Tofauti kadhaa kati ya mwanaume na mwanamke... Nawe ongezea nyngne

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
Vitu 10 Ambavyo Wanawake
Wamewazidi Wanaume...;
1. Wana Nguo Nyingi Kuliko Wanaume.
2. Wanafahamu Nani Ni Baba Halisi Wa
Watoto Wao.
3. Ni Wepesi Kupenda Na Wakipenda Hupenda Kweli.
4. Wanaoga Mara Nyingi Zaidi Kwa Siku.
5. Wana Huruma Sana Ingawa Mara
Nyingi Huwa Inawaponza.
6. Wana Uwezo Wa Kubadilisha Tabia
Ya Mwanaume Muda Wowote.
7. Wana Uwezo Wa Kuishi Na
Kupendeza Bila Kuwa Na Kazi Wala
Biashara Yoyote(Akili Kumkichwa).
8. Kwao Nywele Na Kucha Ndo Vitu
Vya Kwanza Kufikiria Wakitaka Kutoka.
9. Wana Uwezo Wa Ku-Pretend Kwa Muda Mrefu Zaidi Hasa Kwenye Mapenzi.
10.Ni wepesi kusahau na kusamehe.

Andika Nyingine Unayodhani
Nimeisahau..............
 
Kwa kumiliki wingi wa viatu hao!
Achana nao, tena hii ya utajiri wa kumiliki wingi wa viatu ndiyo nadhani ulipaswa uiweke No 1 .
Yupo Dadaangu alikaa na pear ya viatu one year havivai !
Uliza sasa kisa nini ?
Eti nguo za kuvalia viatu vile ziliibiwa! So ni hadi atakaponunua tena nguo ziendanazo na viatu vile, ndiyo vivalike .
 
Da kwenye swala la nguo na viatu usipime kakosa sana mabegi matatu wakt mimi nina nguo sita sita tu na viatu pea moja simple pea moja na sandal pea moja,wao kila nguo ina kiatu chake

Swala la kupendeza kwao first hata kama hana kazi lengo ni kula vichwa,akiwa mchafu hatopata vichwa so anaweza akatumia laki nzima kwenye urembo na asibakize hata hela ya kula.
 
wana machozi ya karibu, (ni wepesi sana kulia) iwe kwa huzuni au furaha.
 
Macho yao hubadilika kila generation. Zamani walikuwa na macho ya mviringo siku hizi wana macho kama ya benzi za kisasa.

Yaani nyuzi inaanzia jichoni inagonga kwenye nywele, hadi raha.
 
Macho yao hubadilika kila generation. Zamani walikuwa na macho ya mviringo siku hizi wana macho kama ya benzi za kisasa.

Yaani nyuzi inaanzia jichoni inagonga kwenye nywele, hadi raha.

Hakyanan Kongosho unanitisha....huu utafiti inabidi ni ufuatilie kwa makini nione kama ni kweli!!!
 
Urafiki wa baina yao wenyewe hubadilika badilika sana, leo Ashura rafiki yake ni Stella, kesho Stella kahamia kwa Siwema na Ashura kagandia kwa Eliza, mara oooh Stella kamshindwa Siwema na akamalizia urafiki kwa Joyce, wakati huo huo Eliza hamtaki Ashura kwa sababu rafiki yake ana bifu na Stella!

Kaazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom