Toa kasoro kwenye cheti hiki cha kumaliza darasa la saba

Lukansola

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
cheti cha kumaliza la saba.jpg

Jamani nina quiz ndogo hapa kwenu GTs, hebu someni kwa makini cheti hiki na mniambie kama mnaona kasoro yoyote kwenye uchapaji wake.

nimefuta taarifa zingine ili kuhifadhi usiri wa mwenye cheti.

Good saturday.

Solution to the quiz:

Angalieni yale maneno yanayosema tabiya yake ni ya kuridhisha yamechapwa kwa mashine toka kwa mchapaji badala ya kuandikwa na mwalimu kwa mkono, ina maana kila aliyepata cheti hiki atasomeka kuwa na tabiya ya kuridhisha hata kama sio kweli.
 
Domhome

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,493
2,000
....ilipaswa iandikwe..."amemaliza Elimu ya Msingi"....na siyo "alimaliza Elimu ya Msingi"...
 
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,887
0
hakina kasoro ila hiki ni cha kumaliza na si vinginevyo.
 
snochet

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,283
2,000
nimeona makosa mawili
1.hamna neno tabiya kwenye kiswahili,bali kuna tabia
2.cheti hiki ni batili kwa sababu kimefutwafutwa na Lukansola
 
Last edited by a moderator:
H

Helios

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
557
500
kuna shule ya msingi pwani wilaya ya kinondoni? pia kwa maandishi mekundu cheti kimetolewa bila ya kufutwa futwa ila kwenye tarehe imefutwa kdg. mwisho hivi hadi leo vyeti vya shule ya msing vyatolewa? sie tuliomaliza miaka ya tisini hatukupata as walisema hawatoi tena
 
2hery

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,460
2,000
Hakuna wizara ya Elimu na Utamaduni Tanzania ya leo.
 
2hery

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,460
2,000
amemaliza vpi elimu ya msingi wakati matokeo hayajatoka
 
NAFIKA

NAFIKA

Senior Member
Dec 3, 2011
126
195
Makosa niliyoyaona ni haya,
1. hakukua na sababu ya kuandika KINACHOTOLEWA BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI, wakati inafahamika kuwa mtu hutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo/kiwango cha elimu fulani.

2. Ni TABIA na sio "tabiya"
3. Sidhani kama ni sahihi kusema ALIMALIZA ELIMU YA MSINGI ila nadhani ni sahihi kuandika AMEMALIZA SHULE YA MSINGI ....... kwa sababu tarehe ndio inaonesha umri wa cheti.
Nimeona hayo tu.
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,457
2,000
Wewe ndio wale wanaokaa posta kufoji vyeti!!!
 
Lukansola

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
kuna shule ya msingi pwani wilaya ya kinondoni? pia kwa maandishi mekundu cheti kimetolewa bila ya kufutwa futwa ila kwenye tarehe imefutwa kdg. mwisho hivi hadi leo vyeti vya shule ya msing vyatolewa? sie tuliomaliza miaka ya tisini hatukupata as walisema hawatoi tena

Shule ya msingi pwani ipo Kunduchi karibu na Feza Boys Secondary. asante kwa kujaribu, lakini bado kuna technical error nataka muione wajameni.
 
MWILI NYUMBA

MWILI NYUMBA

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
818
225
Hapo kwenye wizara wamechemsha, hakuna wizara ya Elimu na Utamaduni kwa upande wa Tanganyika, sina uhakika na visiwani.
 
Lukansola

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Makosa niliyoyaona ni haya,
1. hakukua na sababu ya kuandika KINACHOTOLEWA BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI, wakati inafahamika kuwa mtu hutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo/kiwango cha elimu fulani.

2. Ni TABIA na sio "tabiya"
3. Sidhani kama ni sahihi kusema ALIMALIZA ELIMU YA MSINGI ila nadhani ni sahihi kuandika AMEMALIZA SHULE YA MSINGI ....... kwa sababu tarehe ndio inaonesha umri wa cheti.
Nimeona hayo tu.
Hiyo tabiya hata mimi nilikuwa sijaiona mkuu NAFIKA, lakini hapo hapo ndo kwenye tatizo ambalo hamjaweza kuli address, keep trying.
 
Last edited by a moderator:
Lukansola

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Hapo kwenye wizara wamechemsha, hakuna wizara ya Elimu na Utamaduni kwa upande wa Tanganyika, sina uhakika na visiwani.
Hilo nalo neno mkuu inaonekana cheti cha zamani sana hiki.
 
Lukansola

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Wewe ndio wale wanaokaa posta kufoji vyeti!!!

Teh he he he, haya bwana king kong, mi nimefuta hizo sehemu wasije kumfelisha mwanangu kwa kuwaumbua.
 
Last edited by a moderator:
Lukansola

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Niwape jibu au mnataka kuendelea na chemsha bongo wakuu?
 
marejesho

marejesho

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
6,647
2,000
Hapo chini kimeandikwa Cheti ni batili kama hakina mhuri wa Afisa Elimu wa Mkoa, na ukiangalia cheti hiki kina mhuri wa Mwalimu Mkuu peke yake!!
Kasoro zingine zimeshatajwa!!!
 
Top Bottom