Tofauti baina ya "Usharika" na "Ushirika"

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,497
19,333
Kuna tofauti gani baina ya maneno Usharika na Ushirika katika lugha ya kiswahili.
 
Sina tafsiri rasmi, zaidi ya jinsi ninavyoyaelewa.
Usharika ni neno nimelisikia zaidi kwa upande wa kidini, hasa mgawanyiko wa maeneo ya kanisa. Mfano, Kinondoni, kuna makanisa kadhaa labda Hananasif, Shamba. Sasa haya makanisa yatajulikana kama usharika. Ikitokea kuna mkusanyiko, watatofautishwa kwa kuwaita usharika wa Hananasif, usharika wa Kinondoni Shamba.

Ushirika ni umoja, muungano we aina fulani ili kutekeleza jambo/ lengo pamoja.
 
Umoja wa wakristo wa mahali Fulani........ Usharika

Umoja wa watu wenye mlengo mmoja........ Ushirika eg wakulima
 
Back
Top Bottom