, mtu anaweza akanifahamu lakini asinijue?(na pia kinyume chake)
 
Moja ya tofauti fahamu linatumika sana Zanzibar, kujua linatumika Tanzania bara.
 
Kumjua ni mpaka undani wake... ( Mfano: Mimi sipo hivyo wananisingizia :: Nakujua sana na tabia zako mbaya...)

Kumfahamu ni kumtambua mtu kawaida... (Mfano: unamfahamu fulani, :: ndiyo namfahami sii yule anayefanya kazi mahali fulani..)

Cc: mahondaw
 
Baasi wengi tunayachanganya.
 
Ufahamu unambatana na uelewa, kujua ni moja ya sifa inatokana na kukariri.

Ufahamu hauna mipaka wala mwisho lakini kujua kuna mipaka.

Asante.
 
Back
Top Bottom