Toa kasoro kwenye cheti hiki cha kumaliza darasa la saba

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
cheti cha kumaliza la saba.jpg

Jamani nina quiz ndogo hapa kwenu GTs, hebu someni kwa makini cheti hiki na mniambie kama mnaona kasoro yoyote kwenye uchapaji wake.

nimefuta taarifa zingine ili kuhifadhi usiri wa mwenye cheti.

Good saturday.

Solution to the quiz:

Angalieni yale maneno yanayosema tabiya yake ni ya kuridhisha yamechapwa kwa mashine toka kwa mchapaji badala ya kuandikwa na mwalimu kwa mkono, ina maana kila aliyepata cheti hiki atasomeka kuwa na tabiya ya kuridhisha hata kama sio kweli.
 
nimeona makosa mawili
1.hamna neno tabiya kwenye kiswahili,bali kuna tabia
2.cheti hiki ni batili kwa sababu kimefutwafutwa na Lukansola
 
Last edited by a moderator:
kuna shule ya msingi pwani wilaya ya kinondoni? pia kwa maandishi mekundu cheti kimetolewa bila ya kufutwa futwa ila kwenye tarehe imefutwa kdg. mwisho hivi hadi leo vyeti vya shule ya msing vyatolewa? sie tuliomaliza miaka ya tisini hatukupata as walisema hawatoi tena
 
Makosa niliyoyaona ni haya,
1. hakukua na sababu ya kuandika KINACHOTOLEWA BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI, wakati inafahamika kuwa mtu hutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo/kiwango cha elimu fulani.

2. Ni TABIA na sio "tabiya"
3. Sidhani kama ni sahihi kusema ALIMALIZA ELIMU YA MSINGI ila nadhani ni sahihi kuandika AMEMALIZA SHULE YA MSINGI ....... kwa sababu tarehe ndio inaonesha umri wa cheti.

Nimeona hayo tu.
 
Shule ya msingi pwani ipo Kunduchi karibu na Feza Boys Secondary. asante kwa kujaribu, lakini bado kuna technical error nataka muione wajameni.
 
Hapo kwenye wizara wamechemsha, hakuna wizara ya Elimu na Utamaduni kwa upande wa Tanganyika, sina uhakika na visiwani.
 
Makosa niliyoyaona ni haya,
1. hakukua na sababu ya kuandika KINACHOTOLEWA BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI, wakati inafahamika kuwa mtu hutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo/kiwango cha elimu fulani.

2. Ni TABIA na sio "tabiya"
3. Sidhani kama ni sahihi kusema ALIMALIZA ELIMU YA MSINGI ila nadhani ni sahihi kuandika AMEMALIZA SHULE YA MSINGI ....... kwa sababu tarehe ndio inaonesha umri wa cheti.

Nimeona hayo tu.

Hiyo tabiya hata mimi nilikuwa sijaiona mkuu NAFIKA, lakini hapo hapo ndo kwenye tatizo ambalo hamjaweza kuli address, keep trying.
 
Last edited by a moderator:
Hapo chini kimeandikwa Cheti ni batili kama hakina mhuri wa Afisa Elimu wa Mkoa, na ukiangalia cheti hiki kina mhuri wa Mwalimu Mkuu peke yake!!
Kasoro zingine zimeshatajwa!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom