TMA yatoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya kuwapo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye pwani ya Bahari ya Hindi katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Aidha, imeeleza kuwa mvua zinazonyesha sasa kwenye baadhi ya maeneo ni za kawaida.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA kupitia kwa mchambuzi wa hali ya hewa, Rose Senyagwa, kwa siku ya leo kunatarajia kuwapo upepo mkali unaofikia kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika mita mbili.

“Athari ambazo zinaweza kujitokeza ni ucheleweshwaji wa safari kwa vyombo vya baharini pamoja na shughuli za uvuvi nazo zitaathirika, hivyo ni vyema kwa watu kuchukua tahadhari,” alisema Rose.

Alisema vipindi hivyo vya hali mbaya ya hewa si vya muda mrefu na wanategemea vitakuwa vipindi vifupi, na hali hiyo inaweza kukoma kesho.

Aidha, alisema TMA inaendelea kufuatilia hali ya hewa na itatoa taarifa kadri wawezavyo kwa wananchi ili kuchukua tahadhari kwa hali yoyote ya hewa itakayojitokeza.

Hivi karibuni TMA ilitoa utabiri wa msimu kwa mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka, na kuelezea hali ya mvua za chini ya wastani kutarajiwa, hivyo kusababisha ukame kwa baadhi ya mikoa.

Mikoa ambayo ilitajwa kutarajiwa kupata mvua chini ya wastani ni Dar es Salaam, Mwaza, Kagera, Shinyanga, Simiyu na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Zanzibar.

Chanzo:
IPP MEDIA
 
Tuchukue tahadhari kwani mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kubadili mwelekeo wa maisha pia.
 
Back
Top Bottom