Tofauti ni ipi?

sifa (nm): uzuri au ubaya wa kitu/mtu. Kwa mfano, mgombea hutakiwa kueleza sifa zake, na watu wakamhukumu kwa tabia yake
tabia (nm): mazowea (mazuri au mabaya) yanayotokana na kurudiarudia hali, mwendendo au matendo. Mfano, udaku, undumilakuwili, ukarimu, kulamba vidole wakati wa kula ni tabia.

Tafauti nyengine ni kuwa kisarufi kutokana na neno sifa tunaweza kupata tendo la kusifu, kusifika, kusifiwa lakini neno tabia haliwezi kunyambulika zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom