Hapa chini ni kocha mpya wa Simba akikagua uwanja wa mazoezi unaotumiwa na timu hiyo.
Na hizi picha hapa chini ni vijana wa Yanga wakiwa mazoezini.
Chini ni kocha mpya wa Azam akiwa anatambulishwa kwa wachezaji katika uwanja wao ambao hutumika pia kwenye baadhi ya mechi za ligi kuu.
Kwa haraka haraka ukiangalia hizo picha unaweza kujua kwamba Timu ya Azam inashiriki ligi kuu na zingine ni timu za mtaani au timu za shule kwa ajili ya mashindano ya UMISETA.
Kwa kweli kuna kila sababu ya Simba na Yanga kutengeneza japo pitch kwa ajili ya mazoezi, bora wenzetu Yanga uwanja wao wenyewe wa mazoezi wanao japo ni mbovu sasa kichekesho ni wenzangu na mimi wa pale msimbazi kila siku tunaambiwa uwanja uko Bunju sijui kwa nini wanashindwa kutenga japo milioni mia moja kila mwaka ili kuboresha japo pitch na facilities zingine ili kama inawezekana timu inaweka kambi huko huko wakati inajiandaa na mashindano.
Uongozi ukiamua ni rahisi sana, maana wanahitaji kuwa na kitu kama hostel ambayo inawezakuwa na vyumba kama 30 kwa ajili ya kulala, sehemu ya jiko, sehemu ya mazoezi kwa maana ya gym, sehemu kwa ajili ya mikutano pamoja na kufanyia mafunzo kwa nadharia, wakiamua ni rahisi sana, ni suala la kutenga japo milioni mia tu kila mwaka na baada ya miaka kama kumi watakuwa na uwanja wao wa mazoezi na hostel ambayo inaweza kuwa ni bora sana.