Tofauti kati ya neno Mungu na mungu!

Eghorohe

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
220
78
Nimekuwa nikisoma post za watu mbalimbali humu jamvini, wanaandika neno mungu (god) wakimaanisha Mungu (God). Tafadhalini sana tuelimishane juu ya hili usianze jina la Mwenyezi Mungu kwa herufi ndogo hata kidogo kwa kufanya hivyo unamwabudu shetani anayeitwa mungu (god) kwa wingi miungu.
 
Hiyo tofauti unayoitaja inadhihirika kwenye matamshi au ni maandishi peke yake, ipi nafasi ya dhana yako miongoni mwa watu ambao hawajawahi kuona herufi kabisa maishani mwao.

Unafahamu tofauti kati ya 'deity', 'gods' na 'haethen god'?
 
Sio kweli god sio miungu bali gods. Kuandika god ni kutojua tu matumizi ya herufi kubwa. Pia ni vyema kumuheshimu Mungu kwa kuanza jina lake kwa herufi kubwa.
 
chonde chonde na nyie mnao andika zamaulid badala ya Zamaulid hilo si jina langu!ila yanatamkika sawa tu
 
Last edited by a moderator:
Nimekuwa nikisoma post za watu mbalimbali humu jamvini, wanaandika neno mungu (god) wakimaanisha Mungu (God). Tafadhalini sana tuelimishane juu ya hili usianze jina la Mwenyezi Mungu kwa herufi ndogo hata kidogo kwa kufanya hivyo unamwabudu shetani anayeitwa mungu (god) kwa wingi miungu.

imeandikwa wapi wewe?........kwanza mungu si mungu...
mungu ni jina la kiswahili ambalo tumempa alieitengeneza dunia,lakini sio jina lake
 
uko sahihi mleta uzi nakumbuka hata kipindi niko shuleni mwalim wangu wa kiswahili alisema kuna majina ambayo ni lazima uanze na herufi kubwa likiwemo na jina la Mungu,mji,mkoa,nchi n.k
 
Nimekuwa nikisoma post za watu mbalimbali humu jamvini, wanaandika neno mungu (god) wakimaanisha Mungu (God). Tafadhalini sana tuelimishane juu ya hili usianze jina la Mwenyezi Mungu kwa herufi ndogo hata kidogo kwa kufanya hivyo unamwabudu shetani anayeitwa mungu (god) kwa wingi miungu.
Hata jina langu ukome kuanza na herufi ndogo!
 
imeandikwa wapi wewe?........kwanza mungu si mungu...
mungu ni jina la kiswahili ambalo tumempa alieitengeneza dunia,lakini sio jina lake

ImageUploadedByJamiiForums1444077008.640996.jpg
 
Back
Top Bottom