TMA watahadharisha mvua za masika kwa mikoa kumi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imezitaka mamlaka za miji kuboresha mifumo ya maji taka ili kupunguza athari ya mafuriko zitakapoanza mvua za masika Machi, 2021.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Februari 18, 2021 na mkurugenzi wa huduma za utabiri wa TMA, Dk Hamza Kabelwa katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Alikuwa akieleza kuhusu utabiri msimu wa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza Machi hadi Mei, 2021.

Amesema mvua zinatarajiwa kunyesha katika Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma maeneo Kankoko na Kibondo.

“Mvua zinaweza kusababisha mafuriko, uharibifu wa miundombinu, watu kupoteza maisha pamoja na mali hivyo mamlaka za miji zinatakiwa kuchukua hatua ya kuboresha miundombinu ya maji taka kabla ya athari kujitokeza,” amesema.

Dk Kabelwa amesema maeneo yanayotarajiwa kupata mvua hadi juu ya wastani kuna uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kichocho, homa ya matumbo, malaria na homa ya bonde la ufa.

Kutokana na hali hiyo amezitaka mamlaka husika kuhakikisha zinapatikana dawa za kutosha katika vituo vya kutokea huduma ya afya kutokana na uharibifu wa miundombinu unaoweza kujitokeza.

Amesema katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia inatarajiwa kunyesha mvua za wastani hadi chini ya wastani huku wakulima wakishauriwa kulima mazao ya muda mfupi ili kukabiliana na hali hiyo.

Dk Kabelwa amesema mikoa hiyo itakayopata mvua za wastani hadi chini ya wastani kuna uwezekano wa kunyesha vipindi vifupi vya mvua kubwa zinazoweza kusababisha mafuriko.
 
Asante kwa taarifa TMA.taarifa kama hizi kwa sisi wakulima ni muhimu sana kuliko taarifa za kuunga juhudi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Hawa jamaa nawafuatilaga sana miaka mingi tu, na wapo wrong mara nyini sana wanapotabili masika.

Wamesema mikoa ya pwani ni chini wa wastani watu wapande mazao ya muda mfupi. Tusubiri uone maajabu utashangaa mvua inaanza march mpaka april tena heavy rain hata waliopanda mpunga kama sisi Mwezi February tukavuna mpaka kugalagala
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imezitaka mamlaka za miji kuboresha mifumo ya maji taka ili kupunguza athari ya mafuriko zitakapoanza mvua za masika Machi, 2021
Kuzitaka Mamlaka za miji kuboresha mifumo siyo kazi yake, yeye anatakiwa kutoa taarifa ya kiwango cha mvua tu.
 
Lile daraja la m300 pale jangwani limefikia hatua gani? Mlioko Dar tupeni mrejesho.
Hakuna Lolote Linalofanyika

Zaidi Kuna Bulldozer Zinafukua Mchanga Unaoletwa Na Maji

Hapo Ndiyo Uwezo Wa Wasomi Wetu
 
Sasa tufanyeje, tutengeze Safina au?

Hawa jamaa hamna kitu kabisa hapo ukiona wamesema hivo ujue wameangalia data za mwaka jana miezi kama hiyo mjua ilinyesha kwahiyo wanadhani na leo itajirudia.
 
Back
Top Bottom