Tofauti ya hivi vyeo dr,prof tanzania na nchi nyingine ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti ya hivi vyeo dr,prof tanzania na nchi nyingine ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, Jun 20, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijiuliza kuna nini kati ya madr wetu na nchi kama kenya na rwanda sipati jibu.
  Serikali inakusanya tril 8 halafu inatumia tril 10 hizo mbili nani analipa?
  Na je ikikaa madarakani miaka 10 si itafikisha deni la tril 20 kama watakuwa waungwana wasiongeze zaidi ya hizo mbili?maana yake ukiunganisha na deni lililopo ni kuwa kila mtz atakuwa anadaiwa karibu milioni moja?

  Ccm mnataka kutupeleka wapi?
  Mbona elimu yangu ni ndogo ila naona shida iliyopo katika bajeti yetu?au tume ya vyuo vikuu ianzishe utaratibu wa kuwapa maksi katika utumishi?ukitoka chuo unakuja na udr kavu ukianza utumishi wa umma kila mwaka tunakupa + au - kwa hiyo ukiboronga kwa miaka 5 unakuwa dr-5 potelea mbali hata kama itakuwa tanzania peke yake mbona hata hivyo ndiyo nchi pekee duniani ni tajiri kwa rasilimali lakini ni masikini wa kipato?
  Mbona ndiyo nchi pekee ina serikali ya chama badala ya nchi?
  Mbona ndiyo serikali pekee makusanyo yote ya ndani hayatoshi kuiendesha hiyo serikali ya chama?

  Hivi tanzania tunasoma ili tuelimike au tupate vyeti?
  Hivi wale wabunge wanaosimama na kuipongeza bajeti nzuri ya chama cha mapinduzi hawalioni hili?au wamepofuka?
  Nimwombe rais aitoe hii bajeti mwenyewe akaifanyie marekebisho,hatapungukiwa kitu badala yake atajijenga kama suala la katiba mpya.

  Kama madini yote tanzania hayawezi kutupa tril 10 tunachimba ya nini?nani katuloga?
  Mbona waarabu mafuta yao yanatosha kuendesha nchi?mbona botswana wameweza?au madini yetu ni daraja la 5?

  Naombeni niishie hapo wadau.
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Maprofesa na madokta wameficha elimu zao mfukoni na kuongozwa na wajinga kama lusinde,komba na mwigulu,shame kweli!
   
 3. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ma dr na ma prof wa Tz hawana imagination. matokeo yake wana njaa kali kuliko wasiosoma.
  Kama kuna ma-dr na ma prof waliofanikiwa kimaisha kwa kutumia elimu yao ni wachache ukilinganisha wale ambao. , hawana elimu kubwa. Njaa mbaya mkuu. nani alitegemea huyu waziri mpya wa madini na professor mwenye heshima yake atashabikia upuuzi?
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Baada ya kumuona Yule professor wa madini akirukaruka kwa furaha kama vile anacheza ngwasuma wakati Yule mzinzi akiongea nilibadilisha channel hapo hapo na Yule prof tutajuta atakuwa bonge la fisadi hapo baadae
   
 5. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mdau punguza hasira, unayoyasema tumeyajadili sana mpaka tumechoka na kuamua kuhamia M4C na uanaharakati mwingine. ona UAMSHO mfano, yote ni yaleyale madudu ya viongozi kujifanya viziwi.
  from the underlined statements;
  NO1: huu utaratibu haupo na kama serikali imeshinda kuunda mfano think-tank, ona NECTA wanavyoboronga ndo iwe ktk phd? la hasha hakuna jipya hapo
  NO 2: mzee sisi siyo nchi pekee duniani yenye utajiri wa rsilimali. tuna rasilimali lakini tumekaa tu kama mayatima lazima tuibiwe.

  NO3: kama kulogwa kumekaa kiimani basi ni either tumerogwa na MUNGU yaani laana au SHETANI yaani kurogwa. hapochacha!!!!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ringo Hebu ona dhaifu anavyoteuwa Majaji utafikiri anafyatua tofali
   
Loading...