Tofauti ya baba na mwana

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Miaka 36 ya kifo cha Abeid Amani Karume

Na Jabir Idrissa
WAKATI Wazanzibari wanakumbuka mauaji ya kiongozi wao wa kwanza baada ya Mapinduzi ya 12 Januari 1964, vilevile wanatafakari mustakbali wa taifa alilolifia.

Taifa ambalo Mzee Abeid Amani Karume alilikuta na kiti kwenye Umoja wa Mataifa (UN), leo ni taifa ndani ya taifa; ndani ya kile kinachofahamika zaidi kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini hilo halikuja kwa bahati mbaya. Kama kuna tatizo, litakuwa linatokana na lengo la kuunganisha mataifa mawili, lililokuwa vichwani mwa waasisi wenyewe, pamoja na staili ya uongozi iliyofuatia.

Mawazo ya kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika yaliyomjia Mwalimu Julius Nyerere na yakamridhi Karume, inaonekana yalikuwa tofauti.

Kuna simulizi nyingi kuhusu lengo na shabaha ya muungano kama ilivyoeleweka kwa viongozi hao. Kuna wanaosema Karume aliridhia ili apate nguvu ya kudhibiti kikamilifu mamlaka, bali Mwalimu Nyerere alilenga kuidhibiti Zanzibar.

Inaelezwa Mwalimu alifanikisha Muungano kwa msaada mkubwa wa Marekani na Uingereza. Historia inaonyesha mabalozi wa nchi hizo, hasa waliokuwa Nairobi, walikuwa wakiwasiliana kupanga jinsi ya kuziunganisha Zanzibar na Tanganyika.

Vyovyote ilivyokuwa, leo kuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utawala wake. Zanzibar, baada ya mapinduzi, imepitia vipindi sita hadi sasa.

Kipindi cha kwanza kilikuwa kile ambacho Karume alikuwa kileleni kama kiongozi wa mapinduzi na rais wa nchi. Maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii yalishuhudiwa kipindi hiki.

Kikafuata kipindi cha ujio wa demokrasia na misingi ya utawala bora. Hiki kiliongozwa na Aboud Jumbe Mwinyi hadi alipolazimishwa kujiuzulu, ndani ya vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dodoma, mwaka 1984.

Ni kipindi kilichoipatia Zanzibar Katiba yake ya kwanza, baada ya kuongozwa kwa sheria za amri za Rais. Katiba ilizaa Mahakama ya kisheria dhidi ya ile ya “wananchi;” ikazaa Baraza la Wawakilishi badala ya Baraza la Mapinduzi lililotunga sheria na kuendesha dola.

Kipindi cha tatu, kifupi zaidi ya vyote, ni kilichojenga misingi ya uhuishaji uchumi na uimarishaji sekta za kijamii, pamoja na heshima kwa mwanadamu. Hiki kiliongozwa na Ali Hassan Mwinyi.

Kutoka hapo, kikaja kipindi cha nne, kilichoendeleza mema, ingawa pia kilileta msukosuko mkubwa kisiasa kwa kuwa kulijengeka chuki za Upemba na Uunguja. Kilikuwa chini ya Idris Abdulwakil.

Kilifuata kipindi cha mzinduko wa kiuchumi na harakati za demokrasia ya karne mpya. Hicho kiliongozwa na Dk. Salmin Amour Juma.

Sasa Zanzibar inapita katika kipindi cha sita kinachoongozwa na Amani Abeid Amani Karume, mwana wa kuzaa wa Mzee Karume, muasisi wa mapinduzi.

Tofauti kati ya baba na mwana

Hapa ndipo lengo la makala hii: kukumbuka mauaji ya Mzee Karume kwa kumnasibisha na mwanawe, sambamba na kutazama namna maongozi yao yalivyotofautiana.

Kutofautiana huko ndiko kunakothibitisha kuwa Karume baba ameizalia Zanzibar mwana mwenye sura mbili.

Wazee waliotangulia wakiwemo waliocheza naye, wanamsifia kuwa aliipenda Zanzibar kama nchi yake ya asili. Mwenyewe ana asili ya Wanyasa wa Malawi na alifika Unguja na umri wa miaka saba hivi na kulelewa kijiji cha Kiongoni, Mwera, kilomita tisa kutoka mjini Zanzibar.

Karume alisoma Shule ya Msingi ya Mwera hadi darasa la nne. Baadaye alianza kazi ya ubaharia; akisafiri kwa majahazi, safari zilizomfikisha nchi nyingi kwa kutumia meli za mizigo alimofanya kazi.

Kuchanganyika kwa Karume na vijana wenyeji, kulimvuta katika harakati za kisiasa hadi kuundwa Afro-Shirazi Party (ASP). Alionekana mkakamavu, msemaji mzuri na akapewa uongozi. Akawa mmoja wa vijana madhubuti katika harakati za kupigania uhuru.

Ni Karume baba ambaye aliongoza ASP kuendeleza mapambano dhidi ya himaya ya Masultani ambao 10 Desemba 1963 walikuwa wamepewa “uhuru” na Uingereza chini ya muungano wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP).

Uhuru uliwezesha kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, ikiongozwa na Waziri Mkuu, Mohammed Shamte, mwenyeji wa Pemba, aliyekuwa kiongozi wa ZPPP.

Harakati za kupinga uhuru ambao Waafrika wengi waliita “bandia,” ziliongozwa na ASP, chama kilichokuwa kikilalamika kunyimwa haki ya kuongoza licha ya kupata kura nyingi uchaguzi wa 1957, 1961 na 1963.

Hatimaye ASP wakafanikiwa kuung’oa utawala wa Kisultani kwa Mapinduzi ya 1964.

Karume aliongoza nchi kwa sheria za kiimla (mkono wa chuma), lakini alijenga misingi imara ya kukuza uchumi.

Ni utawala wake uliojenga, Unguja na Pemba, mioundombinu ya barabara, mifumo ya maji safi na majitaka, hospitali, vituo vya afya, shule na mawasiliano, kwa mfano ujenzi wa kituo cha televisheni ya rangi ambacho ni cha kwanza Afrika.

Majengo ya kifahari yanayoonekana leo katika maeneo ya Michenzani, Unguja, na katika miji na vitongoji mbalimbali Unguja na Pemba, ni matokeo ya uongozi wake na visheni ya Zanzibar aliyotaka kujenga.

Hadi leo kuna simulizi kuwa Karume alichukua kamba na kuanza kupima mahali ambapo hoteli kubwa ya Bwawani mjini Zanzibar inaonekana. Alifanya hivyo pia kwa uwanja wa ndege na uwanja wa michezo.

Zipo simulizi nyingi za namna Karume alivyokuwa akipingana na mainjinia wakati wa ujenzi. Viongozi wa serikali, ASP pamoja na mafundi, leo wanasema ujasiri wake ulisaidia kukwamua pale palipokwama.

Karume baba alitumia raslimali za taifa kunufaisha watu, mchango mkubwa ukitokana na karafuu, zao ambalo zaidi ya asilimia 90 ya uzalishaji wake hutegemea kisiwa cha Pemba.

Hadi anauawa, Zanzibar lilikuwa moja ya mataifa machache, ingawa ndani ya Muungano, yaliyokuwa na fedha nyingi za kigeni na uchumi unaokua na kuimarika. Itakumbukwa ni kipindi hicho, Zanzibar iliikopesha fedha Bara.

Yapo aliyoyatenda au kutotenda ambayo yalizua chuki dhidi ya uongozi wake. Kuna madai ya kuruhusu ndoa za “nguvu” kati ya watu wa asili ya Asia na Afrika.

Alidaiwa “kumpoteza” mtu mmoja aitwaye Mohammed Humud, aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya kuua mtu; na ambaye mtoto wake, Humud Mohammed Humud, ndiye alikuja kumuua Karume kwa madai ya kulipa kisasi.

Kifo cha Karume kilitokea 7 Aprili 1972, kwa kumiminiwa risasi akiwa Makao Makuu ya ASP, jengo ambalo sasa ni Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui.

Mzee Karume alikuwa kiongozi wa watu hasa. Akiwajali, akiwatembelea mara kwa mara; alihimiza kazi za maendeleo, akisimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo, yakiwemo makazi bora kama aliyojenga Michenzani.

Mzee Karume alifariki miaka 36 iliyopita lakini bado anakumbukwa kwa mema mengi aliyofanya na kuelekeza. Alipata bahati mbaya kuwa baadhi ya wasaidizi wake katika kuendeleza malengo ya mapinduzi, walikuwa katili, walichochea uhasama miongoni mwa watu.

