TOFAUTI YA MANENO "MWAMBAO na PWANI"

Pwani ni sehemu ya ufukweni (ufuo wa pwani) mpaka sehemu ya bahari yenye kilindi /kina kidogo cha maji, ukienda kina kikubwa basi ni baharini, amma MWAMBAO ni sehemu ya juu kutokea pwani /ufukweni kwenda nchi kavu.(kwa uelewa wangu mdogo, hio ndio tofauti baina yao).
 
Heshima kwenu wakuu,

Naomba kufahamishwa tofauti ya maneno haya mawili, Mwambao na Pwani.
Hali halisi haina tofauti. Kiasili ilkuwa namna mbili tu ya kuiangalia sehemu ileile.
Mwambao inatokana na ku-ambaa, kwa maana wa kupita karibu. Kwa hiyo mwambao ilikuwa kiasili lugha ya wenye boti wanapopita majini karibu na nchi kavu.

Pwani inatokana na ku-pwa (maji kujaa- maji kupwa) + -ni, yaani eneo ambako maji ya bahari yanakuja na kwenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom