Tofauti na CHADEMA, CCM ukikosea unapewa nafasi ya kujieleza, soma yanayojiri Dodoma

Nasikia babu yako kaahidi kutengeneza gongo akichaguliwa 2015

Yaani katika masuala yote muhimu ya nchi yeye na akili zake kaona gongo ndio suala la maana?

Kweli nimeamini Chadema inaongozwa kwa nguvu za viroba

Kweli lukosi leo ndo nimejirizisha kwamba wewe ni mweupe kuliko karatasi, kwahiyo hapo ndo umetueleza nini? kulinda ufisadi, hivi hata wewe kwakiwango chako hicho cha secondary unakubaliana na mtazamo kama ule wa watu wa epa walioiba wakaambiwa warudishe hela? mpaka leo hawajulikani ni akina nani, wengine wanaiba hapa wanahamishiwa kwingine, kulindana lindana ndo sera yenu, wewe bila shaka hayo mabox yameshakuzuru haiwezekani ukaleta kitu kama hiki hapa.
 
Tatizo kwa akili za kichadema mnategemea kama mtu akiwa na mapungufu sehemu fulani basi dawa ni kutimuana,

CCM haiendeshwi kidikteta, mtu akikosea anaulizwa na anaelezwa sehemu aliyokosea ili airekebishe , kama akishindwa kutimiza aliyoagizwa hapo ndio hatua zaidi zitachukuliwa,

Wewe unadhani kubadili mawaziri ndio suluhisho? je akija mwingine ambaye ana mapungufu zaidi? utabadilisha tena?? lini utapata muda wa kujenmga taifa?

JITAMBUE
Uraibu wa wa dawa za kulevya km Bangi,Konyagi,mandrax nk.ni kitu kibaya kuliko ujinga wa aina yeyote.(Kwa niaba yako nitamuomba yule aliye Gharimia matibabu ya RayC agharimie matibabu yako pia) Kama sio ulevi, kwa elimu yako uliyoipata nyumbani na ughaibuni ulitarajiwa kusema jambo baada ya kufanya utafiti. Laiti ungefanya utafiti ungeweza kugundua kuwa, J.s.Malichela,Kolimba, Jumbe,Seif sharif. Hamad Rashidi na wengine pia walichukuliwa hatua mara moja na kuifanya CCM ya wakati huo kusonga mbele vizuri.

Kwa tabia ya CCM ya leo kuwavumilia waizi na Mafisadi ndio maana chama chenu leo kinalazimika kuomba radhi kwa niaba ya Chenge, Lowasa na wahuni wengine wa kisiasa walioko CCM. na hii ndiyo tofauti kati ya Chadema na CCM kwamba kila kukicha ccm inabomoka na CHADEMA inaimarika.
 
Kilikuwa kikao cha kulipana posho tu kwani hamna la maana zaidi ya "upuuzi" wa kila siku.

Hii nchi kuendekea ni mpaka CCM watoke madarakani.
 
Mmmh, chama changu ni kiboko.

Hivi, hayo ambayo katibu mkuu Kanali Abdulrahman Kinana na Sekretariati yake wameyawasilisha kwenye CC km ugunduzi wao kwenye ziara si ni mambo yale yale ambayo wabunge na wananchi wanayalalamikia na kugoma(waalimu) na kuandamana (wakulima wa koro na pamba)?

Nafikiri kwa hali hii naamini nchi inanihitaji zaidi na lazima nitoe azimio langu juu ya hatma ya nchi na wananchi wangu hivi karibuni.
 
Kwenye kikao walikumbuka kumuuliza Kinana ni tembo wangapi keshaua?
Na ile meli vp ni yake kweli?
Walisahau kumwambia kuwa atupe maelezo hayo kwanza kabla hajawaza mambo ya mawaziri mizigo maana hata yeye ametulemea watanzania, ni Mzigo.

Kwenye kikao wangeikumbusha serikali kuwa kuna ardhi ya tanzania ambayo ukiingia unaambiwa 'karibu falme za kiarabu' Waikumbushe kuwa sisi mbona hatujapata mgao wetu?

Pia sidhani kama walikumbuka kuuliza kuwa vp kuhusu nyumba za viongozi? Mawaziri wataishi hoteli hadi lini? Ni mzigo kwetu.

Pia kwenye kikao mngemkumbusha mwenyekiti kuwa kupandisha bei ya Umeme kila wakati si tiba kwa Tanesco kujiendesha, mngemwambia kuwa sio sisi tu tunaounga mkono mageuzi tutakaolala giza bali hata Magamba wenzie wanataabika huku mtaani!.

Pia sidhani kama mlimwambia mwenyekiti amtake CHAWENE atutake radhi kwa kauli zake za kashfa na kejeli kwetu, ajue kuwa alipo ni pa kawaida tu asitutusi!
Siku nyingine avae kwanza akili zake ndio aongee!!
 
CCM siyo madikiteta kama CDM Saccos, lazima watu Mawaziri wapewe nafasi ya kujieleza kwanza, CCM ni taasisi na siyo chama cha ukoo!
 
Kolimba alipewa nafasi kuhijiwa siyo? Imrani Kombe ndiyo alihojiwa vya kutosha hadi akafananishwa na Jambazi lisilo na Silaha.
 
Wababaishaji wamewasifu wawekezaji wao wa pembe za ndovu kama jinsi alivyo katibu wao, ona hapa

(iii).Kamati Kuu imepongeza
juhudi za Serikali kuvutia
wawekezaji kwenye viwanda
vya pamba mjini Shinyanga,
hata hivyo imeitaka Serikali
kuangalia upya urasimu katika
uwekezaji wa viwanda nchini
hasa vinavyoongeza thamani ya
mazao na kutoa ajira nyingi
nchini.

Muwekezaji huyo ni yule mchina aliyecheza kiduku kwa kofia ya ubalozi na kuvunja mkataba wa Vienna

kwa taarifa hii maana yake ni kwamba kamati kuu ilibariki mchina yule kuvunja mkataba wa Vienna.
 
CCM siyo madikiteta kama CDM Saccos, lazima watu Mawaziri wapewe nafasi ya kujieleza kwanza, CCM ni taasisi na siyo chama cha ukoo!
Miaka 52 Ccm kuhojiana, kazi za kuwatumika Watanzania mtafanya mkiwa kaburini, mtu ameharibu na kurudusha nchi nyuma unamuita kumuomba maelezo, yaani hii iko ndani ya chama cha familia Ccm, hakafu cheo chenyewe ni cha kupewa na Rais, Ccm mnakotupeleka siko, hamjui mfanyalo.
 
Tofauti kati ya Chadema na CCM, ni kwamba Chadema wanaweza kumwajibisha kada yoote at any time. Lakini CCM wanageresha hapo kisha wanawasamehe. Ndio maana hata magamba yaliwashinda kuvua.
 
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo CCM ni chama cha watanzania wote kwa ajili ya watanzania.

Kufuatana na kero na malalamiko yaliyojitokeza wakati wa ziara ya Katibu mkuu, Kamati kuu imewaita na kuwahoji baadhi ya viongozi ili kutatua matatizo hayo.

Tofauti na Chadema, ambako tungetegemea kusikia ngumi na vitofali, CCM kama ilivyo ada, wanatumia demokrasia na kufuata haki za binadamu,

Soma taarifa hii;
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana mjini Dodoma kwa kikao chake cha kawaida tarehe 13/12/2013. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.


Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilipokea taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kwenye baadhi ya mikoa nchini.
Kamati Kuu imepongeza ziara hizo kwa kuwa na mafanikio makubwa na kwa jinsi zilivyoongeza uhai wa Chama na zilivyojishughulisha na mambo na mahitaji ya wanachi.


Aidha Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye maeneo yote ambayo Katibu Mkuu ametembea. Maeneo yaliyopongezwa ni pamoja na Miundombinu hasa barabara, hatua kubwa kwenye fursa na ubora wa elimu, maeneo ya afya na umeme vijijini.


Kamati Kuu iliwaita mawaziri saba kuja kutoa maelezo ya mambo mbalimbali yaliyoibuliwa kwenye ziara hizo za Katibu Mkuu wa CCM. Mawaziri hao ni;-


i). Ndg. Christopher Chiza- Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
ii). Ndg. Shukuru Kawambwa- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iii). Ndg. Celina Kombani - Waziri wa Utumishi
iv). Ndg. Hawa Ghasia -Waziri wa TAMISEMI
v). Ndg. Abdallah Kigoda- Waziri wa Viwanda na Biashara
vi). Ndg. Mathayo David Mathayo- Waziri wa Mifugo na Uvuvi
vii). Ndg. Saada Mkuya- Naibu Waziri wa Fedha( kwa niaba ya Waziri wa Fedha).
Baada ya maelezo ya kutosha kutoka kwa mawaziri husika, Kamati Kuu iliagiza yafuatayo kwa Serikali;-


1.Kuhusu wakulima wa Pamba
(i). Serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa Pamba nchini.
(ii). Uwepo wa mbegu bora ni muhimu lakini ni vizuri pakawa na ushindani unaozingatia ubora ili kuondoa ukiritimba wa mtengenezaji mmoja, hivyo kusaidia bei kuwa nzuri kwa wakulima. Hata hivyo Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu. Serikali imetakiwa kuangalia upya utaratibu wa kutoza bei ya mbegu ya Quiton kwa dola za kimarekani badala ya pesa ya kitanzania,wakizingatia mbegu hiyo inazalishwa nchini.
(iii).Kamati Kuu imepongeza juhudi za Serikali kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya pamba mjini Shinyanga, hata hivyo imeitaka Serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nyingi nchini.


(iv). Kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa Pamba, Serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wa kilimo hicho cha mkataba ili kuhakikisha kunakuwa na sheria na kanuni zinazosimamia mfumo huo, ili kuwe na haki kwa pande zote mbili. Aidha wakulima wasilazimishwe kufanya kilimo cha mkataba bali waingie kwa hiari yao wenyewe.


2. Kuhusu wakulima wa Korosho.
(i). Pamoja na kuridhishwa na hatua za muda mfupi kwa msimu wa korosho kwa mwaka 2013/2014 ambazo zimesaidia bei na soko kuwa afadhali, bado Kamati Kuu imesisitiza Serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho kwa suluhisho la kudumu kwa kuhakikisha korosho ina banguliwa nchini.


(ii). Serikali imetakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato wanayokatwa wakulima hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima ili kuongeza kipato cha mkulima.


(iii). Serikali pia imetakiwa kuangalia upya mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini ili uwe ni ule wenye tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla badala ya huu wa sasa unaotoa mwanya kwa walaji kujipenyeza.


3. Kuhusu pembejeo za ruzuku
(i). Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza kuwa pamoja na kuendelea na utafiti wa nini kinachotokea kwenye mbolea hiyo ya Minjingu kiasi cha kuleta malalamiko yote hayo, wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa kutumia mbolea wanayoilalamikia ya Minjingu.


(ii). Serikali iangalie utaratibu bora wa kuratibu swala zima la pembejeo za ruzuku ili lifaidishe zaidi wakulima walio wengi badala ya utaratibu wa sasa ambao licha ya kulalamikiwa na wakulima unaotoa mwanya kwa watu wachache kutumia vibaya utaratibu huo kuiibia serikali na wakulima.


4. Kuhusu wakulima wa mahindi.
(i). Pamoja na Serikali kuanza kulipa madai ya wakulima wa mahindi kwa mikoa ya Ruvuma baada ya ziara ya Katibu Mkuu kwenye maeneo hayo, bado serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.


(ii). Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa Serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa.


5. Kuhusu madai mbalimbali ya waalimu.
(i). Kamati Kuu imesisitiza kupandishwa vyeo na kulipwa stahiki zao waalimu ni haki yao ya msingi hivyo lazima itekelezwe bila kuwa na visingizio na ifanyike kwa haki.


(ii). Kamati Kuu imeiagiza Serikali kukamilisha haraka uhakiki wa madai ya waalimu na kuwalipa haki zao zote mapema iwezekanavyo. Lakini Kamati Kuu imeitaka Serikali kuhakikisha madeni haya hayazaliwi tena kwa kuweka mfumo utakao zuia madeni haya kuzaliwa.


(iii). Kuhusu wakuu wa idara mbalimbali wasiotenda haki kwa waalimu, na wale wanaotumia lugha mbaya na za kejeli kwa waalimu wakibainika wachukuliwe hatua mara moja.


(iv). Pamoja na kuwa Serikali inaangalia utaratibu bora wa kuboresha mawasiliano kati ya wizara zinazohusika na kusimamia waalimu, Kamati Kuu imeitaka Serikali jambo hili lifanyike mapema ili kupunguza malalamiko ya waalimu.


6. Kuhusu ubadhirifu kwenye Halmashauri.
(i). Kamati Kuu imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye Halmashauri mbalimbali nchini. Imewataka madiwani wa CCM kuwa wakali na wasiamamie vizuri halmashauri zao kuhakikisha fedha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kupata thamani ya fedha.
(ii). Aidha Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali na kwa haraka kwa wote wanaobainika kufanya ubadhirifu, ili iwe fundisho kwa wengine.


(iii). Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.


7. Kuhusu tatizo la Maji nchini.
Kamati Kuu ilipokea taarifa ya tatizo kubwa la maji nchini, ambalo lilijitokeza kila sehemu aliyotembelea Katibu Mkuu. Chama kimeishauri Serikali kuchukua juhudi na mkakati wa makusudi na dharura kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wakudumu tatizo la upatikanaji wa maji nchini.


8. Kuhusu migogoro ya Aridhi, Wafugaji na Wakulima.
Pamoja na kupokea taarifa juu ya migogoro mbalimbali ya wakulima ,wafugaji na wakulima nchini, kamati kuu imepongeza uamuzi wa bunge kuunda Kamati teule ya bunge na uamuzi wa kuiagiza kamati ya kudumu ya bunge ya aridhi, maliasili na mazingira kuchunguza migogoro hii na kutoa mapendekezo juu ya namna bora ya kuimaliza kabisa migogoro hii.


Aidha kamati kuu imeitaka Serikali na wabunge wa CCM kuzijadili kwa makini ripoti hizo na kufikia hitimisho la migogoro hii nchini. Hata hivyo Kamati Kuu imeitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu wachache maeneo makubwa ya aridhi, ambao wameshindwa kuyaendeleza badala yake wanayatumia kuwakodishia wakulima wadogo.


Aidha maagizo yote haya yatatolewa taarifa kwenye Chama mara kwa mara, ili kuwezesha Chama kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010/2015.


Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
14/12/2013


AS USUAL YOU DO HAVE SHORT MEMORY... Haufai kuwa Mwanasiasa utaua wengi...
Hauikumbuki Habari hii na uliichangia na kupongeza kwa Madoido ya AINA


MANSOOR afukuzwa CCM

Mansoor Yussuf Himidi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimemeguka baada ya Kamati Maalumu kumvua uanachama Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansoor Yussuf Himid, akidaiwa kukiuka maadili ya chama hicho. Uamuzi huo umekuja baada ya Mansoor kudaiwa kupingana na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayoamini katika muundo wa Serikali mbili.
Chanzo cha kuaminika kutoka katika kamati hiyo, kiliiambia MTANZANIA jana kuwa uamuzi wa kumvua uanachama Mansoor uliwasilishwa katika kikao kilichofanyika CCM Kisiwandui chini ya Makamu Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansoor zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, 2013 katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambapo wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfuta uanachama mwakilishi huyo.
Dk. Shein ndiye aliyeongoza kikao cha Kamati ya Maadili, huku wajumbe wakiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mohamed Hija, Mbaruk Rashid Omari na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd.
Chanzo hicho kutoka ndani ya CCM Zanzibar, kilisema tuhuma za Mansoor zilizowasilishwa zilikuwa tatu, huku ya kwanza ikiwa ni kushindwa kusimamia malengo, madhumuni na masharti ya chama.
Aidha, Mansoor anadaiwa kutokusimamia wajibu wa mwanachama kwa kukiuka maadili ya kiongozi wa CCM, kwa kukiuka Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa suala la kufukuzwa uanachama kwa mwakilishi huyo lilizua mjadala mzito katika kikao cha jana, lakini baadaye wajumbe walikubaliana kwa kauli moja kufukuzwa kwake.
Mansoor amekuwa miongoni mwa Wazanzibari walio katika safu ya mbele kutetea muundo wa Muungano utakaoipa Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa suala la mwakilishi huyo kutakiwa kuwasilisha utetezi dhidi ya tuhuma zake, lilianzia katika kikao cha CCM Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo alisema kama kufungwa afungwe lakini atasimamia Muungano wa mkataba pamoja na mamlaka kamili.
“Katika kikao cha mkoa alitoa utetezi wake na kusema kama kufungwa afungwe, kama kunyongwa anyongwe na kama kufukuzwa afukuzwe, lakini anataka Serikali ya mkataba.
“Wakati anatoa utetezi wake, Mansoor, alikuwa anatumia nakala moja ya gazeti la wiki la Julai 26, mwaka huu na kumtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, kuwa naye anavunja Katiba ya CCM,” kilisema chanzo hicho.
Kutokana na misimamo yake, Mansoor, anaaminika zaidi kwa Wazanzibari hususani wale wanaoamini katika Muungano wa mkataba pamoja na madaraka kamili ya dola ya Zanzibar.
MTANZANIA ilipomtafuta Msemaji wa CCM upande wa Zanzibar, Waride Bakari Jabu, atoe ufafanuzi wa suala hilo, alisema yupo katika kikao.
“Kwa sasa siwezi kusema jambo lolote mwanangu, nafikiri unasikia sauti za wajumbe wakizungumza, nipo katika kikao na siwezi kusema jambo lolote kwa sasa,” alijibu kwa kifupi Waride.
Historia yake
Katika uchaguzi wa mwaka 2005, Mansoor, alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Kiembesamaki kupitia CCM, nafasi ambayo amedumu nayo hadi sasa.
Pia ni mwanachama wa CCM aliyewahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Halmashauri Kuu (NEC) na Mweka Hazina wa CCM upande wa Zanzibar kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2012.
Nje ya CCM, ameshika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Mwaka 2000 hadi mwaka 2004, alikuwa Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, na kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2010 alikuwa waziri kamili katika wizara hiyo na baadaye mwaka 2010 hadi mwaka 2012, alikuwa Waziri wa Kilimo na Rasilimali.
Aidha, alihudumu kama mjumbe wa Baraza la Biashara la Zanzibar kati ya mwaka 2002 hadi 2012.
Kutokana na misimamo yake ndani na nje ya chama na Serikali, Oktoba 15, 2012, Dk. Shein ilimlazimu kufuta uteuzi wake kwa Mansoor kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Mansoor ni mwanasiasa na mfanyabiashara aliyezaliwa Novemba 3, 1967 kisiwani Unguja. Alisoma masomo yake ya msingi na sekondari nchini India kati ya mwaka 1976 na 1987.
Kabla ya kuingia rasmi katika siasa mwaka 2000, aliteuliwa kuwa mjumbe katika Baraza la Wawakilishi na alijihusisha katika biashara ya hoteli.
Mwanasiasa huyo ni mtoto wa Mkuu wa Kwanza wa Jeshi la Zanzibar baada ya Mapinduzi, Brigedia Jenerali Yussuf Himid.
Amekuwa akisimamia maridhiano ya Wazanzibari na Umoja wa Kitaifa akiwa mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano aliyoshiriki kikamilifu kuyaanzisha mwaka 2009.
Pia ni miongoni mwa Wazanzibari walio mstari wa mbele kutetea muundo wa Muungano, utakaoipa Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Mwenyekiti Hassan Nassor Moyo (CCM), Eddie Riyami (CCM), Abubakar Khamis Bakari (CUF), Ismail Jussa Ladhu (CUF) na Salim Bimani (CUF).
 
Tatizo kwa akili za kichadema mnategemea kama mtu akiwa na mapungufu sehemu fulani basi dawa ni kutimuana,

CCM haiendeshwi kidikteta, mtu akikosea anaulizwa na anaelezwa sehemu aliyokosea ili airekebishe , kama akishindwa kutimiza aliyoagizwa hapo ndio hatua zaidi zitachukuliwa,

Wewe unadhani kubadili mawaziri ndio suluhisho? je akija mwingine ambaye ana mapungufu zaidi? utabadilisha tena?? lini utapata muda wa kujenmga taifa?

JITAMBUE

hoja yako dhaifu sana mkuu, Samahani lakini.
 
Tatizo kwa akili za kichadema mnategemea kama mtu akiwa na mapungufu sehemu fulani basi dawa ni kutimuana,

CCM haiendeshwi kidikteta, mtu akikosea anaulizwa na anaelezwa sehemu aliyokosea ili airekebishe , kama akishindwa kutimiza aliyoagizwa hapo ndio hatua zaidi zitachukuliwa,

Wewe unadhani kubadili mawaziri ndio suluhisho? je akija mwingine ambaye ana mapungufu zaidi? utabadilisha tena?? lini utapata muda wa kujenmga taifa?

JITAMBUE

Swali moja kwako bwana Lukosi, Je wale waliokuwa wanapiga kelele kwenye majukwaa na kuwambia watu kuwa mawaziri fulani na fulani ni mzigo kabla hata hao mawaziri hawajasikilizwa watachukuliwa hatua gani? Hizi ndizo aina ya siasa zilizojaa ndani ya CCM watu wanatafuta umaaarufu kwenye majukwaa bila hata ya kufanya chembe ya utafiti. Kwa hakika hakuna cha kusifia kwenye uamuzi wa KK ya CCM kwani wenye akili timamu tulitarajia maamuzi hayo. Serikali haiendeshwi kwa siasa za majukwaani. Hao watendaji wenu wa chama wajitafakari
 
CCM siyo madikiteta kama CDM Saccos, lazima watu Mawaziri wapewe nafasi ya kujieleza kwanza, CCM ni taasisi na siyo chama cha ukoo!

Kwahiyo CCM ilipomfukuza UANACHAMA wa CCM Mwakilishi Mohamed Mansoor wa KIEMBESAMAKI hakupewa nafasi ya kujitetea kwasababu ilionekana ana UKOO ndani ya CCM ?

Kwahiyo NAPE NNAUYE Katibu Mwenezi wa CCM na MOSES NNAUYE Katibu Mwenezi Miaka ya sabini sio NDUGU cheo kimoja na jina la mwisho moja lakini sio UKOO Mmoja --- CCM haina LUPANGO!!!

Au, NCHI YENYE Madaktari Wabunge 15 hakuna anayefaa zaidi ya MTOTO wa RAIS ALI HASSAN MWINYI kuwa WAZIRI wa AFYA ?

Lakini tunakiona CHADEMA pekee ndio chama cha UKOO!!! sisi hatuna DHAMBI sababu tunasema Ukweli ni CHADEMA ndicho CHAMA CHA UKOO na SIO KIPENZI cha WANANCHI CCM...

Yeah... Kwenye MKUTANO MKUU Uchaguzi wa RAIS ni kutumia a BALLOT na sio WHO's WHO hata MKAPA MWINYI na KIKWETE hawakupigiwa ndogondogo na Makundi ndani ya chama... NDIO MAANA aliyekuwa na kura NYINGI Salim Ahmed Salim hakuchaguliwa sababu hakuweza kujitetea vizuri kisiasa...
 

Kwahiyo CCM ilipomfukuza UANACHAMA wa CCM Mwakilishi Mohamed Mansoor wa KIEMBESAMAKI hakupewa nafasi ya kujitetea kwasababu ilionekana ana UKOO ndani ya CCM ?

Kwahiyo NAPE NNAUYE Katibu Mwenezi wa CCM na MOSES NNAUYE Katibu Mwenezi Miaka ya sabini sio NDUGU cheo kimoja na jina la mwisho moja lakini sio UKOO Mmoja --- CCM haina LUPANGO!!!

Au, NCHI YENYE Madaktari Wabunge 15 hakuna anayefaa zaidi ya MTOTO wa RAIS ALI HASSAN MWINYI kuwa WAZIRI wa AFYA ?

Lakini tunakiona CHADEMA pekee ndio chama cha UKOO!!! sisi hatuna DHAMBI sababu tunasema Ukweli ni CHADEMA ndicho CHAMA CHA UKOO na SIO KIPENZI cha WANANCHI CCM...

Yeah... Kwenye MKUTANO MKUU Uchaguzi wa RAIS ni kutumia a BALLOT na sio WHO's WHO hata MKAPA MWINYI na KIKWETE hawakupigiwa ndogondogo na Makundi ndani ya chama... NDIO MAANA aliyekuwa na kura NYINGI Salim Ahmed Salim hakuchaguliwa sababu hakuweza kujitetea vizuri kisiasa...

Mkuu umepiga chini ya mkanda!!!!
 
Tatizo kwa akili za kichadema mnategemea kama mtu akiwa na mapungufu sehemu fulani basi dawa ni kutimuana,

CCM haiendeshwi kidikteta, mtu akikosea anaulizwa na anaelezwa sehemu aliyokosea ili airekebishe , kama akishindwa kutimiza aliyoagizwa hapo ndio hatua zaidi zitachukuliwa,

Wewe unadhani kubadili mawaziri ndio suluhisho? je akija mwingine ambaye ana mapungufu zaidi? utabadilisha tena?? lini utapata muda wa kujenmga taifa?

JITAMBUE
Haikutarajiwa kwa mtu anayetambua asilimia kubwa ya kamati kuu ya ccm kuwa ni ya dini gani halafu tarajie waziri ghasia au kawambwa kuondolewa pamoja na uozo wao wote. Hivi kweli ccm hamkujua kuwa walimu hawapandishwi madaraja kwa wakati mpaka mlipojitengenezea per diem?
 
CCM ya Kinana hakuna mfano wake! Kwa hakika umeweza sana Kibana!

Viva CCM viva Kinana

yaani kama nakuona ,, unavo tuma hii post huku kimoyomoyo roho inakusuta kwa unafiki wa kupaka kinyesi manukato ukidhani utaondoa harufu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom