Tofauti kati ya nyaraka za siri na uwovu waserikali.

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,184
11,200
Tufike mahali watanzania tujifunze nakuelewa kati ya nyaraka za siri za serikali, na nyaraka za siri za uwovu wa serikali ambazo kila mtanzania anapaswa kuzijuwa na hakuna sheria inayo ilinda serikal kuzilinda hzo siri. Nyaraka za siri za serikali ni mipango ya siri,maeneo yasiri,mambo ya jeshi,usalama wa Taifa na miradi ya kijeshi na usalama wa taifa, hayo ukiyatoa basi kifo kinakuandama. Nilazima tujuwe mtu anae toa siri za serikali ambapo zitasaidia kuwakamata wahalifu basi huyo ni mzalendo wakati yule atatoa siri za nchi nakuleta maadui kutambua mambo yetu huyo ni msaliti. Kwanini nasema hvyo kama kunamtu anakumbuka hivi karibuni kuna General mmoja huko marekani amefukuzwa kazi kwakuelezea siri za Marekan kuwapo kijeshi Afighanistan,jambo ambalo sii jema ni usaliti kwa taifa lako. Pia upo mtandao huko marekani unaitwa wikileaks umefungiwa just kwakuweka hadharan mambo ya siri za kiusalama kujulikana na watu. So mtu kama Dr slaa ni mtu mzuri na ambaye anapaswa kuenziwa na vijana kwakuwa mzalendo nakutoa siri za uwovu wa watawala, tumkumbuke Rais mstaafu wa Ghana J. Rolein au JJ. Rais alie taka kuuwawa na watawala just kwakutaka kuipindua serikali iliyo jaa uwovu, lakini at the last akaokolewa nakuwa rais ambae alithubutu kuiangamiza Rushwa kwakuwanyonga mageneral wa Jeshi waliokuwa waovu. Nilazima sisi tulio na pumzi ya uhai kulitetea taifa letu ikibidi hata kufa na ndipo Mungu atatubariki. Tukumbuke "TUNAYO SILAA MOJA TU YA MAANGAMIZI NAYO NI KUPIGA KURA NAKUIONDOA CCM KWA AJILI YA MAENDELEO NA MWANGA MPYA KWA WATANZANIA."
 
Back
Top Bottom