TMA kama tayari Wakenya wameshatahadharishwa leo kuwa kuna hatari kubwa ya ‘ Kimafuriko ‘ inakuja mbona Kwetu mmenyamaza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya na idara ya hali ya anga zimeonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mafuriko katika kipindi cha siku nne zijazo katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.
Maeneo yaliyopo hatarini ni pamoja na jiji la Nairobi na Mombasa.

Chanzo Taarifa: ITV Tanzania ( na ni taarifa iliyotolewa Masaa Matatu tu yaliyopita )

Nimehoji hivyo kwakuwa ‘ Kijiografia ‘ inajulikana kuwa hata ‘ Mfumo ‘ wa Mvua wa Maeneo mengi ya Tanzania hasa kwa Mikoa ya Pwani kama ya Dar es Salaam na hata ule wa Nairobi haupishani sana na Mikoa ya Mombasa na Nairobi iliyopo nchini Kenya.

Sasa kama tayari Wenzetu hao ( Majirani ) Wakenya wameshaambiwa kuwa ndani ya Siku Nne ( 4 ) zijazo inakuja Mvua moja Kubwa sana na itakayokuwa na Madhara hayo ya ‘ Kimafuriko ‘ inakuwaje nyie TMA nanyi hamjatuweka sawa Sisi Watanzania ili nasi tujue mapema na tuanze Kujiandaa Kisaikolojia?

Ngoja nianze mapema Kuchukua Mazoezi ya Kuogelea hasa ya Kuvuka vyema Jangwani, Msimbazi, Kigogo, Mto Mbezi na mingineyo iliyopo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam huku pia nikibeba kabisa na Dawa mbalimbali hasa zile za Kunikinga na Kipindupindu kama Kitaibuka hapa katikati ndani ya hizi Mvua Kubwa ambazo zinaenda Kuja kama ambavyo zitawaanzia Ndugu zetu na Majirani ( Mashemeji ) Wakenya.
 
Kaka Niko Tanga tangu saa tisa usiku mpaka muda huu mvua inamwagika..kuna giza japo inaelekea saa moja asubuhi..hali ikiendelea hivi ni maafa..Mungu aepushie mbali.
 
Back
Top Bottom