TMA yatoa tahadhari ya Mvua kubwa kwa siku 3 mfululizo kuanzia leo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Aprili 11,2021, imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Aprili 12 hadi Aprili 14 mwaka huu katika mikoa 15.

Katika taarifa iliyotolewa na TMA imeonyesha mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha Aprili 12, kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani inayojumuisha Visiwa vya Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara.

Pia mvua hiyo inatarajiwa kunyesh kesho kutwa, Aprili 13, katika mikoa hiyo n mikoa mingine kiwemo pia Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro.

Aidha mvua hiyo inatarajiwa kunyesha Aprili 14 kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, shinyanga, Kigoma, Katavi, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

"Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo.

Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Aprili 12 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Aprili 15, 2021.
 
Sitoshangaa Siku ya kesho kua na Jua kali la utosi.
Yaani huku kwetu sisi wakulima tukionaga tangazo lao la mvua, huwa tunatetemeka maana tunajua kifuatacho ni bonge la juaa!! Hapa kulikuwa na wingu ziitoo, lakini sasa jua limewakaa!! Tunawaomba hao TMA bora wakae kimya ili mvua ziendelee!!
 
Back
Top Bottom