Tofauti ya makato kati ya kutoa pesa kwa mawakala na kutoa kwenye ATM

pangakali 2

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
238
220
Kuendelea kukua kwa teknolojia kumeleta chachu na kupunguza baadhi za adha tulizokuwa tunazipata enzi hizo ilikuwa ikifika mwisho wa mwezi kwenye ATM mashine unakuta kumefurika watu balaa.

Kwa sasa kuna mawakala wengi mtaani kwa kweli wametuepusha na mengi japo nao wana changamoto zake.

Swali la msingi. Je, Kuna tofauti gani kwa maana ya MAKATO ya huduma kati ya anayetolea pesa dirishani , ATM na kwa mawakala?
 
Mimi natumia CRDB, huwa kila mwisho wa mwezi wananitumia bank statement kwa kutumia email yangu. Kila muamala nilioufanya wamekata shilingi 1,017 tu. Sijawahi kufanya muamala kwa wakala, kutumia simbanking wala sijawaji kujiunga na hiyo huduma.
Wanaotumia mawakala watatupa uzoefu.
 
Kwa wakala gharama za makato zipo juu kidogo... Mfano Ukitaka kutoa Laki 4 kwa Wakala utakatwa si chini ya sh3000, wakati Atm unakatwa sh900-1000 ili kutoa Shilingi Laki 4
 
Nilitoa laki nane kwa wakala wa fahari huduma CRDB walikata kama 8,000/=

Kutoa hela hiyo ATM haizidi 2,500/=
 
Ok kwa kweli hizi Bank zinatozo tofauti tafauti, Lkn huwa hazitofautiani xanaa NMB, CRDB, NBC,AZANIA Ila usidanganyike kwenda kutolea hela dirishani si chini ya 6500 kwa NMB benk saccos ATM pia ni Mia 8 mpk Buku kwa mawakala xaxaa 1500 kuendele kulingana na trans-action all n all ATM is more cheaper.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom