Tofauti kati ya chama na Serikali (Jibu kwa wanaosema CCM imefanya mengi toka Uhuru) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti kati ya chama na Serikali (Jibu kwa wanaosema CCM imefanya mengi toka Uhuru)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calnde, Apr 13, 2012.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nianze kwa kuwapa pole wale wapenda mabadiliko kwa namna mchakato wa katiba unavyokwenda. Mashaka yanazidi matumaini.

  Kwa hoja yangu, labda niweke mambo yanayoleta maendeleo kwa nchi yeyote

  A. Inherent factors ( zipo zenyewe kiasili. Hazifanywi na watu)

  1. Rasilimali watu wenye ufahamu wa kutosha ( hawa wanalipa kodi sawasawa, wanafanya ugunduzi, mchanganyiko

  wao unapelekea kukua kwa biashara nk nk)

  2. Rasilimali ghafi/ asilia (Raw materials/Natural resources like land, minerals, water, costs, forests etc)

  B External Factor ( Influences internal/inherent factors)

  3. Mfumo bora wa uongozi. Huu kazi yake ni kuunganisha factors hizo hapo juu mbili ili kuweza kuleta maendeleo.

  Yaani kuiwezesha rasilimali watu kutumia rasilimali asilia kujiletea maendeleo. Nchi isiyokuwa na maendeleo tatizo huwa

  ni mfumo mbaya wa uongozi na si vinginevyo maana kila nchi imejaliwa kuwa na internal factors!


  KUFELI KWA CCM
  Ninasema CCM imefeli kwa sababu imeshindwa kusimamia muunganiko wa group A kuweza kujiletea maendeleo. Ili kujua

  wamefanikiwa unaangalia wingi wa raw materials/natural resources na namna ambavyo watu wameelimishwa na

  kusaidiwa kuzitumia kujiletea maendeleo. Utagundua CCM imefanya kwa kiwango kidogo. Dar Express haiwezi kutoka

  Dar saa moja ikafika kibaha saa kumi na bado ikataka tuisifie kuwa ni gari nzuri! Maana hata bajaji haifanyi hivyo.

  Ileweke kwamba chama hakina njia yeyote yakuleta maendeleo kama group A is not existing.. Hivyo hakiwezi kujisifu

  kimejenga vyuo, hospitali, nk nk maana bila ya group A isingewezekana. Hakitengenezi pesa. Hakitengenezi mito.

  Hakileti mvua. Hakitengezi watu. Hivyo ndo kusema group A wanaweza kuendelea bila group B lakin group B haina

  maana kama group A haipo.

  Chama kinaweza kujisifu kwa moja tuu! Kimetengeneza serikali ambayo ni mfumo tofauti na unaojitegemea nje ya

  chama amabao umesimamia watu kuweza kujiletea maendeleo. Si vinginevyo. CCM imeshindwa hilo. Haina haja ya

  kujisifu kuwa imefanya mengi. Haijafanya. Imeshindwa kutengeneza serikali makini. Matokeo yake imefanikiwa kutupa

  deni la taifa ambalo linazidi sana bajeti yetu ya mwaka. Mafanikio machache yanatokana na growing nature of society.

  Each society has to grow. Hakuna wa kujisifu kwa hili. Bali chama kijisifu kwa kusukuma maendeleo ya nchi beyond

  natural way of growth. Hapa tulipo ni mwendo wa konokono. Hatujisifu kwa hilo. Tunataka mfumo utakaotukimbiza

  mwendo wa rocket. . .
   
 2. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pengine tuchukue nchi kama USA na UK! Hawa vyama vinabadilishana mara kwa mara! Navyo vijisifu vipi? Vimejenga vyuo?
   
Loading...