Ni kweli timu zote mbili kwa hivi sasa zinaendeshwa na wawekezaji wenye malengo binafsi zaidi tofauti na hapo awali walipokuwa pembeni wakisaidia kama wafadhili. Lakini ukifanya tathimini zaidi utagundua kuwa timu hizi mbili ambazo ni kubwa hapa nchini zina malengo tofauti kwa sasa katika uendeshaji wake;-
- Wakati viongozi Simba wanawekeza zaidi katika kujenga Club ya mafanikio uwanjani. Viongozi wa Yanga akili yao ipo katika kutengeneza pesa zaidi kwa sasa kwa kujitangaza kupitia rasilimali za Club kadiri zinapokuwepo kama "'Jersey'' n.k
- Wakati Simba wanafikiria kuboresha utawala mzima wa Club ili kuweza kufikia malengo ya kuwa na Club kubwa na bora zaidi ya mpira wa miguu pamoja na michezo mingine huko mbeleni. Wenzao wa Yanga wanahangaika kuhakikisha kuwa kila anayeingia Yanga awe mchezaji au kiongozi lengo liwe ni kutengeneza pesa ya haraka haraka kupitia mauzo ya ''merchandise'' za club kama jersey kwa lengo la kurudisha pesa ya wawekezaji upesi.
- Wakati Simba wakisajili wachezaji kwa lengo la kuimarisha timu zaidi mbeleni wenzao wa Yanga wameangalia zaidi wachezaji wanaoweza kuwaletea mafanikio ya haraka haraka kwa sasa ili kutengeneza pesa upesi upesi. .
- Wakati wanachama na wapenzi wa SIMBA wamekuwa makini katika kufuatilia na kuhoji nini kinachofanyika ndani ya Club ili kuweza kufikia malengo upande wa pili yaani Yanga, wao wapo kimya na hii kwao sio agenda.
- Wakati Simba wakiwaza kubeba kombe la Club Bingwa Africa na kuwa kati ya timu tano (5) bora za Africa muda woote. Wenzao wa Yanga wanawaza kuwafunga Simba na kutwaa ubingwa wa Tanzania