Tofauti na SADC iliyoleta Marais 8, Jumuiya ya Afrika Mashariki amekuja Rais Kenyatta pekee kumuaga Hayati Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,772
Anayeshikamana na wewe wakati wa shida ndiye rafiki wa kweli.

Kiukweli Jumuiya ya SADC imetushika mkono kiuhakika katika msiba huu mkubwa wa taifa.

Tumeshuhudia Marais kutoka Msumbiji, Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Congo nk wakija kumuaga Hayati Magufuli ambaye alikuwa kiongozi mwenzao.

Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tumemshuhudia Rais Uhuru Kenyatta pekee kati ya Marais 5 wanaounda Jumuiya.

Itoshe tu kusema SADC ndio marafiki wa kweli.
 
Ndiyo ujifunze Bwashee kwenye kuchagua marafiki. Wengi ni wanafiki na ma opportunists! Ila karibia wote nadhani wameogopa Corona bila shaka. Ingawa hii sababu nayo haina mashiko!

Au labda walimpenda sana marehemu! Hivyo wangekuja kumuaga, wangeishia kulia tu 😭😭😭😭😭 hadharani!
 
Ndiyo kipimo chako siyo?

Can't you look the other side of the shilling?

Wameshiriki kwa namna nyingine. Si lazima iwe kwa namna unayotaka. Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan wote hao wanaomboleza na sisi kwa siku 14 na bendera za nchi zao zinapepea nusu mlingoti kipindi chote hiki. Je, hili siyo kubwa sana?

Why don't you at least recognize and appreciate this?

After all mtu hajazikwa. Msiba unaendelea. May be they will come 2morro or even after burial..
 
Wengi nimeona mnalalamika bila hoja za msingi, mmesahau kwamba Ijumaa mwendazake atazikwa na ndiyo siku muhimu sana.

Wasipokuja siku hiyo, tunaweza kuwapa lawama lakini si kwa siku ya jana.

Nina hakika Kenyatta asipokuja siku ya mazishi na hawa marais wengine wakaja basi wabongo lazima mtamsema Kenyatta

Punguzeni upuuzi wa maisha.
 
Msipende kutazama vitu vidogo vidogo. Hapo Burundi, alipofariki Rais wao, Rais wetu alienda?

Hawa Marais ni binadamu, tunayoyajua kuhusu maisha yao ni machache. Ni wangapi walikuwa wanajua kuwa Hayati Magufuli alikuwa na tatizo la moyo? Kila wakati tulimlaumu kwa kutokusafiri, lakini huenda tatizo lake la afya lilimfanya asiwe huru sana kusafiri. Watu wenye matatizo ya afya ya kudumu, mara nyingi hupata matatizo ya hapa na pale. Yawezekana wewe unapopata msiba, yeye siku hiyo akawa ameamka vibaya kutokana na tatizo lake la afya.

Mseveni ni mtu mzima sana, huwezi kujua ana tatizo gani la afya. Raila alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu, hakuja. Yeye angalao tumajua anasumbuliwa na corona. Kagame, hivi karibuni amepokea chanjo. Wakati mwili ukiendelea kujikinga, unashauriwa ujikinge ili usipate maambukizi wakati chanjo ikiwa bado haijakutengenezea kinga.
 
Huwezi kumleta Kagame kirahisi hivi, ziara zake ni kupangwa muda mrefu kabla. Museveni amekuwa akija mara kibao hapa nchini. Salva Kiir naye nchi yake vurugu ziara zake ni za kupangwa kimkakati.

Labda Burundi ndio angeweza kuja. Hata hivo Magufuli mwenyewe alikuwa hasafiri sana. Corona nayo imechangia pakubwa
 
Uhuru ni mtu na nusu.....Development has no party ...Five Again.

Cc: MK254

Hiki ni kipindi hatari sana na nyie Watanzania mnavyokusanyika na kubanana kwenye huu msiba bila kuchukua tahadhari kisha mnategemea nani aje kujitoa mhanga kisa undugu.

Hao watakuja siku ya kumzika kisha wasepe, masuala ya maisha hayana utani maana uhai unao mmoja tu na hauna mbadala, hiki kirusi kinaondoka na yeyote hata uwe tajiri mwenye hela au rais, kinakubeba tu.

Ingekua huyu kwenye hii picha ndiye anaongoza, nahisi mambo yangekua tofauti maana yeye huwa mjanja sana alishasema za kuambiwa ongeza na zako pia. Ona hapa alivyojilinda wakati wengine wamejianika mazima mazima.

2720559_jk.jpg
 
Nadhan itoshe kusema kazi ya Mungu ibakie kama ilivo, he is gone already and kilichobaki ni sisi ambao yatupasa kujiandaa kama yeye alivojiandaaa! binadam hatuna rights zozote za kuishi apa duniani kwa sababu ni kupita, ukishapita we shukuru Mungu thats all and on to the next jouurney
 
Back
Top Bottom