Tofauti kati ya KUJAMIIANA, KUZINI, KUFANYA TENDO LA NDOA

Abuu Said

JF-Expert Member
Jul 5, 2015
4,010
4,761
Saalaam ziwafikie ma Great thinkers wote humu ndani, nimekuja na mada yangu naombeni mchanganuo ktk hili........

Kwanza naomba niandike tafsiri yangu nijuavyo mimi ktk haya mambo 3 hapo juu yaani Kujamiiana, Kuzini na kufanya tendo la ndoa;

Nini maana ya Kujamiiana?

-Ni kile kitendo kinachofanywa baina ya viumbe viwili vyenye jinsia tofauti kuingiliana kimwili kwa dhumuni la kufanya uzalishaji. Hiki ni kitendo kinachofanywa na aina zote za Viumbe vilivyomo Duniani.

Nini maana ya Kuzini?
-Ni kile kitendo cha kujamiiana kinachofanywa na Binaadam pasipo idhini au ruhsa ya Mungu, hii ni kutokana na maamrisho yake yeye Muumba kupitia Vitabu vyake alivyoviteremsha kupitia mitume yake na hii ni kwa Dini zote.

Nini maana ya kufanya tendo la ndoa?
-Ni kile kitendo cha kujamiiana kinachofanywa na Binaadam kwa ruhusa ya Mungu hii inatokana na viumbe hawa wenye jinsia tofauti kufuata sheria na kanuni walizowekewa na Mungu. Na karibu dini zote Duniani zinafuata mfumo mmoja ktk kulifanya jambo hili kuwa halali ikiwemo:-
  • Kukubaliana kati ya pande mbili (mwanamme na mwanamke);
  • Kutoa mahali (mwanaume kuridhia kutoa kile ambacho mwanamke anahitaji);
  • Kushirikisha Ndugu jamaa na wazazi ktk kufanikisha shughuli ya ndoa akiwemo kiongozi wa Dini.

Maswali tata:-

  1. Kwanini Binaadam tumewekewa sheria juu ya kulifanya jambo hili la Kujamiana?
  2. Kwanini iwe ni dhambi ijapokuwa mwanamke na mwanamme wamekubaliana wao wenyewe?
  3. Kuna madhara gani endapo tungekuwa tukifanya km wanyama?
  4. Kwanini kuna utamu ndani yake kuliko kitu chochote Duniani?

Ni hayo tu kwa kifupi naombeni tujadiliane kwa kina
 
Kuna madhara gani endapo tungekuwa tukifanya km wanyama?
Haujatoa maelezo wanyama huwa wanafanya vipi.

Lakini likifanyika nje ya utaratibu aliouweka Mwenyezi Mungu, madhara yake yanajumuisha; kuvunja uhusiano wetu mwema na Mwenyezi Mungu, magonjwa, maumivu ya mwili na nafsi, vifo, ugomvi, uvunjifu wa amani, visasi, n.k.
 
Kujahimiana ndio neno limekaa vizuri . Kama sïo chini ya 18 na mmekubaliana Mungu anabariki kwani mnafurahia kazi yake . Tendo la ndoa na kuzini ni maneno yaliyokuja kwa njia ya meli na wamisionari .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom