TLS yapinga Marekebisho ya Sheria ya kuwakataza watumishi wa Serikali kugombea

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Dodoma. Chama cha Wanasheria nchini (TLS) kimepinga Marekebisho ya Sheria ya TLS yanayolenga kuwakataza watumishi wa Serikali na viongozi wa kisiasa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho kikieleza kuwa marekebisho hayo yanawabagua wanachama.

Akizungumza leo Agosti 24 wakati wadau wa masuala ya sheria wakitoa maoni yao kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, mwakilishi wa TLS, Jebra Kambole alisema marekebisho hayo pia yanalenga katika kumfanya mwanachama mmoja kuwa na nguvu kuliko wengine.

TLS ilikuwa ikitoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria namba mbili wa mwaka 2018.

“Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mwanachama wetu, anapelekewa kanuni kwa ajili ya kupitisha ni wazi hapa mwanachama huyu anakuwa na nguvu kuliko wanachama wengine,”alisema.

Alitaja sababu nyingine ya kupinga mapendekezo hayo ni pale Mwanasheria Mkuu wa Serikali AG atakapopewa mamlaka ya kupitisha kanuni, chama hicho hakitakuwa na uhuru wa kujiendesha.

Mbunge wa Malindi (CUF) Ally Saleh alitaka TLS kiwashawishi kwa nini mkono wa Serikali usiingie katika chama hicho.

Hoja ya Saleh iliungwa mkono na mwenyekiti wa kikao hicho, Dk Damas Ndumbaro ambaye alikitaka chama hicho wakati kinajibu swali hilo kutoa mifano ya bodi nyingine ambazo Serikali haitengenezi kanuni.

“Pia mmesema kuna ubaguzi sasa ikitokea siku Rais anagombea uraisi je mtamruhusu? Tuchukue mfano Rais Magufuli ni mwanachama wa TLS na uchaguzi uko Februari mwakani mtamruhusu agombee? Kama sheria inaruhusu nani atamzuia?” Alihoji Dk Ndumbaro ambaye pia ni mbunge wa

Songea Mjini (CCM).

Dk Ndumbaro ambaye pia ni mwanachama wa siku nyingi wa TLS alisema kumekuwa na mabadiliko ya majukumu ya TLS kutoka katika kushughulikia taaluma na kujiingiza katika siasa.

Akijibu hoja hizo, Kambole alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja kuhusu upitishaji wa kanuni za uendeshaji kwa bodi nyingine lakini kuna tofauti kubwa kati yao na bodi nyingine za kitaaluma.

“Huwezi kukuta daktari anakutana na daktari wa serikali lakini sisi katika mashauri huwa tunakutana na AG sisi upande huu mwingine. Lakini pia chama chetu hakina fungu lolote linalotoka Serikalini, ni michango ya wanachama wenyewe,”alisema.

Alisema iwapo mwanachama anayelipa michango yake ataomba uongozi hata kama ni mtumishi wa Serikali atapigiwa kura sawa na wanachama wengine.

Akizungumzia hoja hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi alisema sehemu ya 14 ya sheria hiyo inapendekeza kurekebisha Sheria ya TLS, Sura ya 307.

Alisema marekebisho hayo yanalenga kuweka vigezo ambavyo vitatumika kwa wajumbe wa baraza na taratibu za

kuzifuata wakati wa utungaji wa kanuni zinazosimamia chama hicho.

“Kwa ufupi mapendekezo ya marekebisho ya sheria hii yana lengo la kuweka masharti ya kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuzipitisha kanuni zinazotungwa na chama kabla ya kuchapishwa. Pia kanuni hizo zitachapishwa kwenye Gazeti la Serikali,”alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
..Dr.Ndumbaru aache kutisha wenzake.

..ikitokea Raisi wa Jamhuri ni mwanachama wa TLS na akagombea nafasi yoyote ile basi hatima yake itakuwa mikononi mwa wanachama wenzake watakaompigia kura.

..kwa maoni yangu, Raisi atapaswa kutumia busara zake kuona kama "inaswihi" kwa kiongozi wa nchi kugombea nafasi ktk chama cha kitaalamu ambacho yeye ni mwanachama.
 
Hiyo itakuwa sawa na baba kwenda kuposa mdogo wa mke wa mtoto wake (mdogo wa mkwewe)
 
Dr Ndumbaru hana maana toka awe Mbunge..
Ukishakuwa CCM sijui kwanini kichwani lazima kuwe hamnazo.
 
Walau tunaanza kuwasikia TLS kwenye mambo ya msingi. Kushinda twita mnajibizana na akina Pole pole waachieni Chadema.

Nyie tusaidienii kwenye maswala ya kisheria bila kuchanganya na siasa. Ukweli ni kwamba TLS hii imekuwa na siasa kuliko wakati wowote hata kipindi ikiongozwa na makada wa CCM.

Wanaharakati mnafanya mshindwe kuaminika sometimes. Hatujawahi kusikia kiongozi wa TLS akijibizana na viongozi wa Chadema achilia mbali CCM. Turudishane kwenye mstari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaaaaa, Kutunga sheria kwa ajili ya kubana kikundi flani ni kama laana ambayo mara nyingi huwarudia hao hao walionuia kuumiza wenzao.Mfano sumaye na Lowassa wangekuwa fair kwa upinzani na kuweka sheria zenye usawa juu ya vyama vingi leo wangefurahia fursa hiyo. Walikuwa miongoni mwa vinara wa mbinu chafu juu ya upinzani leo wako wapi sembuse ndumbaro na magamba kabudi!. Hii ni dunia wote hatujui kesho tuwe fair, tusikomoane, sheria ziwe za nia njema na kwa wote.
 
Walau tunaanza kuwasikia TLS kwenye mambo ya msingi. Kushinda twita mnajibizana na akina Pole pole waachieni Chadema. Nyie tusaidienii kwenye maswala ya kisheria bila kuchanganya na siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
: watanzania wengi ni wanafiki, kwenu siasa ni uovu zinavyofanywa na upande wa pili tu! Miaka yote mmeweka watu wenu hazikuwa siasa! Sasa upande wa pili wamefanikiwa kuweka watu wao mmetunga miswada! Dunia ya Mungu.
 
Walau tunaanza kuwasikia TLS kwenye mambo ya msingi. Kushinda twita mnajibizana na akina Pole pole waachieni Chadema.

Nyie tusaidienii kwenye maswala ya kisheria bila kuchanganya na siasa. Ukweli ni kwamba TLS hii imekuwa na siasa kuliko wakati wowote hata kipindi ikiongozwa na makada wa CCM.

Wanaharakati mnafanya mshindwe kuaminika sometimes. Hatujawahi kusikia kiongozi wa TLS akijibizana na viongozi wa Chadema achilia mbali CCM. Turudishane kwenye mstari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi nchi hii kuna kitu ambacho si siasa? Hiyo ndiyo faida ya kuzuia siasa nchini, kila nafasi itakayopatikana Iwe Twitter, misiba etc people make use of it.... Halafu kujaribu ku contain kila anayetoa hoja kinzani dhidi yako ni bureee tuu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
: watanzania wengi ni wanafiki, kwenu siasa ni uovu zinavyofanywa na upande wa pili tu! Miaka yote mmeweka watu wenu hazikuwa siasa! Sasa upande wa pili wamefanikiwa kuweka watu wao mmetunga miswada! Dunia ya Mungu.
Maovu ya CCM si tiketi ya nyie kufanya hayo hayo. Nimesikia wanasiasa wenu wakiapa kulipa kisasi kwa CCM mara mbili ya wanayotendewa leo na wao watatesa hadi kuku zao wakipewa nchi!!

Sasa mkifanya wanayofanya CCM tutawatofautishaje sasa? Si mtakuja kutuambia CCM waliiba escrow sisi tumeiba kaescrow?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi nchi hii kuna kitu ambacho si siasa? Hiyo ndiyo faida ya kuzuia siasa nchini, kila nafasi itakayopatikana Iwe Twitter, misiba etc people make use of it.... Halafu kujaribu ku contain kila anayetoa hoja kinzani dhidi yako ni bureee tuu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewahi kusikia chama cha wahasibu, mainjinia n.k wakilumbana na akina Polepole? It's simple ...wajirekebishe ...yapo mengi kwenye sheria zetu ya kufanyia kazi ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maovu ya CCM si tiketi ya nyie kufanya hayo hayo. Nimesikia wanasiasa wenu wakiapa kulipa kisasi kwa CCM mara mbili ya wanayotendewa leo na wao watatesa hadi kuku zao wakipewa nchi!!

Sasa mkifanya wanayofanya CCM tutawatofautishaje sasa? Si mtakuja kutuambia CCM waliiba escrow sisi tumeiba kaescrow?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni dhambi gani chama cha wanasheria kuongelea sheria kandamizi?, au tatizo ni itikadi za anaezitoa?. Watu wameziiwa kufanya siasa anachofanya polepole ni maoni ya katiba mpya! Chaguzi ndogo za ununuzi wa wabunge ni nini kama sio siasa kwanza siasa chafu!. TLS ikisema inawakera sasa tuwabane.,,, peleka miswada. Mlitaka muwa control ! Angekuwa mwenyekiti ndumbaru usingeona hiyo miswada maana issue za kuishauri serikali ange mute! Hasa juu ya ukanyagaji wa katiba! Shangazi anawakera tunajua! Kaka wa taifa nae alisukwasukwa mpaka mda wake ukaisha!
 
Umewahi kusikia chama cha wahasibu, mainjinia n.k wakilumbana na akina Polepole? It's simple ...wajirekebishe ...yapo mengi kwenye sheria zetu ya kufanyia kazi ....

Sent using Jamii Forums mobile app
: hujui uhusiano wa TLS jamii na serikali wewe! Au unafanya maksudi!. Hata mahakamani wasiende kwa kuwa mainjinia hawaendi!una uwezo zaidi ya ulichoandika!
 
Umewahi kusikia chama cha wahasibu, mainjinia n.k wakilumbana na akina Polepole? It's simple ...wajirekebishe ...yapo mengi kwenye sheria zetu ya kufanyia kazi ....

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi kusikia kwa sababu issues zao haziwagusi wanasiasa, hasa walioko madarakani. Hata TLS kabla ya Lissu haikuwa ikifuatwa fuatwa. Ni jambo baya sana kukimbilia kubadilisha sheria kwa kila kitu kidogo ilimradi tuu kuwabana watanzania wenzako ambao wanakushinda kwa mijadala, tena ya kawaida. Nimesikia pia baada ya sakata la TWAWEZA wanaandaa muswaada mpya.... Mwisho wa siku inawakuta na wao just like waluvyofanya akina Lowassa, Sumaye, Nappe etc enzi zao....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo itakuwa sawa na baba kwenda kuposa mdogo wa mke wa mtoto wake (mdogo wa mkwewe)
Mfano wako ni sawa kusema baba ni mdogo wa mkwewe. Yaani rais kuwa mwanachama wa chama fulani ni sawa. Ila kugombea nafasi za uongozi sio sawa
 
Back
Top Bottom