Tofauti kati ya Augustino Mrema na Jakaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti kati ya Augustino Mrema na Jakaya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Mar 23, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wote kwa nyakati tofauti jana wameripotiwa wakiagiza kuwa waliofuja fedha za umma washughulikiwe

  Wakati Mrema anapambana na waliofuja fedha hizo kwenye halmashauri, Kikwete anapambana na walioajiri wafanyakazi hewa kupitia wizara ya utumishi wa umma.

  Hata hivyo mi naona kuna tofauti kati ya hatua hizo mbili. Mrema ameagiza kuwa wale wote waliohamishwa halmashauri baada ya kugundulika wamefuja fedha za umma WAKAMATWE na kuletwa kwenye kamati yake ili wahojiwe. Kikwete ameagiza wale wote waliofuja fedha kwa kupitia wafanyakazi hewa, WARUDISHE fedha hizo na IKIBIDI washtakiwe.

  Mrema amegundua ubadhirifu, kutoka katika ripoti mbalimbali ndani ya halmashauri kadhaa, ripoti ambazo kwa kiasi kikubwa zilijitahidi kuficha uozo huo. Kikwete ametajiwa katika ripoti ya waziri, juu ya zoezi la uhakiki wa wafanyakazi, kuwa kulikuwa na wafanyakazi hewa.

  Ina maana kuwa Kikwete, hajaweza kutumia vyombo vingine hata vya siri kugundua hili, bali ameegemea moja kwa moja taarifa ya waziri, ambayo upo uwezekano mkubwa kuwa umeficha madhaifu mengi ya wizara hiyo.

  Kwa kweli naweza kusema kuwa kwa kuangalia mamlaka ya watu hawa wawili yalivyotofautiana, siwezi kupata jibu la haraka ni kwa nini Mrema amemzidi Kikwete. Wakati Mrema anawajua kwa majina wabadhirifu wa fedha katika halmashauri, Kikwete anaagiza kushughulikiwa kwa 'ghosts' ambao hawajulikani ni akina nani.

  Sasa mi naomba tupewe mda. Nitakuja tena hapa hapa baada ya utekelezaji wa maagizo haya mawili kutoka kwa hawa watu. Sitaki ku pre-empty mambo, bali kwa approach ya Mrema, naona ana nafasi kubwa zaidi ya kulifikisha hilo suala pazuri, ikilinganishwa na approach ya Mkulu....
   
 2. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  Wote naona Hamna mtu wote wanafiki tu,

  Mkuu angetoa agizo la Moja kwa moja la kusimasha kazi wahusika wote huku zoezi la kutafuta watu waiochomekwa hau hewa wakitafutwa ushaidi wa kutosha na kupisha upelelezi huru, sijaona sehemu kama hiyo yeye anafanya rahisi tu eti WAZIRUDISHE kama walivyordisha za EPA,

  Si sahii kabisa angeamuru wakamatwe wote usiku huu kwani Hawa Ghasia nafikiri tiyari alikuwa na orodha ya watu hawa, wakiendelea kuwa kazini wanaweza choma nyaraka hara nyumba nzima kupotosha ushaidi.

  Mrema huyu mtu siye kabisa, alizoea siku saba Tangia hawajue hawa watu sijaoana katika chombochochote wakitajwa kuwa wameshughulikiwa, hizo ni mbwembwe tu kwa kuwa ametoka rasmi kwenye upinzani na kuwa CCM B kwa hilo lao nimoja tu kubaliki ufisadi
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni wale wale
   
 4. Jayfour

  Jayfour Senior Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa wale ambao hawakuwahi kuuona utendaji kazi wa Mrema ni kuwa yeye hakai chumba kimoja na mafisadi, ni mzalendo mpenda maendeleo ya nchi asiye na ubaguzi ... ni mbunifu, mwenye mbinu ya kupambana na kero mbalimbali kwa ufanisi..na zaidi, huzifuatilia kauli na maagizo anayotoa...

  Mimi nina matumaini makubwa kuwa atang'oa mizizi ya ufisadi ktk halmashauri zetu za wilaya na hivyo kuokoa fedha ambazo zingeishia matumboni mwa mafisadi...kiutendaji namfananisha Mrema na Magufuli au hayati Edward Moringe Sokoine(RIP)...ambao wanachosema ndicho wanachomaanisha...
   
 5. p

  plawala JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo lake Mrema anabadilika badilika,kwa sasa hivi simtofautishi na na huyo mwenzake
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  mrema wa leo sio huyo wa zamani hizo. binafsi sioni kama kutakuwa na lolote.besides hana nguvu ya viiiiile na ukizingatia ni ccm kivuli tu huyo. hamna kitu ndugu yangu
   
 7. p

  police Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tofauti mrema hawaogopi wabadhirifu a.k.a mafisadi, kikwete anawalinda..
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,302
  Likes Received: 22,103
  Trophy Points: 280
  Kikwete bwana, bonge la myeyushaji
   
 9. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Jk mkweere
  mrema mchaga
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kikwete handsome, mrema JITU LA KAZI.
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mrema ni ccm ndo wale wale
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  Kikwete yuko tayari watz wamhukumu baadaye kuliko kuwafunga au kuwanyonga mafisadi
   
 13. M

  Majasho JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mrema ni jembe
   
 14. b

  bashemere Senior Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mrema mkristo na mchaga.
  kikwete muislam na ******.
  utendaji wao wa kazi wote ni vilaza kikwete anachekacheka.
  mrema alikuwa hachekicheki

   
Loading...