Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Introver

JF-Expert Member
Apr 6, 2019
484
544
images-1.jpeg

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Mtu ni kiumbe cha kwanza kilichoumbwa na Mungu duniani, chenye mfano wake na sura yake, kilichoumbiwa utashi na ujuzi ndani yake, kilichotofautishwa na wanyama wote na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu duniani Ndicho kinachoitwa mtu.

Tunasoma hilo katika,

Mwanzo 1:26

[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Lakini jina Binadamu/mwanadamu, ni neno lililozuka kufuatana na jina la mtu wa kwanza aliyeitwa Adamu.

Jina hilo alipewa na Mungu..Hivyo watu wote waliozaliwa na yeye waliita “wana wa Adamu”kwa kifupi “wanadamu” ambapo jina hilo kwa kiharabu linatamkwa “bin-Adam” ambapo sisi tunatamka “Binadamu”

Lakini ni mtu yule yule..isipokuwa asingeweza kuitwa binadamu siku ile ya kwanza alipoumbwa kwasababu alikuwa bado hajapewa jina, na pia halikuwa hana baba wa mwilini.

Ni sawa na Neno mwebrania na mwisraeli… kabla ya Yakobo kubadilishwa jina lake wana wote wa Ibrahimu hata Ibrahimu mwenyewe aliitwa Mwebrania..(Mwanzo 14:13)

Lakini Yakobo alipobadilishwa jina na kuitwa Israeli, utaona uzao wake wote baada ya pale ulizoeleka na kuitwa waisraeli mpaka leo. Lakini bado mahali pengine waliendelea pia kuitwa waebrania kwa asili yao.

Ndivyo ilivyo kwa mtu na mwanadamu. Ni yule yule kulingana na majira.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
 
Mtu ni mnyama lakini binadamu ni kiumbe wa juu zaidi anayeweza kuishi kwenye mwili wa mtu au hata nje ya mwili wa mtu.
 
View attachment 2190706

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Mtu ni kiumbe cha kwanza kilichoumbwa na Mungu duniani, chenye mfano wake na sura yake, kilichoumbiwa utashi na ujuzi ndani yake, kilichotofautishwa na wanyama wote na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu duniani Ndicho kinachoitwa mtu.

Tunasoma hilo katika,

Mwanzo 1:26

Lakini jina Binadamu/mwanadamu, ni neno lililozuka kufuatana na jina la mtu wa kwanza aliyeitwa Adamu.

Jina hilo alipewa na Mungu..Hivyo watu wote waliozaliwa na yeye waliita “wana wa Adamu”kwa kifupi “wanadamu” ambapo jina hilo kwa kiharabu linatamkwa “bin-Adam” ambapo sisi tunatamka “Binadamu”

Lakini ni mtu yule yule..isipokuwa asingeweza kuitwa binadamu siku ile ya kwanza alipoumbwa kwasababu alikuwa bado hajapewa jina, na pia halikuwa hana baba wa mwilini.

Ni sawa na Neno mwebrania na mwisraeli… kabla ya Yakobo kubadilishwa jina lake wana wote wa Ibrahimu hata Ibrahimu mwenyewe aliitwa Mwebrania..(Mwanzo 14:13)

Lakini Yakobo alipobadilishwa jina na kuitwa Israeli, utaona uzao wake wote baada ya pale ulizoeleka na kuitwa waisraeli mpaka leo. Lakini bado mahali pengine waliendelea pia kuitwa waebrania kwa asili yao.

Ndivyo ilivyo kwa mtu na mwanadamu. Ni yule yule kulingana na majira.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Kwamba mtu ameumbwa kwa sura ya Mungu? Yaani Mungu ana sura kama ya mtu? Naomba ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom