Tobias Adengenya Anajua kuwa Arusha ni Jiji la Kitalii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tobias Adengenya Anajua kuwa Arusha ni Jiji la Kitalii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wambugani, Jan 7, 2011.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Vurugu zilizosababishwa na Polisi katika Jiji la Arusha tarehe 5 Januari, 2011, kwa kweli zimeleta athari katika biashara ya utalii.

  Inawezekana alipohamishwa Arusha hakupata maelekezo ya kutosha ama ameyapuuza.

  Inaonekana huyu Kamanda wa Polisi hana mwamko wo wote wa kiuchumi na ndiyo maana aliwaamuru Jeshi lake kufanya kama yeye alivyotaka.
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swali hili kamuulize aliyemtoa Uluguruni na kumpeleka huko A. Town, alitegemea nini?
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  ....ndio tatizo la kutumia ubongo ulio matakoni badala ya ulio kichwani!
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwani amri ya kusitisha maandamano ya Chadema ni ya Adengenya au ya Wema? Ninavyofahamu Chadema walikuwa na kibali toka kwa Adengenya ila Wema akisitisha hayo maandamano. Na isitoshe Adengenya hana uwezo wa kuamuru polisi watoke nje ya Mkoa wake mfano Moshi, Manyara n.k. hivyo kwa swala la Arusha hili ni la WEMA na WAZIRI wake.
   
 5. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Anafikiri watu Arusha ni wa kupelekeshwa na waarabu na wahindi kama huko alikotoka...tutaondoka na kichwa chake!
   
 6. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tujikumbushe ya Mh. Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani - Januari 1977:

  Kwa maneno yake Mwinyi alisema: "Kisiasa nakiri kuwa nahusika, siwezi kukwepa kwa sababu dhamana yangu ya uwaziri inaambatana na wajibu unaonitaka nijue yanayotendeka wizarani na pia niweze kudhibiti na kuhakikisha mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi."

  Mwinyi alijikuta katika matatizo hayo baada ya Jeshi la Polisi kufanya mauaji katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga, na alikiri kwamba:

  "…vyombo vinavyohusika na utekelezaji, polisi ikiwemo, vilivuka mipaka ya wajibu wao na vikajipa madaraka ya kuogelea katika vitendo viovu vya kishenzi, kinyama na kikatili hata baadhi ya watu waliokamatwa kwa kushukiwa tu kwamba wanahusika wakafa na wengine wakapata vilema vya kudumu."
  Mwinyi aliweka wazi kwa Mwalimu Nyerere, kwa kusema "Kijinai, mimi binafsi nisingehusika kwani sikushiriki wala kushauri, kuagiza wala kuelekeza mambo hayo yafanywe. …………….. Hivyo, kisiasa nakiri kwamba nahusika.
  Mwinyi alisema: "Kwa hiyo, Mwalimu, nakuomba mambo matatu. Kwanza naomba radhi mimi nafsi yangu na pia naomba radhi kwa niaba ya askari wote walio wema. Pili, naomba vilevile uelewe sehemu yangu katika kosa hili. Tatu, kwa fedheha hili, naomba unikubalie kujiuzulu."

  Arusha ina tofauti gani na hayo?
   
 7. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kunukuu mambo kama Kasuku wewe..

  Kwani kilichomshusha cheo Basilio ninini...si alikataa kutekeleza matakwa ya Wanasiasa, na ya mabosi wake ambapo aliona kuwa wanatumia akili za mgando zaidi kuliko profession!!!
  Andengenye alikuwa na nafaso hiyo, na amei-misuse...he is a stooge in the first place!!! kweeeee!
   
 8. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Pamoja na kwamba Andengenye anaonekana kutimiza order ya mkuu wake, lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia yaliyotokea kwa sababu yeye ndiyo alikuwa kwenye ground. kitendo cha waandamanaji kutembea takribani kilomita mbili bilas vurugu, ilikuwa ni ushahidi tosha kupingana na kile kilichoitwa na Mwema intelegensia kwamba kungekuwepo na uvunjifu wa amani.

  Alikuwa na uwezo wa kumwambia bosi wake hali halisi iliyokuwepo na hivyo angekuwa shujaa wa siku ile. Andengenye hawezi kukwepa hilo na kwangu mimi nasema He is among the killer of the year 2011. KAANZA VIBAYA
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nakuambia adhabu ya mungu haita mwacha andengenye wala mwema......mwema alianza kazi vizuri kasimamia uchaguzi mkuu vizuri lakina naona sasa siasa inamuingia kichwani...aache mara moja maana nguvu ya umma inakujaaaaaaaaaaa dani iliyomwagia ya wapigania haki haitaenda bure!
   
Loading...