TMA: Kuna uwezekano wa kuwepo Mvua za EL Nino kwa 60%

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,432
49,096
TMA inasema Kuna uwezekano wa kuwepo Kwa mvua za EL Nino Kwa 60% .

Hii nakubaliana nayo maana ni mwezi wa 5 Sasa Bado mvua ni nyingi licha ya mazao kukomaa hivyo yanaanza kuharibika..

Tujiandae Kisaikolojia

---

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema inafuatilia mifumo ya hali ya hewa kuhusu kunyesha kwa mvua za El Nino baada ya kuonesha kuwa mpaka sasa kuna uwezekano wa kunyesha mvua hizo kwa asilimia 60.

Hatua hiyo inatokana na taarifa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) iliyoeleza kunyesha kwa mvua hizo nyingi katika nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Mashariki ya mbali na Amerika ya Kati. Mvua hizo ambazo zimekuwa zikinyesha kila baada ya miaka miwili na kwa mara ya mwisho nchini zilinyesha mwaka 2016 na kusababisha madhara yakiwemo mafuriko.

Kaimu Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri TMA, Dk Mafuru Biseke alisema kwa sasa mifumo ya hali ya hewa inaonesha joto la Bahari ya Pasifiki kuongezeka katika eneo la kati na kuonesha uwezekano wa kunyesha kwa mvua hizo kwa asilimia 60.

Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom