Tofauti ya Demokrasia ya CCM na Demokrasia ya Watanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti ya Demokrasia ya CCM na Demokrasia ya Watanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by niweze, Nov 21, 2010.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tumeona CCM Inalia Foul ya Offside kwa Wabunge wa Chadema Kutoka Nje Katika Hotuba ya Dikteta JK. Kitu Gani na Haki Ipi ni Muhimu kwa Wananchi? CCM Wanaamini Wananchi Hawana Haki ya Kujua Matumizi ya Serikali, Wananchi Hawana Umuhimu wa Huduma Nzuri Mahospitali ila Wao Kutumia Uwezo Wao Kutibiwa London na India, Wananchi Hawana Haki ya Kuajiliwa ila Familia Zao na Watoto Wao Ndio Wapate Kazi tu, Wananchi Hawana Haki ya Elimu Nzuri ila Familia Zao Wapelekwa Nje ya Inchi Kusoma, Wananchi Hawana Haki ya Kujua Kura Zilipigwa Vipi na Nani Alihesabu Kura za Wananchi ila CCM Wanahaki ya Kusherehekea Uraisi na Kuhutubia Bungeni Kama Wanavyotaka.

  Demokrasia ya Wananchi Inafanana na Demokrasia Zote Duniani. Demokrasia Duniani Inasema Hivi: Uchaguzi wa Wazi na Haki kwa Wananchi. Demokrasia Haina Siri kwa Wananchi. Demokrasia ya Kweli Inasema Viongozi Wanachaguliwa na Wananchi na Kuongoza Inchi ili Kutatua Matatizo ya Inchi. Demokrasia ya Kweli Inaleta New Ideas za Kukabili Challenges za Inchi Kuanzia Matatizo ya Maji, Mikataba ya Machimbo ya Madini, Ufumbuzi wa Kilimo Bora, Uwekezaji wa Viwanda na Biashara ili Kupunguza Ukosefu Ajira Inchini, Ufumbuzi wa Elimu Bora na Huduma Mahospitalini na Mengi Yanayoikabili Inchi "Demokrasia Inasisitiza Uhumimu wa Katiba ya Ukweli kwa Manufaa ya Wananchi"

  Leo CCM Wanalia Wanataka Kujua Kwanini Chadema Wanatoka Bungeni. Jibu ni Hili: Kikwete Hakuchaguliwa na Wananchi na Kila Mwananchi Anayo Haki ya Kutomtambua JK. Katiba ya CCM Inawalinda CCM na JK, Wanafikiri Sisi Sote ni Vipofu Kama Green Guards? Kama Wanataka Negotiation Tutaanzia Katiba Mpya ya Inchi.
  "Hatuwezi Kuwa na Katiba ya Chama Kimoja na Kuwaeleza Wananchi na Dunia Tunakaribisha Siasa ya Vyama Vingi Duniani, This is Not Going to Fly Anymore"
   
Loading...