Kifo chake kinasikitisha maana hakikupaswa kuwa cha kikatili namna ile. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin.

Utawala wa mwana

Tangu 2000 Zanzibar inatawaliwa na mtoto wake, Amani Abeid Karume aliyeingia katika siasa baada ya kuwa mfanyabiashara. Alishika nafasi za kiutendaji serikalini hadi kufikia ngazi ya Katibu Mkuu wa wizara.

Mwaka 1990, wakati Rais akiwa Dk. Salmin, aligombea uwakilishi jimbo la Rahaleo na kushinda. Aliteuliwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko. Baada ya uchaguzi wa 1995, aliposhinda tena uwakilishi, aliteuliwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.

Ulipokaribia mchakato wa CCM kutafuta mgombea urais kwa ajili ya uchaguzi wa 2000, Karume hakupendezwa na mkakati wa Dk. Salmin wa kutaka marekebisho ya Katiba ya Zanzibar, ili aweze kugombea tena.

Karume aliongoza kundi la kupinga mkakati huo, akiwa pamoja na Mohamed Aboud Mohamed, mbunge mteule wa Rais Jakaya Kikwete, na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Baada ya mkakati wa Dk. Salmin kuuliwa Julai 2000 na maamuzi ya vikao vya juu vya CCM mjini Dodoma, jina la Karume lilipaa akionekana mwanasiasa mzalendo na mwanademokrasia akisaidiwa na kampeni za “tunataka kijana” zilizovumishwa na akina Kikwete na wenzake.

Bahati ya mtende

Kwa karata hiyo, badala ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kumteua Dk. Mohamed Gharib Bilal, aliyekuwa Waziri Kiongozi kwa miaka 10 chini ya Dk. Salmin, na ambaye ndiye aliongoza kwa alama katika Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, ilimteua Karume.

Karume alipata kura tisa (9) tu dhidi ya kura 44 alizopata Dk. Bilal kwenye Kamati Maalum.

Inatosha kusema hayo ndiyo yaliyotilia nguvu kampeni ya CCM na serikali kuhakikisha Karume anapata ushindi na kuunda serikali, liwe liwalo.

Karume alitangazwa mshindi baada ya kukurukakara nyingi za dola. Visanduku vilikwapuliwa kutoka kwa mawakala na kura zikachezewa. Baada ya wiki mbili, CCM wakajitangazia ushindi.

Rais Karume aliunda serikali. Akateua mawaziri watatu tu kutoka Pemba; Salim Juma Othman, aliyempa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Dk. Ali Mohamed Shein, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora, na Mohamed Aboud.

Udhaifu wake ulianzia hapo. Ukiacha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Iddi Pandu Hassan, aliwatupa mawaziri wote aliowateua Dk. Salmin.

Chini ya Karume mtoto, utawala wake umeengua Wapemba katika ajira pamoja na nafasi za masomo. Ameendeleza sera za vituko na visa dhidi ya vyama vya upinzani. Ni kawaida kwa vyama hivi, kunyimwa hata haki ya kufanya mikutano.

Ni utawala huu uliozuia vyama hivi kufanya kampeni katika baadhi ya majimbo wakati wa uchaguzi, ukidai wananchi katika maeneo hayo “tayari wameichagua CCM.”

Pale vyama viliporuhusiwa kufanya kampeni, taarifa zao hazikutoka kwenye vyombo vya habari vya serikali.

Utendaji wa aina hiyo, mgawanyiko ndani ya CCM ukakua na makundi kushamiri.

Ni utawala wa Karume mtoto uliokumbwa na kashfa ya mauaji ya raia walioandamana wakidai haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Migogoro ya ardhi imezidi, huku rais na mawaziri wake wakihusishwa na vyanzo vya migogoro hiyo na kujitwalia ardhi katika maeneo muhimu kwa hadhi na kiuchumi. Hapa ameshindwa kusimamia mgawanyo sawa na matumizi bora na endelevu ya raslimali ardhi.

Chuki za kisiasa kati ya wafuasi wa CCM na upinzani, hasa wa CUF, zimechochewa kwa kebehi na kejeli za viongozi wa CCM kudai wapinzani wataisikia ikulu redioni, kamwe hawatapasogelea.

