Tofauti kati ya Wanamuziki wa BONGO FLEVA/TZ, wa Kenya na Uganda

NGULI

NGULI

JF-Expert Member
4,811
1,225
Wakuu wasalaamu,

Ni J5 tulivu kabisa naomba tujadili kwa nini wanamuziki wetu hasa wa bongo fleva wana hit ila hawana mafanikio mazuri ya kiuchumi ukilanganisha na majirani zetu kenya na uganda.

Wanamuziki wa kizazi kipya/Bongo Fleva walimkapeni rais Kikwete na hatimae akashinda kwa kishindo, aliposhinda aliwaalika ikulu akawauliza mnataka serikali au mimi niwafanyie nini? Kwa pamoja wakaomba studio,Tayari hio ilikuwa wrong move opportunity kubwa kama hio mnaomba studio?. Kwani hapa nchini hakuna studio? mbona mnasafiri hadi Kenya kwa Ogopa Dejays na US kurecord? na hata Studio ilivyokuja wakazungukwa na wazee wa fursa.

Pia wenyewe kwa wenyewe wanamakundi kama ccm (mafisadi na wazawa) na cdm (Family na Asilia), kuna kundi la kina JD na kundi lililoolewa na clouds kuna venaga sijui na kina nani. Kuna wabana pua na waachia pua. Na wote hawa hawana common understanding.

Wakenya nao walifanya hivyo hivyo ku campaing Mwai Kibaki na Uhuru wao walivyoulizwa mnataka nini walikuwa sawa na wenzao wa Kenya kuwa wakifanya biashara au kuagiza bidhaa yoyote kutoka nje ya nchi ziwe duty free ili kunyanyua kipato chao. Pia serikali iwagaie maeneo (estate) kwa ajili ya kujenga nyumba za kuendana na hadhi zao na hata kufanya kilimo cha kisasa.

The way forward,

Wa bongo fleva mpunguze bangi au madawa ya kulevya au muuache kabisa kwa vile yanapunguza uwezo wenu wa kufikiri na wengi baada ya hit moja mnachoka kabisa na kuwa mateja e.g TID, Daz baba etc waliokufa RIP.

Pia jitahidi kusoma maendeleo ya wenzenu jifunzeni kujitegemea na kuwa na ma-manager kweli kweli wenye ujuzi na elimu na sio walamba midomo waendesha vipindi vya radio.
 
Boflo

Boflo

JF-Expert Member
4,390
1,225
Safi sana Nguli umewachana kisawa sawa walamba midomo
 
Asprin

Asprin

JF-Expert Member
61,366
2,000
Waliomba kujengewa studio, wakajengewa kina Ruge.

Bongofleva bangi zinawaharibu. Uzuri wakiharibika, mkulu anawatafutia tiba. Kama huamini muulize Ray C.
 
NGULI

NGULI

JF-Expert Member
4,811
1,225
Waliomba kujengewa studio, wakajengewa kina Ruge.

Bongofleva bangi zinawaharibu. Uzuri wakiharibika, mkulu anawatafutia tiba. Kama huamini muulize Ray C.
Wanatia aibu, embu angalia wanamuziki wa Kenya na Uganda wanamaendeleo makubwa sana.... au labda bangi zao zina akili zaidi ya hizi za kinondoni studio
 
Ilonga Msalabani

Ilonga Msalabani

Senior Member
111
170
Kuna wakati huwa nafikiri wamerogwa sijui? Maana kuna wengine wamesoma Km FA, noorah lakini hamna kitu. Kwa kweli amkeni na mpendane ninyi kwa ninyi sio kuibiana, mnashinda hata na madereva Bodaboda, wanaushirikiano. Umoja ni nguvu, rudini muwe pamoja acheni bangi na madawa ya kulevya. Adui yenu ni ninyi wenyewe...
 
warumi

warumi

JF-Expert Member
15,074
2,000
Tatizo wanapenda sana sifa wakati uwezo hawana,wanaishiwa kugeuzwa nyuma tu na wanaume wenzao,haswa nanii anageuzwa hallaf anaachiwa gari auzie nalo sura baada ya wiki anarudisha,akinunuliwa nguo mbili pale robby one pamoja na galaxy,basi aah maisha wameyapatia,bado sana hao kujitambua
 
Justin Dimee

Justin Dimee

JF-Expert Member
1,146
1,225
Wataa juaa wenyeewee shaaurii zaoo wachezee nafasii umrii na ukisogeea na wamee ishiwaa kutoa 0712 wata jiju?
 
KAFA.cOm

KAFA.cOm

JF-Expert Member
1,303
2,000
Waliomba kujengewa studio, wakajengewa kina Ruge.

Bongofleva bangi zinawaharibu. Uzuri wakiharibika, mkulu anawatafutia tiba. Kama huamini muulize Ray C.
ile ni mali ya kaka mkuu ndo maana ilitafutiwa free tiba.
 

Forum statistics


Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom