Toa msaada Kwa watu wengine kufikia malengo yako

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Kila mtu duniani ni msafiri na katika safari yake anategemea kufika kituoni siku moja.

Kwa kuwa njiani kuna dhoruba nyingi huwa anahitaji msaada wa watu wengine.

Kama wewe ndiye uliyefikwa na wajibu huo usisite kutoa msaada. Mtu anayesaidia wengine huwa na mahusiano mazuri na watu na hata yeye kusaidiwa pale anapopata majanga. Kumbuka msaada mzuri ni ule unaoutoa bila kutegemea malipo yoyote, na kama unataka kusaidia basi msaidie yule ambaye unajua hana uwezo wala jinsi ya kukulipa. Hii itakupa faraja na utajenga jina lako na wasifu wako kwa watu.

Neno msaada lina maana pana sana, linaanzia katika vitu mpaka hali. Kuanzia hela, ushauri, kufundisha, kuelimisha na mambo yanayofanana na hayo.

Uwe na siku njema yenye tafakari na utekelezaji mwema rafiki yangu!!
 
Neno msaada lina maana pana sana, linaanzia katika vitu mpaka hali. Kuanzia hela, ushauri, kufundisha, kuelimisha na mambo yanayofanana na hayo.
Soma hii mada yangu pia;

 
Back
Top Bottom