TLS: Uchaguzi wa wasomi - Je watatuonyesha Usomi ?

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,465
Kati ya matokeo ya uchaguzi yanayosubiriwa kwa hamu ni Rais wa TLS mjini Arusha.

Chama hiki kimeweza kujidani na shughuli zake kujulikana kwa jamii ya watanzania ingawa kipo zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Wakili na mwanasiasa machachari ndani ya mahakama na bungeni alipochukua form ya kugombea - Rais wa nchi na waziri wa sheria na katiba wametishia kukifuta chama hiki kama nguli wa sheria atachaguliwa.

Woga wa ikulu umejidhihirisha wazi baada ya kumwandama Tundu Lissu - kumfunga na kumshitaki kila siku ili asihudhurie uchaguzi huu.

Nendeni Arusha mawakili wote mchagueni Tundu Lissu kibuyu kipasuka- wengi tunataka kujua kuna nini ndani ya kibuyu.
 
Sirikali ilikuwa haijui kuwa Tundu Lissu ni mtundu wa sheria.
Hivi angekuwa anagombea urais wa nchi sijui ingekuwaje
 
Majina haya usije ukampa mwanao, Mpinzile, Wasonga na Bashite....Twende na Lissu kwa manufaa makubwa ya nchi yetu.
Yaaani endapo hao mawakili watashindwa kuwa wamoja na kumchagua lisu kuwa rais wao!! Basi tena nitajua kumbe ndio maadui namba moja wa sisi walala hoi!! Na dunia nzima itawacheka!! Kwani kama ni kudharirika wamedharirishw sana kwa matamko ya kimzuka mzuka!
 
Hii thread mbona haichangiwi na watu waliokwenda shule tupate tupate vionjo vya maana. Naona minyumbu inajitekenya na kujichekesha, duh kumbuka bado hamjavuka mto mara!!! You will see the music
 
Ukitaka Kujuwa Tz kuna Watu wa Hovyo Lissu anaweza kushindwa kwa Kura.
 
TLS kipo ICU ni Lissu wa kukiokoa ama kukiacha kife mikononi mwa wanasheria wa siri kali wanaopinga hata haki ya mtu pale mahakamani kwa ule usemi mtumikie kafiri upate mradi wako
 
Lissu akigombea uraisi 2020 itakuwaje kwa watawala ikiwa sasa tu wanamgwaya na kumpa kiki
 
Ccm wanachoogopa TLS ikiwa huru 2020 tutaruhusiwa kulinda kura umbali wa mita 200, itapelekea idadi ya wabunge wa upinzani kuzidi wa ccm hata kama watapiga bao la mkono kura za urais.
 
Back
Top Bottom