Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
359
1,363
1715945551117.png

UWEPO WA KIMBUNGA “IALY” KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR​

Dar es Salaam, 17 Mei 2024:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.

Aidha, kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini. Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.

USHAURI: Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.

Imetolewa na:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

PIA, SOMA:
-
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa serikali kuhusu kimbunga Ialy na hali yake, Mei 19, 2024
 
Hivi hivi vimbunga nani his anavipa majina? Seriously 😂😂😂 Ni TMA wanakaa vikao kuamua hiki tukiite Hidaya hiki Fatuma au how do they come up with these names? Na kwanini majina ya watu na sio eneo ???Im curious
 
View attachment 2992545

UWEPO WA KIMBUNGA “IALY” KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR​

Dar es Salaam, 17 Mei 2024:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.

Aidha, kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini. Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.

USHAURI: Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.

Imetolewa na:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
huu sasa uchawi
 
Hivi hivi vimbunga nani his anavipa majina?
Wenye dunia yao! Usiwasifie sana TMA, wenye dunia yao huwapa taarifa hao TMA!

Tropical Cyclone Naming

WMO (World Meteorological Organization) maintains
rotating lists of names which are appropriate for each Tropical Cyclone basin. If a cyclone is particularly deadly or costly, then its name is retired and replaced by another one.

They are now maintained and updated by an international committee of the World Meteorological Organization.

The original name lists featured only women's names. In 1979, men's names were introduced and they alternate with the women's names. Six lists are used in rotation. Thus, the 2019 list will be used again in 2025.

Kimbunga hidaya kimemwita shosti wake Kimbunga latifa kwamba Bongo mababa ya kudanga mengi aisee
 
Back
Top Bottom