Ni Karume, katika mkutano wake wa kampeni ya uchaguzi 2005, alisema kama wapinzani wanafanya masihara, wanamapinduzi wataandaa “silaha za 1964.”

Hapa alikusudia kukumbusha watu mapinduzi yaliyofanikishwa kwa mapanga na mashoka. Alimaanisha kuwa patakuja mapinduzi iwapo CUF watashinda uchaguzi.

Karume ameongoza wahafidhina wanaoamini wanayo hatimiliki ya utawala Zanzibar. Kwa hilo, Karume mtoto anatawala, wakati baba yake, aliongoza.

Karume baba alilinda mapinduzi kwa kujenga nchi na kuwatumainisha na maendeleo yanayoonekana, Karume mtoto ni mtu wa majigambo na ana “sera” ya chuki na masimango.

Wananchi wanashuhudia matumizi mabaya ya raslimali na mapato; harakati za kudhibiti mamlaka badala ya kutumia mapato kujenga watu kielimu na kiuchumi.

Ukipita mitaani utakuta ujenzi mpya, lakini mwingi umefanyika kwa fedha za misaada na nguvu za wananchi. Fedha za walipa kodi zinakwenda wapi, wanauliza wananchi.

Karume amesema asiyetaka serikali yake ahame nchi; kwamba atashinda uchaguzi hata kwa kura yake na mkewe tu.

Sasa anatajwa kuwa ndiye aliyeshauri kuitishwa kura ya maoni Zanzibar, ili kuondoa mgogoro wa kisiasa uliopo. Aseme na kutenda nini zaidi ndio athibitishe uhafidhina na hata mpinga demokrasia na maendeleo?

Tulikuwa na Karume na tunaye Karume, bali huyu wa sasa, na siasa anazojenga, haleti matumaini kwa wananchi, leo na kwa kizazi kijacho.

Source: MwanaHalisi
 
Taifa ambalo Mzee Abeid Amani Karume alilikuta na kiti kwenye Umoja wa Mataifa (UN), leo ni taifa ndani ya taifa; ndani ya kile kinachofahamika zaidi kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini hilo halikuja kwa bahati mbaya. Kama kuna tatizo, litakuwa linatokana na lengo la kuunganisha mataifa mawili, lililokuwa vichwani mwa waasisi wenyewe, pamoja na staili ya uongozi iliyofuatia.

Mawazo ya kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika yaliyomjia Mwalimu Julius Nyerere na yakamridhi Karume, inaonekana yalikuwa tofauti.

Majengo ya kifahari yanayoonekana leo katika maeneo ya Michenzani, Unguja, na katika miji na vitongoji mbalimbali Unguja na Pemba, ni matokeo ya uongozi wake na visheni ya Zanzibar aliyotaka kujenga.

Hadi leo kuna simulizi kuwa Karume alichukua kamba na kuanza kupima mahali ambapo hoteli kubwa ya Bwawani mjini Zanzibar inaonekana. Alifanya hivyo pia kwa uwanja wa ndege na uwanja wa michezo.

Zipo simulizi nyingi za namna Karume alivyokuwa akipingana na mainjinia wakati wa ujenzi. Viongozi wa serikali, ASP pamoja na mafundi, leo wanasema ujasiri wake ulisaidia kukwamua pale palipokwama.

Karume baba alitumia raslimali za taifa kunufaisha watu, mchango mkubwa ukitokana na karafuu, zao ambalo zaidi ya asilimia 90 ya uzalishaji wake hutegemea kisiwa cha Pemba.

Hadi anauawa, Zanzibar lilikuwa moja ya mataifa machache, ingawa ndani ya Muungano, yaliyokuwa na fedha nyingi za kigeni na uchumi unaokua na kuimarika. Itakumbukwa ni kipindi hicho, Zanzibar iliikopesha fedha Bara.

Mzee Karume alikuwa kiongozi wa watu hasa. Akiwajali, akiwatembelea mara kwa mara; alihimiza kazi za maendeleo, akisimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo, yakiwemo makazi bora kama aliyojenga Michenzani.

