Tofauti na Magufuli, Nyerere alielewa mataifa tajiri yanatuonea, kutuingilia na alijua jinsi ya kubabiliana nayo kwa busara bila nguvu na umwamba!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kuna kitu kimoja ambacho Magufuli anapaswa kutafakari sana - jinsi ya kukabiliana na mataifa tajiri pale ambapo anaona kama yanatukandamiza au kutuingilia.

Nasema hivi kwa kuwa ni wazi sana Magufuli anapewa ushauri usiofaa na Kabudi - kujaribu kuyakabili haya mataifa kama vile tuko sawa nayo - tuna uzito sawa. Ukweli ambao Magufuli anapaswa kuujua na kuukubali ni kwamba haya ni mataifa yenye nguvu, na yanaweza kutufanya chochote na tusiwe la kufanya. Na hata yanaweza kumuondoa Magufuli madarakani kwa namna yeyote ile.

Hatusemi kwamba tunapaswa kufyata mkia kila wakati mataifa haya tajiri yanapoonekana kama yanatunyanyasa au kuingilia mambo yetu. Inabidi kuwa na busara kujua ni jinsi gani tunaweza kukabiliana nayo kwa hekima - non-confrontational engagement with first world countries.

Kwa mfano, kuna wakati naona Kabudi anatumia sana sheria kubisha kwamba tuna haki ya kufanya mambo fulani. Basi ushauri wangu kwa Kabudi ni kwamba jinsi Magufuli anavyojali kuheshimu Katiba ya Tanzania ndivyo hivyo hivyo haya mataifa yanajali sheria za kimataifa! Kwa mfano, Tanzania inawafukuza wawakilishi wa UN au mabalozi wa nje kwa kuwa wanaingilia mambo yetu. Kweli tunataka kuonyesha umwamba huu? Kwani tukiwafukuza hao wanaooteuliwa tena ndio hawataingilia mambo yetu? Sasa sana tunakuwa tumejiwekea historia mbaya na haya mataifa. Wao wanaweza kutuumiza sana zaidi ya sisi kuwafukuza wateule wao. Sometimes kinachohitajika ni kulaani tu vitendo vyao hadharani, sio kuwafukuza na kujiwekea rekodi mbaya katika mahusiano.

Angalia kwa mfano, Nyerere alijua wazi kwamba UK, USA kama mataifa walikuwa rafiki wa serikali ya Makaburu, lakini bado Nyerere alijua jinsi ya kuwa na uhusiano na UK na USA nje ya uwanja wa kuongelea suala la ubaguzi wa Makaburu.

Na mara nyingine sio kwamba haya mataifa yanakuwa yanasema uongo juu ya mambo tunayaokwaruzana nayo. Kwa mfano suala la uchaguzi au kuonea wanasiasa wa upinzani. Ni kweli kuna mambo mengi sana hapa yana kasoro kubwa, na tunapaswa kushutumiwa kama taifa. Hatupaswi kulalamika wanapotuchukua hatua dhidi yetu. Tunapaswa kujiuliza kama yot wanayosema sio kweli. Kwa nini Tanzania na sio Botswana, au Kenya, au Namibia? Kwani nchi hizi hawana chaguzi au vyama vya upinzani?

Kwa hiyo ningependa kutoa ushauri wa bure kwa Magufuli na Kabudi. Mkakati mnaochukua kukabiliana na mataifa tajiri ni potofu sana. Msipoangalia sisi ndio tutaumia. Hata Nyerere alisema, kumpambanisha bondia wa uzito wa unyoya, feather na heavy weight ni murder! Sasa nyie mnajua sisi ni feather weight, na bado mnajipeleka mbelembele kupambana na haya mataifa ambayo ni heavy weight, mnatarajia kweli mtashinda hilo pambano? Kuna njia mbadala za kumpiga mtu wa heavy weight ukiona anakuonea, sio kuitisha mpambano naye - atakuua, murder!
 
Hizi ni headlines za awamu ya Magufuli peke yake haijawahi tokea

1605799480005.png

Huyo ni mtu binafsi, hata kama anawa support sio kwa kuiwakilisha UN. Na wakiwa na ushahidi wapeleke UN ataondolewa kwenye wadhifa wake wa UN
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Nyerere yupi unae mzungumzia?
Nijuavyo Nyerere alibanwa na benki ya dunia kuhusu Sera za Tanzania kwenye uchumi, ndio mpaka akaingizwa kwenye vita na Uganda ili kuikamua nchi kiuchumi, na baada ya hapo nchi ikayumba sana mpaka akalazimika ang'atuke ili kupisha mageuzi (matakwa ya benki ya dunia) ya uchumi kwa bwana ruksa ndio nchi ikaanza kukaa vizuri, kila raisi ana changamoto zake maana wao ni binadamu, kukosea kupo, japokuwa sio Sera za kibepari kuona masikini anafanikiwa, utatumia kila aina ya rasilimali zilizopo kumkandamiza!
 
Kabudi awe makini sana akienda huko kwa mabberu wanaweza kumkamata kama ndege zetu akashindwa kurudi
 
Labda nikuulize maswali binafsi, una mtoto na Familia ya kulea ? I mean, kwa nini uko dhaifu kiasi hicho ? Je unaweza kuilinda na kuitetea Familia yako kama unayao ? Hauna baba na mama kama wengine ? Hivi mnafikiri Muzungu amakeaa huko muda wote anaiwaza Tanzania ni nani aliwadanganya? Kwa taarifa yenu tu katika nchi ambazo siyo muhimu kwa Muzungu Tanzania ni mojawapo, Muzungu hawezi kupoteza usingizi sababu ya tanzania, his plate is full, acheni ujinga fanyeni kazi, ...
 
Mtasubiri sana hayo ya mnyoosho,
Na hata ikitokea anaeumia ni wewe na sio yeye.
Utakekosa huduma ni wewe sasa unafurahia nini?
Ujinga mtupu.
Wewe, watoto wako, nduguzo hamtaumia? Maana umekomaa tuu kumwambia wewe, wewe as if unaishi Somalia...
 
Wewe, watoto wako, nduguzo hamtaumia? Maana umekomaa tuu kumwambia wewe, wewe as if unaishi Somalia...
UWezo wa kutafuta ninao hata katika hali ngumu, kwa hiyo nyie watoto mayai ndio mtayeseka
 
Labda nikuulize maswali binafsi, una mtoto na Familia ya kulea ? I mean, kwa nini uko dhaifu kiasi hicho ? Je unaweza kuilinda na kuitetea Familia yako kama unayao ? Hauna baba na mama kama wengine ? Hivi mnafikiri Muzungu amakeaa huko muda wote anaiwaza Tanzania ni nani aliwadanganya? Kwa taarifa yenu tu katika nchi ambazo siyo muhimu kwa Muzungu Tanzania ni mojawapo, Muzungu hawezi kupoteza usingizi sababu ya tanzania, his plate is full, acheni ujinga fanyeni kazi, ...
Nyerere was very clever, Ndiyo maana hata uhuru kaupata kwa kuwashinda wazungu kwa hoja na siyo kwa kumwaga damu unnecessarily....
 
Back
Top Bottom