Tofauti 3 kati ya Samia Suluhu na Hayati Magufuli

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Rais Samia Suluhu ameingia madarakani tarehe 19 Machi 2021 baada ya kufariki kwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli. Hadi leo tarehe 2 Julai 2022 Rais Samia Suluhu ana siku 470 madarakani. Licha ya kuwa madarakani kwa siku chache, Rais Samia Suluhu ameweza kuonesha utofauti mkubwa sana na mtangulizi wake. Ziko tofauti nyingi sana kati ya Samia na Magufuli. Binafsi nitatazama tofauti tatu alizonazo Magufuli na Samia na Samia Suluhu.
Samia Suluhu ni muuni wa Multilateralism na JPM alikuwa muuni wa Economic Nationalism

Rais Samia ni ni mtu anayeamini hasa katika kujenga ushirika mzuri na mataifa na mashirika ya nje ili kuifungua nchi na kuchochoe maendeleo. Ndio maana unaona Mama anafanya sana safari za nje na kupewa mikopo ya mashirika na nchi mbali na wawekezaji wengi kuja nchini kuwekeza. Samia anaamini kwamba Tanzania haipaswi kuwa kama kisiwa, bali ifunguke watu waje kuleta fursa ili kutoa ajira za kutosha na watu wanufaike. Hii ni tofauti na JMP ambaye ni Economic Nationalist. Ni mtu anayepinga masuala ya utandawazi na ushirikiano bali anaamini kwamba rasilimali za nchi husika lazima zinufaishe watu wa eneo husika kwanza kabla ya mtu yeyote pasi na kujali watu wengine watajisikiaje.

Ndio maana JPM alipokuwa Rais aliona kwamba Mikataba ya madini hainufaishi watanzania kama inavyopaswa, hivyo aliamua kubadilisha sheria za sekta ya madini akiamini kwamba watanzania hawatendewi haki, kitu ambacho kilidunisha sana imani ya wawekezaji na kuteteresha uchumi kwa kiasi fulani. Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado uchumi wake ni dhaifu, uongozi aina ya Magufuli ni ngumu kufanya kazi ndio maana tulijijitutumua kwamba "Hii nchi ni tajiri" lakini miradi yote mikubwa aliyotekeleza alichukua mikopo ya siri ambayo hata Bunge halikuhusishwa katika kukopa kwake na kulianchai taifa madeni makubwa.

Samia ana ustahamilivu mkubwa wa kisiasa kuliko Magufuli
Wakati wa JPM kulikuwa na matukio ya kutisha sana ya watu kutekwa na kuuwawa kwa siri kubwa na vikosi vya watu wasiojulikana. Rais Samia ana siku 470 tu madarakani na unaweza kusema ni mapema sana kumjua ni mtu wa aina gani, lakini siku hizo zinatosha sana kusema Rais Samia si mtu wa kaliba ya JPM. Uvumilivu wa kisiasa ni ule uwezo wa kuheshimu mawazo ya mwingine na pia kuwapatia haki zote za msingi hata wale walio kinyume na wewe bila kuwafanyia ubaya.

JPM licha ya kuwa na huruma na wanyonge, lakini alikosa kaba dhidi ya watu waliomkosa waziwazi. JPM katika wakati wake waandishi wa habari walikufa, kutekwa, kujeruhiwa, kufungwa, kupewa kesi na wengine kukimbilia ughaibuni kuhofia maisha yao. Haya yote hatuyaoni ndani ya wakati wa Rais Samia Suluhu. Rais Samia hutukanwa sana na vijana mtandaoni, huchorwa katuni na waandishi wa habari wanaandika watakavyo kumhusu lakini yeye ametulia akiwekeza akili yake katika kuleta maendeleo kwa watanzania.

Rais Samia Suluhu ni reformist na JPM ni conservative (Mhafidhina)

Rais Samia Suluhu amejipambanua vyema tangu aingie madarakani kwamba yeye ni mwana mabadiliko. Kama umepata kusoma barua yake ya wazi kwa Watanzania jana wakati tunaadhimisha miaka 30 demokrasi ya vyama vingi Tanzania, utaamini kwamba Rais Samia Suluhu ni mtu anayewiwa kuleta mabadiliko. Rais Samia kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Chama chake kimetamka dhahiri kwamba kinayo nia ya dhati ya kutaka kuandika Katiba Mpya, jambo ambalo lilikuwa ni dhambi kubwa hata kulitaja tu wakati wa JPM.