Mzee Karume alifariki miaka 36 iliyopita lakini bado anakumbukwa kwa mema mengi aliyofanya na kuelekeza. Alipata bahati mbaya kuwa baadhi ya wasaidizi wake katika kuendeleza malengo ya mapinduzi, walikuwa katili, walichochea uhasama miongoni mwa watu.

Kifo chake kinasikitisha maana hakikupaswa kuwa cha kikatili namna ile. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin.

Utawala wa mwana

Tangu 2000 Zanzibar inatawaliwa na mtoto wake, Amani Abeid Karume aliyeingia katika siasa baada ya kuwa mfanyabiashara. Alishika nafasi za kiutendaji serikalini hadi kufikia ngazi ya Katibu Mkuu wa wizara.

Bahati ya mtende

Kwa karata hiyo, badala ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kumteua Dk. Mohamed Gharib Bilal, aliyekuwa Waziri Kiongozi kwa miaka 10 chini ya Dk. Salmin, na ambaye ndiye aliongoza kwa alama katika Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, ilimteua Karume.

Karume alipata kura tisa (9) tu dhidi ya kura 44 alizopata Dk. Bilal kwenye Kamati Maalum.

Inatosha kusema hayo ndiyo yaliyotilia nguvu kampeni ya CCM na serikali kuhakikisha Karume anapata ushindi na kuunda serikali, liwe liwalo.

Karume alitangazwa mshindi baada ya kukurukakara nyingi za dola. Visanduku vilikwapuliwa kutoka kwa mawakala na kura zikachezewa. Baada ya wiki mbili, CCM wakajitangazia ushindi.

Ni utawala huu uliozuia vyama hivi kufanya kampeni katika baadhi ya majimbo wakati wa uchaguzi, ukidai wananchi katika maeneo hayo “tayari wameichagua CCM.”

Ni utawala wa Karume mtoto uliokumbwa na kashfa ya mauaji ya raia walioandamana wakidai haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Migogoro ya ardhi imezidi, huku rais na mawaziri wake wakihusishwa na vyanzo vya migogoro hiyo na kujitwalia ardhi katika maeneo muhimu kwa hadhi na kiuchumi. Hapa ameshindwa kusimamia mgawanyo sawa na matumizi bora na endelevu ya raslimali ardhi.
.

Ni Karume, katika mkutano wake wa kampeni ya uchaguzi 2005, alisema kama wapinzani wanafanya masihara, wanamapinduzi wataandaa “silaha za 1964.”

Hapa alikusudia kukumbusha watu mapinduzi yaliyofanikishwa kwa mapanga na mashoka. Alimaanisha kuwa patakuja mapinduzi iwapo CUF watashinda uchaguzi.

Karume ameongoza wahafidhina wanaoamini wanayo hatimiliki ya utawala Zanzibar. Kwa hilo, Karume mtoto anatawala, wakati baba yake, aliongoza.

Karume baba alilinda mapinduzi kwa kujenga nchi na kuwatumainisha na maendeleo yanayoonekana, Karume mtoto ni mtu wa majigambo na ana “sera” ya chuki na masimango.

Ukipita mitaani utakuta ujenzi mpya, lakini mwingi umefanyika kwa fedha za misaada na nguvu za wananchi. Fedha za walipa kodi zinakwenda wapi, wanauliza wananchi.

Karume amesema asiyetaka serikali yake ahame nchi; kwamba atashinda uchaguzi hata kwa kura yake na mkewe tu.

Sasa anatajwa kuwa ndiye aliyeshauri kuitishwa kura ya maoni Zanzibar, ili kuondoa mgogoro wa kisiasa uliopo. Aseme na kutenda nini zaidi ndio athibitishe uhafidhina na hata mpinga demokrasia na maendeleo?

Tulikuwa na Karume na tunaye Karume, bali huyu wa sasa, na siasa anazojenga, haleti matumaini kwa wananchi, leo na kwa kizazi kijacho.

Source: MwanaHalisi

Tofauti kubwa kati ya baba na mwana hapa ni kama mbingu na Ardhi Mwandishi wa makala hiyo ameonyesha jinsi Karume Baba alivyojitahidi kuinua hali ya maisha ya wananchi wa zanzibar. Mwandishi anasema ilifika kipindi bara ilikopeshwa na Zanzibar leo hii china ya Karume mtoto Zanzibar ina ubavuwa kuikopesha Bara?
 
Back
Top Bottom