TMDA tafadhari angalieni bei za dawa tunazouziwa tunaumia huku

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,879
4,880
Habari za asubuhi wakuu.

Nayaandika haya nikiwa na masikitiko makubwa kwamba hospitali zetu na pharmacy hasa za private kwa kweli bei za dawa ni ghali mno yani kwa sababu mtu unakuwa unamatatizo basi wanafanya kama kukomoa.

Usiku wa jana nilipata mgonjwa hapa nyumbani nikampeleke dispensary moja kwa ajili ya huduma usiku huohuo. Akafanyiwa vipimo na kupewa dawa. Ki ukweli hata kama sizijui dawa lakini bei niliyouziwa ni kama walikua wanakomoa. Yani nimelipia 50,000/= kwa dawa ambazo ingekua mchana ningeenda pharmacy isingezidi 20,000/= maana hapo nyuma nilishawahi kununu dawa na aina hii.

Rai kwa serikali ni kuwa mmeweka masharti magumu ya kupata bima basi fanyeni hata regulation ya bei za dawa, tunaumia huku. Kwa kuwa nyie mnahudumiwa kwa bima mnasahau kabisa kwamba kuna watanzania hatuna bima.

TMDA kama mna mamlaka kisheria ikiwezakana fanyeni regulation ya bei za dawa, tunapigwa huku.
 
Hizi hospitali binafsi za kijinga sana.

Niliwahi pima malaria ikawa +ve shughuli inakuja dawa.

Mseto 10,000/= sijui vikolokolo gani huko total kama 30k .

Nikawambia ngoja nikachukue hela. Nikapita pharmacy hata 10k haikufika.
 
Dawa zenyewe hazifanyi kazi na hasa zie za hapa nchini na zile za kutoka China, India na Kenya.

Dawa zinazofanya kazi vema ni zile za Ujerumani, Ubeligiji, Italy na nchi zingine za Ulaya
 
Shida inaanzia kwenye manunuzi ya hizo dawa. Hakuna chombo maalum kinachodhibiti manunuzi ya dawa nje ya nchi. Kila mtu ananunua anakopajua yeye, yaan in short soko la dawa ni huria. Kungekuwa na chombo cha serikali ambacho kingefanya manunuzi ya jumla kama vile ilivyo kwa Ewura kwny ununuzi wa mafuta ingekuwa rahisi sana kudhibit bei. Saiv kila mtu anahaki ya kupanga bei anayoitaka akisingizia kanunua kwa bei ghali.

TMDA wao hawahusiki na udhibiti wa bei, kazi yao ni kudhibiti ubora,ufanisi na usalama wa dawa zinazoingia nchini. Pengine ni wakati sahihi sasa TMDA Kuongezewa majukumu hayo
 
Kwa kweli inaumiza sn,hata hizi barabara ni shida tu,kipimo cha malaria bei ni kubwa kuliko dawa yenyewe ya malaria?
 
Habari za asubuhi wakuu.

Nayaandika haya nikiwa na masikitiko makubwa kwamba hospitali zetu na pharmacy hasa za private kwa kweli bei za dawa ni ghali mno yani kwa sababu mtu unakuwa unamatatizo basi wanafanya kama kukomoa.

Usiku wa jana nilipata mgonjwa hapa nyumbani nikampeleke dispensary moja kwa ajili ya huduma usiku huohuo. Akafanyiwa vipimo na kupewa dawa. Ki ukweli hata kama sizijui dawa lakini bei niliyouziwa ni kama walikua wanakomoa. Yani nimelipia 50,000/= kwa dawa ambazo ingekua mchana ningeenda pharmacy isingezidi 20,000/= maana hapo nyuma nilishawahi kununu dawa na aina hii.

Rai kwa serikali ni kuwa mmeweka masharti magumu ya kupata bima basi fanyeni hata regulation ya bei za dawa, tunaumia huku. Kwa kuwa nyie mnahudumiwa kwa bima mnasahau kabisa kwamba kuna watanzania hatuna bima.

TMDA kama mna mamlaka kisheria ikiwezakana fanyeni regulation ya bei za dawa, tunapigwa huku.
Limefika kwa watawala ilo
 
Mkuu yani kwa sababu wanajua hakuna bargain basi ndo wanafanya kama kukomoa

Back
Top Bottom