Tofauti kati ya Christmas na X- Mas

Meinraldm

Senior Member
Sep 1, 2015
150
79
*UFAFANUZI WA MANENO CHRISTMAS NA X-MAS*
maelezo kuhusiana na maneno “CHRISTMAS” na “X-MAS”
Kwa Kifupi, maelezo yanayosambazwa kwenye mitandao yetu ni kwamba “Christmas” ni sahihi na “X-mas” siyo sahihi. Maelezo haya yanayosambazwa si sahihi, ni ya *uongo*.

1.Tukianzia kwenye maneno hayo, kwa karibu kabisa tunarudi kwenye maneno ya lugha ya Kiingereza cha enzi tatu: Kiingereza cha zamani, Kiingereza cha enzi ya miaka ya kati (karne 5 hadi15) na Kiingereza cha siku hizi.

2.Kwa Kiingereza cha zamani “Christmas” ilitamkwa “Cristes maesse” na maana yake ilikuwa “Christ’s festival” yaani sikukuu ya Kristo.
“Crist” ndiyo “Christ” ndiyo Kristo. Kristo maana yake “Mpakwa” ndiyo inayotafsiri jina la Kiebrania (lugha ya Wayahudi) “Meshiah”, yaani “Mpakwa wa Bwana” . “Meshiah” ndiyo tunayotamka sisi Waswahili kama Masiya au Masiha.

2.Neno “maesse” maana yake “festival” yaani sikukuu au sherehe. Katika Kiingereza za enzi ya kati “Cristes maesse” ilinyooshwa na kuwa “Cristemas” ndipo katika Kiingereza cha siku hizi ikafika kutamkwa na kuandikwa “Christmass”.

3.Yaani hapa tunacheza na maendeleo ya lugha ya Kiingereza katika matamshi na maandishi tu. Hadi hapo nadhani nimeeleweka.

4.Lakini suala la CHRISTMAS na X-MAS linarudi kwenye lugha ya Agano Jipya ndiyo Kigiriki au Kiyunani. Jina hilo “Crist” au “Christ” limetoholewa kutoka jina “CHRISTOS” ndiyo Kristo (tukifupisha kwa kudondosha “s” ya mwishoni).

5.Walatini (watu wa Dola ya Rumi) wakatamka “CHRISTUS” ndiyo Kristu (tukifupisha kwa kudondosha “s” ya mwishoni). “Christos” maana yake ni Mpakwa, Masiya au Masiha. Masiya au Masiha yenyewe inatoholewa kutoka jina la Kiebrania “Meshiah” kama nilivyoonesha hapo juu. Waingereza hutohoa “Meshiah” na kuandika na kutamka “Messiah”.

6.Kumbe katika Kigiriki au Kiyunani, “CHRISTOS” huandikwa kwa herufi ndogo *"Χριστός”* na kwa herufi kubwa “XPICTOC” au “ΧPIΣTOΣ” au kwa sanaa “XPISTOS”.

7. Katika Kigiriki hiyo “X” siyo “eksi” bali ni “ch” na hiyo “P” siyo “pi” bali “r”. Hivi kwa Kigiriki “XPI” husomwa “Chri.”
Halafu, kutokana na herufi “X” na “P” kusimama mwanzoni mwa jina “XPISTOS” au "XPICTOC",

8. Wakristo wa mwanzo walizitumia herufi hizo mbili kufupisha jina “CHRISTOS” hivyo wakawa wanaandika wakibebanisha “X” na “P” na kuzaa alama moja maarufu sana mnayozoea kuiona kwenye nguo za misa au vitambaa vya altareni na kwenye vitabu. Ni alama ya “P” iliyokatwa mguuni kwa mstari -- au X.

9.Kwa maelezo haya basi, “X-MAS” si neno tofauti na CHRISTMAS”. Ni neno lile lile isipokuwa badala ya kuandika CHRIST kirefu watu wanafupisha kwa X tu. Ndipo inapotokea X-MAS mahali pa CHRISTMAS. Hivyo hiyo “X” ya mwanzoni haimaanishi “mkasi” wenye maana ya “kukata” au “hakuna” bali “X” yenye kufupisha jina “CHRISTOS” na “MAS” huko mwishoni kumaanisha “SIKUKUU” au “SHEREHE”.

10.Kwa hiyo, asiwadanganyeni mtu wala asiwababaisheni mtu kwamba “X-MAS” maana yake “HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO” eti kwa vile “MAS” ni neno la Kigiriki linalomaanisha “MKUSANYIKO”. Hakuna neno la Kigiriki MAS linalomaanisha MKUSANYIKO. Iweni na amani,. Hata mtu akilazimisha maneno ya Kigiriki maneno yote yanayokaribiana na MAS japo kwa maandishi na matamshi hakuna neno lenye maana ya mkusanyiko.

11.Tazama maneno yaliyopo ni “μασάομαι” lenye maana ya kuuma, kung’ata, “μαστιγόω”lenye maana ya mchapo wa kiboko au kuadhibu, “μαστίζω”lenye maana ya kuchapa, “μάστιξ” lenye maana ya pigo la mjeledi na maradhi na “μαστός” lenye maana ya kifua. Kama msomavyo hapa katika maneno haya hakuna neno linalomaanisha “MKUSANYIKO”.

12.Basi, kuweni na amani. X-MAS si neno tofauti na CHRISTMAS. Ni neno lile lile isipokuwa badala ya kuandika CHRIST kwa urefu watu wanafupisha kwa X tu.

12.Nawatakieni maandalizi mema ya Krismasi au Noeli.
Kwisha kumaliza somo hili la lugha ya Kiingereza na Kigiriki naomba kuwaongezea mambo kidogo.
Majina: sikukuu hii huitwa pia Kuzaliwa (Nativity) au Yule. Ni sikukuu ya utamaduni wa Kikristo. Maana yake ni kukumbuka na kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Na kwa vile ni shauri la Mungu kutupatia sisi wakosefu zawadi ya Mkombozi, katika kuadhimisha sikukuu hii zawadi hutawala. Ni sikukuu inayosherehekewa kwa mikusanyiko, upambaji wenye ishara nyingi kama vile miti ya Krismasi na dhifa za keki, kula na kunywa pamoja.

13.Tarehe ya kuadhimisha katika Kanisa la Magharibi na baadhi ya Makanisa ya Mashariki pamoja na walimwengu wengine ni tarehe 25 Desemba. Lakini katika baadhi ya Makanisa ya Mashariki huadhimishwa tarehe 7 Januari. Na katika makanisa ya Kiarme byni huadhimishwa tarehe 6 Januari.


KILA LA HERI KWENU NYOTE!
 
Pole.
mambo ya Theology Hayo.
hakuna theology hapo ni historia tu. X means an-known number. mass means crew of the people.so people are worshiping and celebrating to an-known god under the sun, but is not the God who created the earth and the heaven
 
Bado Brother hata Jesus wapo waliogeuza na kuita wanavyojua wao.... Swali la kujiuliza ni kwa nini wafupishe kwa alama hiyo moja? Shetani hafanyi mapya sana kuwapotosha watu ila anayatumia yaleyale kupotosha kwa kutumia uongo unaofanana na ukweli.
Umejitahidi kujenga hoja yako kiufafanuzi na kuijaza ushawishi ili kuleta ukubalifu uleule ambao unataka kufananisha nuru na giza.
X'mas siyo Christmass. Kwa sababu haipo haja na sababu yoyote ile ya kufupisha jina la Yesu au Mungu.
Ni sawa na kuchekesha hapa kutumia herufi "Y"na kusema inawakilisha Yesu au "M"kumwakilisha Mungu.
Hakuna mantiki yoyote ile ya kufupisha hapo labda tuseme kupotosha.
Nitaendelea kukataa kuwa X"mas ni Christmass.
V, W. M
 
Back
Top Bottom