TMA yatabiri mvua kubwa mikoa minne Tanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA) imetoa tahadhali ya mvua kubwa itakayonyesha katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa Morogoro leo Jumatano Januari 22, 2020.

Pia, TMA imetoa tahadhali ya upepo mkali na mawimbi makubwa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa ya TMA iliyotolewa jana Jumanne Januari 21,2020 inasema mvua hizo zitaanza mvua hizo zinaweza kuleta athari ikiwamo uharibifu wa miundombinu na mali na makazi kuzunguukwa na maji.

Athari zingine zinazoweza kutokea hatari kwa maisha ya watu kutokana na maji kutiririka kwa kasi, ucheleweshaji wa usafiri na kusimama kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wa tahadhali ya upepo mkali na mawimbi makubwa TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza katika mikoa hiyo kuathirika kwa shughuli za uvuvi, ucheleweshaji wa usafiri pamoja na kuanguka kwa majani na matawi ya miti.

Kesho Alhamisi Januari 23, 2020 imesema mvua kubwa inatarajia kunyesha katika maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Ijumaa ya Januari 24, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

TMA imesema Jumamosi ya Januari 25, 2020 mvua kubwa itanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma.
Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wananchi wakati wa kipindi hicho kuhakikisha wanachukua hatua.

Chanzo: Mwananchi
 
Mamlaka na raia wajiandae na madhara yanayoeza kusababishwa na mvua hizo.
 
Kwanza wamalize viporo vya mvua za siku tano tano mara tatu walizotuahidi lakini zote hazikunyesha.
 
Mamlaka na raia wajiandae na madhara yanayoeza kusababishwa na mvua hizo.
Kabisaa unawaamini TMA?
Mwenye kumbukumbu ya uzi uliopita walivyotabiri mvua kubwa mikoa ya Dodoma, Mbeya, Singida, Njombe n.k aulete alafu waje wakazi wa mikoa hiyo watuambie zilinyesha?
 
Kabisaa unawaamini TMA?
Mwenye kumbukumbu ya uzi uliopita walivyotabiri mvua kubwa mikoa ya Dodoma, Mbeya, Singida, Njombe n.k aulete alafu waje wakazi wa mikoa hiyo watuambie zilinyesha?
Bora niwaamini hata isiponyesha hamna shida. Ndio mamlaka zetu mkuu.
 
Kwanza wamalize viporo vya mvua za siku tano tano mara tatu walizotuahidi lakini zote hazikunyesha.

Ambacho huwa mnashindwa kuelewa ni nini..?

Neno tabiri ni kitu kuwa au kutokuwa!

Kuna namna wakipima huona viashiria vya kitu fulani hivyo huwa wanatabiri uwezekano wa kuwepo kwa mvua au lah!

Mazingira ya hali ya hewa Ni kitu kinachobadilika na kunaathari nyingi zinaweza pelekea hali hiyo.. una habari muda mwengine ndege huweza kuanguka pasipo hitilafu ila mabadiliko ya hali ya hewa..?

Hakuna mvua hakuna radi unashangaa ndege inaanguka! Hili hujitokeza ila mara chache na ni ngumu kuliepuka kama hauna vifaa vya kung'amua mashinikizo ya hewa.

Mkuu ule ni utabiri inaweza ikawa au isiwe.
 
Sikumbuki hata siku moja hao jamaa wakatabiri na ikawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom