Toa maoni yako juu ya wagombea hawa wa BAVICHA (Chadema) taifa

Be blessed
Nawafahamu baadhi so ingekuwa vizuri tukapata CV na motivational letter zao(why wanagombea) ili tuwazungumzia vizuri.

Kwa kuanzia Silinde David naomba ajiondoe as yeye ni mbunge anayo sehemu nzuri ya kutuwakilisha na kutusemea so angeruhusu hiyo nafasi imdondokee underground mwingine ili kuongeza stock ya future viongozi wa CDM hence taifa
 
MIE NAWAFAGILIA
Mwenyekiti - Silinde David (Mbozi)
Makamu - Sharifa (Zanzibar)

Katibu - Deo Munishi (Moshi)
Naibu Katibu - Odero Oderos (Rorya)

Hawa ni vijana walio makini na uwezo wa kukieneza chama hadi vijijini badala ya mijini tu
 
AINA YA 'BAVICHA' NINAYOISUBIRI KI-DOTI KOMU ZAIDI HAPO BAADA YA UCHAGUZI WETU KITAIFA NA KAZI YA UTETEZI WA MASLAHI YA UMMA NA SISI VIJANA

Napendekeza Mchakato uwe mgumu saaaana laki wa kidemokrasia, na wenye kuzingatia misingi yooote ya dhana ya utawala bora.

Vile vile pindi mwenyekiti huyo atakapopatikana basi (1) apewe Job Description mahsusi, (2) asaini Mkataba wa Utendaji bora kule kwa Katibu Mkuu CDM na baada ya hapo (3) awe akipimwa mara kwa mara utendaji wake kwenye utaratibu wa Performance Appraisal.

Nasubiri kuona a working BAVICHA na kufunguliwa matawi katika kila kijiji na kitongoji na wala si kule watu kujaza vyeo hapo.

Na uongozi wa BAVICHA ijiandae kabisa na hilo maana vijana tutakua wakali kweli kweli kwenye mambo ya utendaji na tija unayoiletea chama katika kila siku iendayo kwa Mungu!!!!!!!!!!!!
 
Wanajamvi, haya ni baadhi ya majina niliyoyasikia yakitajwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa Baraza la Vijana la Chadema, toa maoni yako tafadhali.

NAFASI YA MWENYEKITI.
1. John Heche (rorya)
2. Silinde David (mbozi mbeya)
3. Mwampamba (mbozi mbeya)
4. Habib Mchange ( kibaha pwani)
5. Ben Saanane ( dar/morogoro)

MAKAMU.
1. Gwakisa Baton (mbeya)
2. Kinabo (moshi)
3. Shalifa (zanzibar)
4.

NAFASI YA KATIBU MKUU.

1. Nassari Joshua (arumeru mashariki)
2. Deogratius Munishi (moshi)
3. Steven Owawa (rorya)

NAIBU KATIBU MKUU.
1. Dadi Igogo (rorya)
2. Odero Oderos (rorya)


mengine nitaweka nikiconfirm. Wadau na wanachadema toeni maoni yenu.

Siwafahamu ila kwa kuangalia Jiographia safu niliyowekea damu ya mzee ingewaondolea tuhuma za ukanda. Katibu msaidizi yeyote atawakilisha
 
Itakuwa vizuri tukipata CV za kila mgombea kwanza, mi namjua Steven Owawa! lakini si kivile hadi nimpe point zote za kuwa kiongozi. Wengine nawasikia tu.
 
Be blessed
Nawafahamu baadhi so ingekuwa vizuri tukapata CV na motivational letter zao(why wanagombea) ili tuwazungumzia vizuri.

Kwa kuanzia Silinde David naomba ajiondoe as yeye ni mbunge anayo sehemu nzuri ya kutuwakilisha na kutusemea so angeruhusu hiyo nafasi imdondokee underground mwingine ili kuongeza stock ya future viongozi wa CDM hence taifa


Sina CV zao kwa sasa nazisaka ila kwa haraka,

John Heche - alikuwa diwani wa tarime baada ya kifo cha Chacha Wangwe na alikuwa kwenye timu ya Dr. 2010
Silinde ni mbunge wa mbozi magharibi
Mwampamba aligombea mbozi mashariki
Habib Mchange - aligombea kibaha


Nassari Joshua- aligombea Arumeru masha akachakachuliwa nadhani mlimwona kwenye mchakato majimboni pia aliwahi kuwa spika DARUSO wakati nasoma UDSM namkumbuka.

Deogratius Munishi - alishawahi kuwa mbunge DARUSO alimaliza chuo mwaka jana.


Dadi Igogo- alikuwa afsa makao makuu ya chama sheria na haki za binadamu, na alikuwa mratibu wa wagombea tz.

Oderos Odero - aligombea udiwani kwenye kata ta ya Baraa arusha hakushinda.
 
Serikali ya Kenya kupitia Rais wake Mwai Kibaki imekataa kupeleka kesi za watuhumiwa wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo (post election violence) katika mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita (International Criminal Court –ICC)

Kijana na hiyo masters zako unatia mashaka.

Mbona watuhumiwa wameshafikishwa mahakamani the hague,?

Halafu uliona wapi ugomvi wa kidiplomasia kati ya serikali na wananchi wa nchi nyingine?

Ilichofanya serikali ni kuunga mkono serikali ya kenya kama mwanachama wa EAC.

Raila akichukua madaraka kwa wakati huo itategemea hali ya kisiasa na sera zetu zikoje,pengine hata hao CCM hawatakuwepo madarakani.

Huwezi kuomba kura BAVICHA kwa kuchimba mkwara CCM,inaoneka huna wana mkakati wazuri.

Pamoja na kujibodoa kote,umeonesha kuwa ulikua mpiga debe tu wakati wa Uchaguzi,Je tutakuamini vipi kukupa nafasi hii nzito?
 
wewe unaonekana mda wooote umesoma na kukulia India utajuaje matatizo ya vijana wetu ili uyaweke wazi kwenye ngazi husika ili yatatuliwe?!! ni haki yako ya kikatiba kugombea ila nilivyoona wewe bado hutoshi!! waunge mkono vijana wenzako wanaogombea baadae utapata nafasi miaka ijayo
 
Viongozi wangu BAVICHA hao hapo.

Lakini nalalamika kutokujitokeza wenzetu wa kule Makao Makuu ya Mabadiliko ya kweli nchini 'Mkoa wa Arusha' kule kwa Machalii wangu wenyewe.

Wanajamvi, haya ni baadhi ya majina niliyoyasikia yakitajwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa Baraza la Vijana la Chadema, toa maoni yako tafadhali.

NAFASI YA MWENYEKITI.
1. John Heche (rorya)
2. Silinde David (mbozi mbeya)
3. Mwampamba (mbozi mbeya)
4. Habib Mchange ( kibaha pwani)
5. Ben Saanane ( dar/morogoro)

MAKAMU.
1. Gwakisa Baton (mbeya)
2. Kinabo (moshi)
3. Shalifa (zanzibar)
4.

NAFASI YA KATIBU MKUU.

1. Nassari Joshua (arumeru mashariki)
2. Deogratius Munishi (moshi)
3. Steven Owawa (rorya)

NAIBU KATIBU MKUU.
1. Dadi Igogo (rorya)
2. Odero Oderos (rorya)


mengine nitaweka nikiconfirm. Wadau na wanachadema toeni maoni yenu.
 
silinde.JPG nassari na lema.jpg

Picha ya kwanza ni ya Silinde David (mb) wa mbozi (uenyekiti)
Picha ya Pili ni ya Nassari Joshua (ukatibu mkuu) akiwa na lema walipoenda kufungua tawi kwenye chuo cha Tumaini SECUCO kilichopo lushoto. Natafuta picha za wagombea wengine then nitazipost.
 
Good Luck guy, let us see if it will make it happen to you.

After all umesomea India, that mean utakuwa unakautamaduni wa kifisadi kama wa kihindi kihindi Ben.

We have vijana wazuri waliosomea kwenye vyuo vya kwetu Tanzania, nao wamebobea kwenye taaluma zaidi kama si ya kwako.
John Heche is almost the best. Vote for him kama unaipenda CHADEMA

Good luck!
Ufisadi haufundishwi shuleni, ni tamaa ya mtu mwenyewe.

Sio kweli kwamba waliosemea Nchi wamebobea zaidi ya waliosoma India.Kikwete ana degree ya uchumi kutoka UDSM lakini cha kushangaza hajui ni kwa nini sisi ni maskini.Lowassa na Chenge walisoma UDSM(Harvard yetu) lakini tunaona jinsi wanavyo taabishwa na kijani aliyesomea India,Nape.

Ben kila la heri
 
Ben,

Ndo wewe? Hongera kwa kuonyesha nia kwa vitendo. Kama sio wewe mwambie aje hapa akomazwe. Pia patamuongezea umaarufu wa kukutana na vijana kama Heche, David.

Ole wenu mjenge makundi kwa faida ya chama cha magamba bila kujijua.

Selous,

Ndiyo mimi.Asante sana mkuu wangu.Mimi sina kundi ndani ya chama.Kampeni zimekatazwa,na hata muda wa kampeni ukifika nitakuwa na mtandao uliojaa watu makini na wanaokitakia chama mazuri kwa manufaa ya watanzania.Nashukuru sana,na nitazingatia ushauri wako mkuu
 
Hongera Ben,

Ushauri wangu ni kuwa unapotaka kugombea Chadema hakikisha unajishughulisha na masuala yanayohusu Chadema pekee. Kuwataja CCM kwenye mkakati wako huu ni kuwapa heshima wasiyostahili... wamepoteza heshima hiyo na hawatakiwa kuwepo kwenye mkakati wako wa kuingoza BAVICHA na Chadema kwenda 2015.

Nakushauri pia ukifanikiwa usaidie kuongeza kasi ya kufungua matawi ya chama ... watu wengi wanataka kujiunga na Chadema lakini changamoto kubwa iliyopo ni kupata ofisi ya Chadema (mimi ni miongoni mwa wanaotaka kujiunga kwa miaka miwili sasa)

Ntemi,

Nashukuru sana kwa ushauri wako.Nitauweka katika kumbukumbu na nitauzingatia.Changamaoto tuliyo nayo ni kukusanya raslimali za kutosha na kuhakikisha zinagawanywa vizuri ili kutekeleza mkakati wetu wa kukieneza chama nchi nzima.Kwa mahesabu yangu,naona inabidi tuweke mkakati wa kuvuna kura za wapiga kura wapya na wale ambao hawakupiga kura.
 
Back
Top Bottom