Today is World Wildlife Day

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,743
4,270
Leo ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya viumbe hai wa porini na majini ambayo huadhimishwa kila mwaka mnamo Machi 3 ili kueneza uelewa wa mimea na wanyama mwituni

Mwaka huu, siku hii imefanywa mahususi ya kueneza uelewa kuhusu viumbe hai wa majini na umuhimu wao kwa maendeleo ili kuhakikisha wanatunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Tanzania imebarikiwa kuwa na viumbehai lukuki walio nchi kavu na majini. Wanyamapori walio katika mbuga mbalimbali wamekuwa vivutio kwa watalii na kuleta ukuaji wa pato la taifa.

Mwaka 2018, hifadhi ya wanyamapori ya Serengeti iliibuka kuwa bora kuliko zote Afrika ikiipita Mala Mala ya Afrika Kusini na Mana Pools ya Zimbabwe katika utafiti uliofanywa na kampuni ya utalii ya Safari Bookings.
 
Wakati tuna adhimisha siku ya leo tuendelee kupiga vita ujangii huu uliowekwa kisheria.

Hivi inakuaje unaruhusu kuwinda tembo, chui au simba wakati inafahamika kabisa hawa wanyama wanakaribia kutoweka?
Screenshot_20190205-133946~2.jpeg
Screenshot_20190205-131243~2.jpeg
 
Binadamu tuna kazi sana hao wanaofanyiwa hata hawana habari yoyote hlf utakuta sisi ndo tunakula mvinyo na nyama
 
Back
Top Bottom