johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,779
- 141,667
Wakati CCM wanayo sekretarieti ya uchumi na fedha ambayo husimamia na kuratibu mapato na matumizi ya chama wakifuatiliwa kwa karibu na Katibu Mkuu, kule CHADEMA mambo ni tofauti.
Ofisi za Ufipa mapato na matumizi yote husimamiwa na Mwenyekiti huku kumbukumbu za nyaraka zikitunzwa na mhazini hivyo kufanya kanuni za kitaaluma za kiuhasibu kuwa ngumu kutekelezeka.
Ingependeza kama Mhazini wa CHADEMA akapitia pale Lumumba apate kozi fupi ya usimamizi wa fedha za chama vinginevyo kuna siku ataozea Segerea.
Najua TAKUKURU wameshaanza kupita pita hapo ofisi kuu Ufipa so natoa tu angalizo. Mwisho kabisa wana CHADEMA muanze kujiandaa kisaikolojia lolote linaweza kutokea maana matumizi mabaya ya ruzuku ni uhujumu uchumi.
Niishie hapo!