Tofauti ya "Masharti" na "Vigezo"

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Mfano mwenye nyumba akikwambia, ukitaka kupanga nyumba yangu unapashwa uwe na "kigezo" hichi, uwe umeoa.
Ivi hilo si sharti?
 
Mfano mwenye nyumba akikwambia, ukitaka kupanga nyumba yangu unapashwa uwe na "vigezo" hichi, uwe umeoa.
Ivi hilo si sharti?

Vigenzo: ni sifa au ni njia ya kuingilia pahala,kwanza ukamilishe vigenzo ndio uingie au ukubaliwe,Mfano: Ili uingie chuo cha ufundi ni lazima uwe umefaulu Hesabu,Fiziksi, na kiengereza.

Masharti : ni Taratibu au mambo ambayo ni lazima kuyafanya,sikuzote huja baada ya kigenzo, Mfano: mwanafunzi atakaekubaliwa anatakiwa aingie darasani saa 1 kamili asubuhi, kama hakufika kwa muda atafukuzwa skuli. kufukuzwa skuli sio kua kakosa vigenzo au sifa za kusoma bali ameshindwa kufuata taratibu za shule, ila sifa anazo.


Tukirudi kwenye mfano wako,Kigenzo cha kuoa ni sifa anayotakiwa mpangaji awenayo, lakini masharti ataambiwa adumishe usafi,alipe umeme na maji, usafi,kulipa umeme na maji sio sifa( vigenzo) bali ni taratibu za nyuma alopanga(masharti).

 
8][/I]Vigenzo: ni sifa au ni njia ya kuingilia pahala,kwanza ukamilishe vigenzo ndio uingie au ukubaliwe,Mfano: Ili uingie chuo cha ufundi ni lazima uwe umefaulu Hesabu,Fiziksi, na kiengereza.

Masharti : ni Taratibu au mambo ambayo ni lazima kuyafanya,sikuzote huja baada yakigenzo, Mfano: mwanafunzi atakaekubaliwa anatakiwa aingie darasani saa 1 kamili asubuhi, kama hakufika kwa muda atafukuzwa skuli. kufukuzwa skuli sio kua kakosa vigenzo au sifa za kusoma bali ameshindwa kufuata taratibu za shule, ila sifa anazo.


Tukirudi kwenye mfano wako
,Kigenzo cha kuoa ni sifa anayotakiwa mpangaji awenayo, lakini masharti ataambiwa adumishe usafi,alipe umeme na maji, usafi,kulipa umeme na maji sio sifa( vigenzo) bali ni taratibu za nyuma alopanga(masharti).


Samahani mkuu, hapa tupo katika kuelimishana. Hapo kwenye italiki ni Vigezo au Vigenzo? maana
ingekuwa ni mara moja tu ningesema labda vidole vimeteleza.
 
Samahani mkuu, hapa tupo katika kuelimishana. Hapo kwenye italiki ni Vigezo au Vigenzo? maana
ingekuwa ni mara moja tu ningesema labda vidole vimeteleza.

Mkuu ni VIGENZO ndio niliokusudia sio kimakosa ila kwa hili sina uhakika kua niko sawa au wewe ndio uko sawa,
 
VIGEZO=factor,criteria

MASHARTI=conditions/terms


Nilitegemea jibu kama hili! Sisi Miafrika bwana hivi ni kwanini hatuna akili???!!! Kwani amekuuliza tafsiri ya maneno ,,masharti" na ,,vigezo" kwa Kiingereza?

Haya na nini tofauti kati ya conditions na factor/criteria?
 
Back
Top Bottom