Tofauti kati ya LIBYA, IVORY COAST, BAHRAIN, SAUDIA, ISRAEL/PALESTINE & YEMEN! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti kati ya LIBYA, IVORY COAST, BAHRAIN, SAUDIA, ISRAEL/PALESTINE & YEMEN!

Discussion in 'International Forum' started by Ghost, Mar 20, 2011.

 1. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu kama kichwa hapo juu kilivyo jieleza, naomba munisaidie kuelewa tofauti ya mapigano/maandamano kwenye hizo nchi zote.
  Na kwanini Libya imeshambuliwa na sio hizo zingine...
  Asanteni:panda:
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni rasilimali na utajiri wa Libya ambapo Ghaddaffi hakuingilika kirahisi na wakubwa wa magharibi.
  Saudia pale ni base kubwa ya USA.
  Israel hao ni wateule WANALINDWA na wakubwa wote, ikumbukwe waisrael ni mithili ya wao ndio wanaoiongoza dunia kwa nyanja nyingi ndio maana hawaingiliwi hata na UN.
  Palestine ni threats wa taifa teule la Israel, hawa hawana sauti wala umuhimu kwa wakubwa.
  Ivory Coast ingalikuwa kama DRC...mara moja wangevamiwa na kukombolewa.
  Yemen haina utajiri mkubwa na itakuwa ni hasara kubwa kwa WAKUBWA kupeleka vikosi huko na uchumi wa nchi zao utadorora na kuleta mtikisiko wa kiuchumi duniani.
   
 3. M

  Mchili JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hayo ni mawazo Pevu, Hawa wakubwa wanachukulia Africa kama pori lisilokuwa na mwenyewe ukiona sungura unakimbiza na ukikutana na bweha au hata simba anaekuzuia unapiga mshale. Hawaoni waafrika kama binadamu wanaostahili kumiliki mali. Hata kuwalipa kwa rasilimali wanazochukua wanajisikia vibaya.
   
 4. S

  SELEWISE Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I dont see any differenc there,i think there iz issue which they going to grant nji oil tu...
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Libya na Ivory Coast hakuna tofauti. Ila Kuhusu Libya, Muungano ya nchi za Kiarabu uliomba UN Security Council iingilie kuokoa maisha ya watu. In fact, security council haikufnya move yoyote mpaka Arab league ilipoomba msaada. Kuhusu Ivory Coast, African Union imekataa kuomba msaada on the ground that watatatua huo mgogoro wao wenyewe. In fact they have failed, lakini hawataki kuomba msaada toka UN.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hizi bloc sasa zinanichanganya!! Arab League na African Union, Libya iko kotekote mbona sasa AL ndio wanaomba UN? AU vipi? Unafiki mtupu. Mbona Amri Mousa anapiga mayowe?
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hizi bloc sasa zinanichanganya!! Arab League na African Union, Libya iko kotekote mbona sasa AL ndio wanaomba UN? AU vipi? Unafiki mtupu. Mbona Amri Mousa anapiga mayowe?
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  AU hawakuomba. Amri Mousa anapiga mayowe but AU club imesema itatatua mgogoro. Matokea yake ndio watu wanaendelea kufa huko.
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Na AU siwaelewi kabisa kwani Gaddafi alipoanza kupokea kichapo wakatoa tamko kwa wazee wa kazi wa dunia hii kwenye uwanja wa vita kusitisha kichapo. Na Gaddafi alikwisha waambia yeye ni mfalme wa wafalme Afrika, sasa huu si upuuzi kweli?
   
 10. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wachache sana wenye akili timamu ya kuliona hilo... wengi wamesahau kwamba Libya ni nchi iliyonyanyua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Afrika, hususan SA na Uganda.. nafasi zilizopatikana kwa Tanzania hazikutumika ipasavyo bali watu waliitumia Libya kama kigezo cha kupata misaada ya kujengea misikiti midogomidogo na mkubwa wa Dodoma na ule wa Butiama lakini hebu nendeni Rwanda, Uganda, SA mkatazame nini kimefanyika kutokana na usaidizi wa Libya... Walichosahau watanzania kupata msaada kutoka kwa Gaddaf ni kujenga hoteli za kitalii na lodge! Maana wakati wenzetu wamejenga shule na vyuo vikubwa sisi.........
   
 11. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wanaokufa ni WAAFRIKA, na wale waandamanaji (rebels) ndio inabidi walindwe!! wale wasio na silaha wa-YEMEN na BAHRAIN wafe wamalizike!!! Hiyo ndio HURUMA ya WAKUBWA WANAOTAWALA DUNIA!

  Siku nikiwa Rais wa Tanzania, Nitahakikisha nakuwa na silaha bora kabisa kama Korea kaskazini, kama ni tabu na mashaka tulishazizoea ili wakija wajue nao hawatoki patupu kwenye UKOLONI WA KISASA NA UKIBARAKA
   
 12. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160

  wewe na mimi tunafikiri sawa... nitaanza na mikataba ya madini na kuuzwa kwa Loliondo kwa waarabu :washing:
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na pia ujilize kwanini Amerika/UK waliivamia na kuivuruga Iraq (former middleastern haven), pamoja na Saddam repeatedly kusema hana silaha za WMD na ikaja kuwa kweli. Na kwanini isiivamie North Korea inayokiri kuwa nazo na hata kusema wana nuclear misile ya kuweza fika California na badala yake kuiomba China na Urusi imediate "talks"?
   
 14. S

  SELEWISE Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Bahrain,Israel,Palestina na Yemen?
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  ...ndio maana nasema "nikiwa rais wa Tanzania nitahakiksha nalimbikiza na kuunda silaha hatari kwa ajili ya kulinda nchi! la sivyo tutachezewa na wakoloni mpaka kiama kitakapofika!!"

  Na wakioka huko wanatupa majina ya ajabu ajabu... mpaka nafikia wengine kusema "waafrika wamelaaniwa"!! Hebu fikiria!? Lazima tuwe na la kufanya... Mbona Mugabe hawakumvamia?
   
 16. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Tofauti ni kuwa US inanufaika na uongozi ulioko madarakani Yemen!

  [​IMG]

  Yemeni anti-government protesters in the Yemeni capital, Sana'a, on March 5, 2011.
  The director of Institute for [Persian] Gulf Affairs says the US has played a direct role in the killing anti-government protesters in Yemen.


  "There is a direct link between US aid to Yemen and the killings of hundreds of demonstrators," Ali al-Ahmed told Press TV.

  Ahmed, referring to the arming of Yemeni regime by the US and the presence of the American forces in the country under the pretext of fighting terrorism, argued that the US is responsible for the high death toll among Yemeni protesters......

  Details>>>>>>PressTV - 'US directly linked to Yemen killings'
   
 17. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kila mtu ana haki ya kutazama migogoro hii anavyotaka. Nimekuwa nikiuliza mara nyingi, mfano kwa nini Arab League haijaiomba UN kuingilia mgogoro wa Yemen kwa kiwango na haraka ileile ilivyoomba kuhusu Libya? Tumekomalia tu kulaumu mataifa ya magharibi.. Ndo maana mtu anaweza kulinganisha migogoro ya nchi hizo na mgogoro wa Israel/Palestina kama vile huu ni kati ya wananchi wa taifa moja. Wabongo mjiulize kwa nini watuhumiwa kama Zombe, D Yona, B Mramba nk walikuwa wanapewa treatment tofauti na wengine na hatukuona maandamano wala kelele za usawa kama tunaotaka uonyeshwe na mataƬfa makubwa? Leo hii tunasimama kwenye ngazi ya unafiki kuwapigia kelele wazungu wasifanye unafiki!!!
   
 18. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  If wishes were horses...
   
 19. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ivory Coast Mchezo umeisha. Yaliyomkuta Gbagbo hayo hapa 206365_207736342579467_100000293081389_733028_7182962_n.jpg Haya ndiyo matunda ya Ukaidi. Mzee Mzima aubuliwa na vijana wa kazi.
   
Loading...