Tofauti na CHADEMA, CCM ukikosea unapewa nafasi ya kujieleza, soma yanayojiri Dodoma

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,937
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo CCM ni chama cha watanzania wote kwa ajili ya watanzania.

Kufuatana na kero na malalamiko yaliyojitokeza wakati wa ziara ya Katibu mkuu, Kamati kuu imewaita na kuwahoji baadhi ya viongozi ili kutatua matatizo hayo.

Tofauti na Chadema, ambako tungetegemea kusikia ngumi na vitofali, CCM kama ilivyo ada, wanatumia demokrasia na kufuata haki za binadamu,

Soma taarifa hii;
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana mjini Dodoma kwa kikao chake cha kawaida tarehe 13/12/2013. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilipokea taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kwenye baadhi ya mikoa nchini.
Kamati Kuu imepongeza ziara hizo kwa kuwa na mafanikio makubwa na kwa jinsi zilivyoongeza uhai wa Chama na zilivyojishughulisha na mambo na mahitaji ya wanachi.

Aidha Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye maeneo yote ambayo Katibu Mkuu ametembea. Maeneo yaliyopongezwa ni pamoja na Miundombinu hasa barabara, hatua kubwa kwenye fursa na ubora wa elimu, maeneo ya afya na umeme vijijini.

Kamati Kuu iliwaita mawaziri saba kuja kutoa maelezo ya mambo mbalimbali yaliyoibuliwa kwenye ziara hizo za Katibu Mkuu wa CCM. Mawaziri hao ni;-

i). Ndg. Christopher Chiza- Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
ii). Ndg. Shukuru Kawambwa- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iii). Ndg. Celina Kombani - Waziri wa Utumishi
iv). Ndg. Hawa Ghasia -Waziri wa TAMISEMI
v). Ndg. Abdallah Kigoda- Waziri wa Viwanda na Biashara
vi). Ndg. Mathayo David Mathayo- Waziri wa Mifugo na Uvuvi
vii). Ndg. Saada Mkuya- Naibu Waziri wa Fedha( kwa niaba ya Waziri wa Fedha).
Baada ya maelezo ya kutosha kutoka kwa mawaziri husika, Kamati Kuu iliagiza yafuatayo kwa Serikali;-

1.Kuhusu wakulima wa Pamba
(i). Serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa Pamba nchini.
(ii). Uwepo wa mbegu bora ni muhimu lakini ni vizuri pakawa na ushindani unaozingatia ubora ili kuondoa ukiritimba wa mtengenezaji mmoja, hivyo kusaidia bei kuwa nzuri kwa wakulima. Hata hivyo Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu. Serikali imetakiwa kuangalia upya utaratibu wa kutoza bei ya mbegu ya Quiton kwa dola za kimarekani badala ya pesa ya kitanzania,wakizingatia mbegu hiyo inazalishwa nchini.
(iii).Kamati Kuu imepongeza juhudi za Serikali kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya pamba mjini Shinyanga, hata hivyo imeitaka Serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nyingi nchini.

(iv). Kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa Pamba, Serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wa kilimo hicho cha mkataba ili kuhakikisha kunakuwa na sheria na kanuni zinazosimamia mfumo huo, ili kuwe na haki kwa pande zote mbili. Aidha wakulima wasilazimishwe kufanya kilimo cha mkataba bali waingie kwa hiari yao wenyewe.

2. Kuhusu wakulima wa Korosho.
(i). Pamoja na kuridhishwa na hatua za muda mfupi kwa msimu wa korosho kwa mwaka 2013/2014 ambazo zimesaidia bei na soko kuwa afadhali, bado Kamati Kuu imesisitiza Serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho kwa suluhisho la kudumu kwa kuhakikisha korosho ina banguliwa nchini.

(ii). Serikali imetakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato wanayokatwa wakulima hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima ili kuongeza kipato cha mkulima.

(iii). Serikali pia imetakiwa kuangalia upya mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini ili uwe ni ule wenye tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla badala ya huu wa sasa unaotoa mwanya kwa walaji kujipenyeza.

3. Kuhusu pembejeo za ruzuku
(i). Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza kuwa pamoja na kuendelea na utafiti wa nini kinachotokea kwenye mbolea hiyo ya Minjingu kiasi cha kuleta malalamiko yote hayo, wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa kutumia mbolea wanayoilalamikia ya Minjingu.

(ii). Serikali iangalie utaratibu bora wa kuratibu swala zima la pembejeo za ruzuku ili lifaidishe zaidi wakulima walio wengi badala ya utaratibu wa sasa ambao licha ya kulalamikiwa na wakulima unaotoa mwanya kwa watu wachache kutumia vibaya utaratibu huo kuiibia serikali na wakulima.

4. Kuhusu wakulima wa mahindi.
(i). Pamoja na Serikali kuanza kulipa madai ya wakulima wa mahindi kwa mikoa ya Ruvuma baada ya ziara ya Katibu Mkuu kwenye maeneo hayo, bado serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.

(ii). Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa Serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa.

5. Kuhusu madai mbalimbali ya waalimu.
(i). Kamati Kuu imesisitiza kupandishwa vyeo na kulipwa stahiki zao waalimu ni haki yao ya msingi hivyo lazima itekelezwe bila kuwa na visingizio na ifanyike kwa haki.

(ii). Kamati Kuu imeiagiza Serikali kukamilisha haraka uhakiki wa madai ya waalimu na kuwalipa haki zao zote mapema iwezekanavyo. Lakini Kamati Kuu imeitaka Serikali kuhakikisha madeni haya hayazaliwi tena kwa kuweka mfumo utakao zuia madeni haya kuzaliwa.

(iii). Kuhusu wakuu wa idara mbalimbali wasiotenda haki kwa waalimu, na wale wanaotumia lugha mbaya na za kejeli kwa waalimu wakibainika wachukuliwe hatua mara moja.

(iv). Pamoja na kuwa Serikali inaangalia utaratibu bora wa kuboresha mawasiliano kati ya wizara zinazohusika na kusimamia waalimu, Kamati Kuu imeitaka Serikali jambo hili lifanyike mapema ili kupunguza malalamiko ya waalimu.

6. Kuhusu ubadhirifu kwenye Halmashauri.
(i). Kamati Kuu imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye Halmashauri mbalimbali nchini. Imewataka madiwani wa CCM kuwa wakali na wasiamamie vizuri halmashauri zao kuhakikisha fedha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kupata thamani ya fedha.
(ii). Aidha Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali na kwa haraka kwa wote wanaobainika kufanya ubadhirifu, ili iwe fundisho kwa wengine.

(iii). Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

7. Kuhusu tatizo la Maji nchini.
Kamati Kuu ilipokea taarifa ya tatizo kubwa la maji nchini, ambalo lilijitokeza kila sehemu aliyotembelea Katibu Mkuu. Chama kimeishauri Serikali kuchukua juhudi na mkakati wa makusudi na dharura kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wakudumu tatizo la upatikanaji wa maji nchini.

8. Kuhusu migogoro ya Aridhi, Wafugaji na Wakulima.
Pamoja na kupokea taarifa juu ya migogoro mbalimbali ya wakulima ,wafugaji na wakulima nchini, kamati kuu imepongeza uamuzi wa bunge kuunda Kamati teule ya bunge na uamuzi wa kuiagiza kamati ya kudumu ya bunge ya aridhi, maliasili na mazingira kuchunguza migogoro hii na kutoa mapendekezo juu ya namna bora ya kuimaliza kabisa migogoro hii.

Aidha kamati kuu imeitaka Serikali na wabunge wa CCM kuzijadili kwa makini ripoti hizo na kufikia hitimisho la migogoro hii nchini. Hata hivyo Kamati Kuu imeitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu wachache maeneo makubwa ya aridhi, ambao wameshindwa kuyaendeleza badala yake wanayatumia kuwakodishia wakulima wadogo.

Aidha maagizo yote haya yatatolewa taarifa kwenye Chama mara kwa mara, ili kuwezesha Chama kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010/2015.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
14/12/2013
 
hawa mawaziri je hawajawajibishwa?
Tatizo kwa akili za kichadema mnategemea kama mtu akiwa na mapungufu sehemu fulani basi dawa ni kutimuana,

CCM haiendeshwi kidikteta, mtu akikosea anaulizwa na anaelezwa sehemu aliyokosea ili airekebishe , kama akishindwa kutimiza aliyoagizwa hapo ndio hatua zaidi zitachukuliwa,

Wewe unadhani kubadili mawaziri ndio suluhisho? je akija mwingine ambaye ana mapungufu zaidi? utabadilisha tena?? lini utapata muda wa kujenmga taifa?

JITAMBUE
 
Vipi kuhusu rambi rambi za mwangosi ulizoiba??? Je hiyo ndio demokrasia ya magamba? Kuchangisha pesa za wafiwa na kuzila?? Rudisha kwanza rambi rambi za mwangosi ndio jamii itakuelewa...otherwise tutaendelea kukudharau .
 
Naomba kuelekezwa, hivi mawaziri wanawajibika kamati kuu au serikalini? Is it possible mawaziri wakaitwa na kamati kuu ya CHADEMA au chama kingine chochote kutoa maelezo?
 
Huyu mla rambi rambi ndio" AJITAMBUWE" maana laana inamtafuna. Eti naye kwa magamba ndio gr8 thinker hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha .
 
tulijua tuuuu hamna ubavu wa kuwawajibisha na je haya yote yakiendelea mtawaambiaje watanzania porojo tuuuu ccm hamna utekelezaji huku kwetu kwa maghembe ndo umeme ni masaa 6 kwa siku tena usiku maji ndo ya kusearch kwa password bado mnaitana kupeana posho ovyooooo
 
Lukosi kweli uwezo wako wa kufikiri mdogo sana....sasa jibu si jepesi, CCM wote mafisadi lazima wapeane muda wa kusikilizana na kujieleza kwasababu hakuna msafi anayeweza kumuadabisha mwenzake. Hivi wewe unaamini mzee wa "weka mbali na tembo" anaujasiri wa kuwaadabisha "mizigo" ya kweli katika chama? hao wote mnawaonewa tu, mzigo namba moja kwenye chama chenu ni yule aliyewateua hao.
 
Hivi ccm mpaka leo bado mnafanya maigizo, sasa hayo maigizo mnayofanya kwanza tunajua mna tatizo la rasilimali watu kama ni mawaziri wamebadilishwa mpaka hamna tena watu wakuwapa wenye sifa hata za kufitinika sasa hata mkiwawajibisha mtamuweka nani ? sisi tunasubiri 2015 tuwanyooshe vizuri ndo mtajua kuwa Watanzania hatutaki ujinga tunamaanisha

Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo CCM ni chama cha watanzania wote kwa ajili ya watanzania.

Kufuatana na kero na malalamiko yaliyojitokeza wakati wa ziara ya Katibu mkuu, Kamati kuu imewaita na kuwahoji baadhi ya viongozi ili kutatua matatizo hayo.

Tofauti na Chadema, ambako tungetegemea kusikia ngumi na vitofali, CCM kama ilivyo ada, wanatumia demokrasia na kufuata haki za binadamu,

Soma taarifa hii;
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana mjini Dodoma kwa kikao chake cha kawaida tarehe 13/12/2013. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilipokea taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kwenye baadhi ya mikoa nchini.
Kamati Kuu imepongeza ziara hizo kwa kuwa na mafanikio makubwa na kwa jinsi zilivyoongeza uhai wa Chama na zilivyojishughulisha na mambo na mahitaji ya wanachi.

Aidha Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye maeneo yote ambayo Katibu Mkuu ametembea. Maeneo yaliyopongezwa ni pamoja na Miundombinu hasa barabara, hatua kubwa kwenye fursa na ubora wa elimu, maeneo ya afya na umeme vijijini.

Kamati Kuu iliwaita mawaziri saba kuja kutoa maelezo ya mambo mbalimbali yaliyoibuliwa kwenye ziara hizo za Katibu Mkuu wa CCM. Mawaziri hao ni;-

i). Ndg. Christopher Chiza- Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
ii). Ndg. Shukuru Kawambwa- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iii). Ndg. Celina Kombani - Waziri wa Utumishi
iv). Ndg. Hawa Ghasia -Waziri wa TAMISEMI
v). Ndg. Abdallah Kigoda- Waziri wa Viwanda na Biashara
vi). Ndg. Mathayo David Mathayo- Waziri wa Mifugo na Uvuvi
vii). Ndg. Saada Mkuya- Naibu Waziri wa Fedha( kwa niaba ya Waziri wa Fedha).
Baada ya maelezo ya kutosha kutoka kwa mawaziri husika, Kamati Kuu iliagiza yafuatayo kwa Serikali;-

1.Kuhusu wakulima wa Pamba
(i). Serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa Pamba nchini.
(ii). Uwepo wa mbegu bora ni muhimu lakini ni vizuri pakawa na ushindani unaozingatia ubora ili kuondoa ukiritimba wa mtengenezaji mmoja, hivyo kusaidia bei kuwa nzuri kwa wakulima. Hata hivyo Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu. Serikali imetakiwa kuangalia upya utaratibu wa kutoza bei ya mbegu ya Quiton kwa dola za kimarekani badala ya pesa ya kitanzania,wakizingatia mbegu hiyo inazalishwa nchini.
(iii).Kamati Kuu imepongeza juhudi za Serikali kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya pamba mjini Shinyanga, hata hivyo imeitaka Serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nyingi nchini.

(iv). Kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa Pamba, Serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wa kilimo hicho cha mkataba ili kuhakikisha kunakuwa na sheria na kanuni zinazosimamia mfumo huo, ili kuwe na haki kwa pande zote mbili. Aidha wakulima wasilazimishwe kufanya kilimo cha mkataba bali waingie kwa hiari yao wenyewe.

2. Kuhusu wakulima wa Korosho.
(i). Pamoja na kuridhishwa na hatua za muda mfupi kwa msimu wa korosho kwa mwaka 2013/2014 ambazo zimesaidia bei na soko kuwa afadhali, bado Kamati Kuu imesisitiza Serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho kwa suluhisho la kudumu kwa kuhakikisha korosho ina banguliwa nchini.

(ii). Serikali imetakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato wanayokatwa wakulima hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima ili kuongeza kipato cha mkulima.

(iii). Serikali pia imetakiwa kuangalia upya mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini ili uwe ni ule wenye tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla badala ya huu wa sasa unaotoa mwanya kwa walaji kujipenyeza.

3. Kuhusu pembejeo za ruzuku
(i). Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza kuwa pamoja na kuendelea na utafiti wa nini kinachotokea kwenye mbolea hiyo ya Minjingu kiasi cha kuleta malalamiko yote hayo, wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa kutumia mbolea wanayoilalamikia ya Minjingu.

(ii). Serikali iangalie utaratibu bora wa kuratibu swala zima la pembejeo za ruzuku ili lifaidishe zaidi wakulima walio wengi badala ya utaratibu wa sasa ambao licha ya kulalamikiwa na wakulima unaotoa mwanya kwa watu wachache kutumia vibaya utaratibu huo kuiibia serikali na wakulima.

4. Kuhusu wakulima wa mahindi.
(i). Pamoja na Serikali kuanza kulipa madai ya wakulima wa mahindi kwa mikoa ya Ruvuma baada ya ziara ya Katibu Mkuu kwenye maeneo hayo, bado serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.

(ii). Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa Serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa.

5. Kuhusu madai mbalimbali ya waalimu.
(i). Kamati Kuu imesisitiza kupandishwa vyeo na kulipwa stahiki zao waalimu ni haki yao ya msingi hivyo lazima itekelezwe bila kuwa na visingizio na ifanyike kwa haki.

(ii). Kamati Kuu imeiagiza Serikali kukamilisha haraka uhakiki wa madai ya waalimu na kuwalipa haki zao zote mapema iwezekanavyo. Lakini Kamati Kuu imeitaka Serikali kuhakikisha madeni haya hayazaliwi tena kwa kuweka mfumo utakao zuia madeni haya kuzaliwa.

(iii). Kuhusu wakuu wa idara mbalimbali wasiotenda haki kwa waalimu, na wale wanaotumia lugha mbaya na za kejeli kwa waalimu wakibainika wachukuliwe hatua mara moja.

(iv). Pamoja na kuwa Serikali inaangalia utaratibu bora wa kuboresha mawasiliano kati ya wizara zinazohusika na kusimamia waalimu, Kamati Kuu imeitaka Serikali jambo hili lifanyike mapema ili kupunguza malalamiko ya waalimu.

6. Kuhusu ubadhirifu kwenye Halmashauri.
(i). Kamati Kuu imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye Halmashauri mbalimbali nchini. Imewataka madiwani wa CCM kuwa wakali na wasiamamie vizuri halmashauri zao kuhakikisha fedha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kupata thamani ya fedha.
(ii). Aidha Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali na kwa haraka kwa wote wanaobainika kufanya ubadhirifu, ili iwe fundisho kwa wengine.

(iii). Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

7. Kuhusu tatizo la Maji nchini.
Kamati Kuu ilipokea taarifa ya tatizo kubwa la maji nchini, ambalo lilijitokeza kila sehemu aliyotembelea Katibu Mkuu. Chama kimeishauri Serikali kuchukua juhudi na mkakati wa makusudi na dharura kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wakudumu tatizo la upatikanaji wa maji nchini.

8. Kuhusu migogoro ya Aridhi, Wafugaji na Wakulima.
Pamoja na kupokea taarifa juu ya migogoro mbalimbali ya wakulima ,wafugaji na wakulima nchini, kamati kuu imepongeza uamuzi wa bunge kuunda Kamati teule ya bunge na uamuzi wa kuiagiza kamati ya kudumu ya bunge ya aridhi, maliasili na mazingira kuchunguza migogoro hii na kutoa mapendekezo juu ya namna bora ya kuimaliza kabisa migogoro hii.

Aidha kamati kuu imeitaka Serikali na wabunge wa CCM kuzijadili kwa makini ripoti hizo na kufikia hitimisho la migogoro hii nchini. Hata hivyo Kamati Kuu imeitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu wachache maeneo makubwa ya aridhi, ambao wameshindwa kuyaendeleza badala yake wanayatumia kuwakodishia wakulima wadogo.

Aidha maagizo yote haya yatatolewa taarifa kwenye Chama mara kwa mara, ili kuwezesha Chama kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010/2015.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
14/12/2013
 
katika post yangu 'Waziri Mkuu aitia Kitanzini CCM' nilieleza kuwa ningeshangaa kama watamfukuza waziri mkuu.sijui kwa nini ccm inafanya mambo kwa makusudi yanayoingamiza.kwa mfano Kinana akiwa Bunda alimpatia miezi sita waziri wa elimu awe amelipa madeni ya walimu,lakini miezi hiyo inakaribia kuisha hakuna chochote.kwa nini asinyamaza ili madhara yasiwe makubwa hivi.
 
Pumba express.
Nasikia babu yako kaahidi kutengeneza gongo akichaguliwa 2015

Yaani katika masuala yote muhimu ya nchi yeye na akili zake kaona gongo ndio suala la maana?

Kweli nimeamini Chadema inaongozwa kwa nguvu za viroba
 
Kwa hiyo Kikwete wa CCM kamwagiza Kikwete aliyepo serikalini atekeleze ngonjera za miaka yote !? Katika hayo kwako lipi jipya ambalo halijawahi AGIZWA!
 
Tatizo kwa akili za kichadema mnategemea kama mtu akiwa na mapungufu sehemu fulani basi dawa ni kutimuana,

CCM haiendeshwi kidikteta, mtu akikosea anaulizwa na anaelezwa sehemu aliyokosea ili airekebishe , kama akishindwa kutimiza aliyoagizwa hapo ndio hatua zaidi zitachukuliwa,

Wewe unadhani kubadili mawaziri ndio suluhisho? je akija mwingine ambaye ana mapungufu zaidi? utabadilisha tena?? lini utapata muda wa kujenmga taifa?

JITAMBUE

Mkuu Chadema ipi unayozungumzia Chdema asili au Chadema family, chadema chumbani au Sebuleni?
mkuu kuwawajibisha sio lazima kuwafukuza hadi kufikia kuitwa na KK lazima kuna mapungufu sasa ni hatua zipi zimechukuliwa dhidi yao
 
Naomba kuelekezwa, hivi mawaziri wanawajibika kamati kuu au serikalini? Is it possible mawaziri wakaitwa na kamati kuu ya CHADEMA au chama kingine chochote kutoa maelezo?

kweli wewe ni bavicha,hujui kuwa serikali yote inatekeleza sera za ccm?wenye serikali ni ccm,wana wajibu kuwaita watendaji ktk nafasi za uwaziri kuhoji utendaji,chadema au cuf wakiuza sera wananchi wakawbmini nao watakua na haki kuhoji watendaji,ccm sasa imepata viongozi,hongera kinana
 
Huu ni upuuzi mkubwa sana kuacha kuwashughulikia wazembe kwa misingi ya kuleana na kulindana. Kama hawa mawaziri wameshindwa kutekeleza wajibu wao basi wawajike au wawajibishwe. Lakini kama alivyosema Dr Lwaitama CCM haina ubavu wa kuwajibishana kama ambavyo inafanya CHADEMA.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
CCM mlishindwa kung'oa shina la mchicha (madiwani) ndio mtaweza mbuyu(mawaziri).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom