TMA yatahadharisha hali mbaya ya hewa baharini kwa siku 5 zijazo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa matarajio ya Hali Mbaya ya Hewa kwa siku tano zijazo na Athari zinazoweza kutokea. Hali mbaya baharini inaweza kuathiri shughuli za uvuvi.

Imetabiri kuwa na upepo mkali na mawimbi makubwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi, kwa jumla ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Utabiri huo umetolewa Jumapili, Juni 7, 2020 saa Tisa Alasiri

1591590930903.png
 
Watanzania hatuna utaratibu wa kufuatilia hali ya hewa yakitokea majanga ndio wa kwanza kulaumu serikali,na wakati mamlaka ya hali ya hewa washatoa angalizo kwa watu kuzingatia na kujiandaa kwa lolote.
 
Hakuna watu wanafuatilia utabiri wa hali ya hewa kma watu wa pwani....hasa wavuvi
 
... siku mbili tatu tulihabarishwa humu kupatwa kwa Mwezi; hizo ndio athari zake mihimili ya angani (heavenly bodies) ikijisigina japo "chafya" hatukwepi chini huku tuliko maana sisi ni particles or mere debris before the heavenly powers!
 
Watanzania hatuna utaratibu wa kufuatilia hali ya hewa yakitokea majanga ndio wa kwanza kulaumu serikali,na wakati mamlaka ya hali ya hewa washatoa angalizo kwa watu kuzingatia na kujiandaa kwa lolote.

Na ni lini labda Watanzania hawa unaowasema na kuwasemea hapa walikupa Jukumu la Kuwasemea kuwa wengi Wao hawafuatilii Hali ya Hewa?
 
Back
Top Bottom