JPM ni mhafidhina ambaye alipenda sana kuendesha mambo kizamani akiamini kwamba nchi yetu kufuata mabadiliko ya dunia ni kuurejea ukoloni na pia ni mtego wa watu wa magharibi kutaka kuiba rasilimali zetu. Magufuli hakuamini mambo ya mabadiliko ya tabia nchi, hakutaka kusikia mambo ya uzazi wa mpango na ajenda nyingine za kimataifa, aliamini katika njia zake hasa zile zenye kulinda utamaduni wa mwafrika.
 
Mmoja alikuwa Rais wa Tanzania, Mwenyezi Mungu akamchukua kwa mapenzi yake kutimiza ibada.

Mmoja ni Rais wa Tanzania kwa sasa.

Mwisho wa siku wote ni binadamu tu viumbe wa mwenyezi Mungu, mmoja marehemu alikufa akiwatumikia WaTanzania na mwingine bado ni mtumishi wa Watanzania.

Aliyekufa Mungu amrehemu na tunamshukuru kwa kazi yake abarikiwe huko aliko, tunamuombea aliyepo kheri atende haki na awape faraja watanzania.
 
Samia ni legacy ya Magufuli kwa hiyo huwezi kuwashindanisha.

Samia anavyofanya vizuri ndiyo Magufuli anafurahia alichagua jembe
 
Rais Samia Suluhu ameingia madarakani tarehe 19 Machi 2021 baada ya kufariki kwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli. Hadi leo tarehe 2 Julai 2022 Rais Samia Suluhu ana siku 470 madarakani. Licha ya kuwa madarakani kwa siku chache, Rais Samia Suluhu ameweza kuonesha utofauti mkubwa sana na mtangulizi wake. Ziko tofauti nyingi sana kati ya Samia na Magufuli. Binafsi nitatazama tofauti tatu alizonazo Magufuli na Samia na Samia Suluhu.
Samia Suluhu ni muuni wa Multilateralism na JPM alikuwa muuni wa Economic Nationalism

Rais Samia ni ni mtu anayeamini hasa katika kujenga ushirika mzuri na mataifa na mashirika ya nje ili kuifungua nchi na kuchochoe maendeleo. Ndio maana unaona Mama anafanya sana safari za nje na kupewa mikopo ya mashirika na nchi mbali na wawekezaji wengi kuja nchini kuwekeza. Samia anaamini kwamba Tanzania haipaswi kuwa kama kisiwa, bali ifunguke watu waje kuleta fursa ili kutoa ajira za kutosha na watu wanufaike. Hii ni tofauti na JMP ambaye ni Economic Nationalist. Ni mtu anayepinga masuala ya utandawazi na ushirikiano bali anaamini kwamba rasilimali za nchi husika lazima zinufaishe watu wa eneo husika kwanza kabla ya mtu yeyote pasi na kujali watu wengine watajisikiaje.

Ndio maana JPM alipokuwa Rais aliona kwamba Mikataba ya madini hainufaishi watanzania kama inavyopaswa, hivyo aliamua kubadilisha sheria za sekta ya madini akiamini kwamba watanzania hawatendewi haki, kitu ambacho kilidunisha sana imani ya wawekezaji na kuteteresha uchumi kwa kiasi fulani. Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado uchumi wake ni dhaifu, uongozi aina ya Magufuli ni ngumu kufanya kazi ndio maana tulijijitutumua kwamba "Hii nchi ni tajiri" lakini miradi yote mikubwa aliyotekeleza alichukua mikopo ya siri ambayo hata Bunge halikuhusishwa katika kukopa kwake na kulianchai taifa madeni makubwa.

Samia ana ustahamilivu mkubwa wa kisiasa kuliko Magufuli
Wakati wa JPM kulikuwa na matukio ya kutisha sana ya watu kutekwa na kuuwawa kwa siri kubwa na vikosi vya watu wasiojulikana. Rais Samia ana siku 470 tu madarakani na unaweza kusema ni mapema sana kumjua ni mtu wa aina gani, lakini siku hizo zinatosha sana kusema Rais Samia si mtu wa kaliba ya JPM. Uvumilivu wa kisiasa ni ule uwezo wa kuheshimu mawazo ya mwingine na pia kuwapatia haki zote za msingi hata wale walio kinyume na wewe bila kuwafanyia ubaya.

JPM licha ya kuwa na huruma na wanyonge, lakini alikosa kaba dhidi ya watu waliomkosa waziwazi. JPM katika wakati wake waandishi wa habari walikufa, kutekwa, kujeruhiwa, kufungwa, kupewa kesi na wengine kukimbilia ughaibuni kuhofia maisha yao. Haya yote hatuyaoni ndani ya wakati wa Rais Samia Suluhu. Rais Samia hutukanwa sana na vijana mtandaoni, huchorwa katuni na waandishi wa habari wanaandika watakavyo kumhusu lakini yeye ametulia akiwekeza akili yake katika kuleta maendeleo kwa watanzania.

Rais Samia Suluhu ni reformist na JPM ni conservative (Mhafidhina)

Rais Samia Suluhu amejipambanua vyema tangu aingie madarakani kwamba yeye ni mwana mabadiliko. Kama umepata kusoma barua yake ya wazi kwa Watanzania jana wakati tunaadhimisha miaka 30 demokrasi ya vyama vingi Tanzania, utaamini kwamba Rais Samia Suluhu ni mtu anayewiwa kuleta mabadiliko. Rais Samia kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Chama chake kimetamka dhahiri kwamba kinayo nia ya dhati ya kutaka kuandika Katiba Mpya, jambo ambalo lilikuwa ni dhambi kubwa hata kulitaja tu wakati wa JPM.

JPM ni mhafidhina ambaye alipenda sana kuendesha mambo kizamani akiamini kwamba nchi yetu kufuata mabadiliko ya dunia ni kuurejea ukoloni na pia ni mtego wa watu wa magharibi kutaka kuiba rasilimali zetu. Magufuli hakuamini mambo ya mabadiliko ya tabia nchi, hakutaka kusikia mambo ya uzazi wa mpango na ajenda nyingine za kimataifa, aliamini katika njia zake hasa zile zenye kulinda utamaduni wa mwafrika.
Hawa ndowale tunawaita kenge mtu achana na jiwe wewe fala
 
Mbona hao wana itikadi tofauti kabisa lakini ni wapo chama kimoja?
Kwa tofauti zao kubwa namna hiyo za kiitikadi si walitakiwa kuwa vyama tofauti?

Huoni hii inasababisha CCM kutokueleweka. Maana Magufuli alipokuwa akikataa kusafiri na kuwaita mataifa ya nje mabeberu mlimshangilia, lakini Samia yupo tofauti na hilo mnamshangilia tena??
 
Economic nationalism, also called economic patriotism and economic populism, is an ideology that favors state interventionism over other market mechanisms, with policies such as domestic control of the economy, labor, and capital formation, including if this requires the imposition of tariffs and other restrictions on the movement of labor, goods and capital.[1] The core belief of economic nationalism is that the economy should serve nationalist goals.[2]

Economic nationalists oppose globalization or at least question the benefits of unrestricted free trade. They favor protectionism and advocate for self-sufficiency.[3] To economic nationalists, markets are to be subordinate to the state, and should serve the interests of the state (such as providing national security and accumulating military power). The doctrine of mercantilism is a prominent variant of economic nationalism.[4] Economic nationalists tend to see international trade as zero-sum, where the goal is to derive relative gains (as opposed to mutual gains).[1]

Economic nationalism tends to emphasize industrialization (and often aids industries with state support), due to beliefs that industry has positive spillover effects on the rest of the economy, enhances the self-sufficiency and political autonomy of the country, and is a crucial aspect in building military power.[1]

Mkuu ulimaanisha hicho hapo juu au?
 
Back
Top Bottom