TLS ni mali ya umma, sheria ya TLS imetungwa na Bunge

Mligo Augustino

Senior Member
Nov 29, 2017
126
278
Sheria inayounda chama cha mawakili Tanganyika/TLS imetungwa na Bunge. Bunge ni mali ya wananchi/umma. Wakili Kambole anajiongoza vibaya kusema TLS siyo mali ya umma. Labda anachanganya kati ya serikali na umma. Hivi ni vitu viwili tofauti.

From legal point of view TLS ni mali ya umma. Kwamba eti serikali haihusiki kwenye administration ya TLS.Hii ni mipango tu ambayo inaongeleka.

Hii hoja haiondoi ukweli kuwa TLS ni mali umma/wananchi.The law establishing TLS is Tanganyika Law Society Act of 1954(CAP 307).

Mwenye mamlaka ya kuifuta TLS ni Bunge tu. Hata mawakili wakifanya mkutano(AGM) wakaamua kuifuta TLS, hawawezi. Hawana mamlaka.

Note: Bunge la JMT = RAISI +WABUNGE(ibara ya 62(1) ya katiba ya JMT 1977)

Kumbe NGO,Private companies nk zinafutwa na msajiri wa taasisi husika kama BRELA,RITA nk.

Kwa mujibu wa kifungu 4 (1)(b) of the Advocate's Act CAP 341 Mwanasheria Mkuu wa serikali au Naibu wake au DPP ni ex officio wajumbe wa Disciplinary Committee ya mawakili(Advocates' Committe). Je kama TLS siyo ya umma AG(serikali)kwanini ameingizwa kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili?

Tena kifungu 4(5) of Advocates Act kinasema ilikutengeneza quorum of the committee Mwanasheria mkuu wa serikali lazima AWEPO. Je kwanini bunge linataka mwanasheria mkuu wa serikali(serikali) awe necessary part kwenye kamati ya maadili ya mawakili?

Kifungu cha 11 cha Advocates Act kinasema wazi yakwamba Attorney General ana mamlaka ya kupokea information toka kwa yeyote yule inayohusu wakili na kuipeleka kwenye kamati ya maadili. Je kwa nini bunge lilimpa mamlaka hayo AG ya kinidhamu kama TLS siyo mali ya umma?

Conclusion: The legal findings herein above suggest and entail that TLS ni MALI ya UMMA.

Note: Hii ishu ni ya kisheria. Wanaopinga waje na facts za kisheria. Nilivyoona wanaopinga hawana legal facts. Ni mihemko tu. Ruzuku siyo hoja. Hata NSSF,NHIF,PSPF ni taasisi za umma lakini hazina ruzuku toka serikalini.
 
Nadhani alichomaanisha Magufuli ni kwamba TLS lazima iwe "controlled" na mkono wake kama anavyotaka kuzicontrol TBC, BOT, TRA au "mali nyingine ya Umma" anayoipa Ruzuku. Wakili Kambole anapingana na hilo. Magu hawezi kusema TLS ijump nayo ikajump bila kuuliza why.

Ila kuwa chini ya Jiwe ni mtihani mkubwa sana. Wasomi kama AG, CAG na wengine wooote wamegeuzwa mazwazwa wa kutupwa na kila wanapoitwa Ikulu wanaenda washajipanga kukubali kila wanachoambiwa maana Jiwe halikawii kuagiza lolote.
 
TLS Sio Ya Umma. Ni Ya Mawakili Tu. Kama Kuna Wanachama Mbali Na Mawakili Bhasi Naunga Mkono Hoja.
Huwezi kusema Bunge ni mali ya wabunge tu. Bunge ni mali ya umma. Huwezi kusema mahakama ni mali ya majaji na mahakimu tu. Mahakama ni mali ya umma. The sama applies to TLS. TLS siyo mali ya mawakili tu. TLS ni mali ya umma.
 
Bunge Ni Chama? TLS Ni Chama. Wabunge Wanachaguliwa Na Umma. Mawakili Hawachaguliwi Na Umma. Mawakili Wanalipa Ada Ili Kuendesha Chama Chao Hawapokei Ruzuku Yeyote Kutoka Serikalini. Hayo Mambo Ni Ushahidi Tosha TLS Sio Ya Umma Kama Ilivyo Bunge, Serikali Na Mahakama.

TLS Is A Professional Society Not A Public Society.

Kimajukumu Inagusa Umma Wa Tanzania. Hapa Sikatai.
 
Huwezi kusema Bunge ni mali ya wabunge tu. Bunge ni mali ya umma. Huwezi kusema mahakama ni mali ya majaji na mahakimu tu. Mahakama ni mali ya umma. The sama applies to TLS. TLS siyo mali ya mawakili tu. TLS ni mali ya umma.
Duh, kazi ipo! Kilangila.
 
Nadhani alichomaanisha Magufuli ni kwamba TLS lazima iwe "controlled" na mkono wake kama anavyotaka kuzicontrol TBC, BOT, TRA au "mali nyingine ya Umma" anayoipa Ruzuku. Wakili Kambole anapingana na hilo. Magu hawezi kusema TLS ijump nayo ikajump bila kuuliza why.

Ila kuwa chini ya Jiwe ni mtihani mkubwa sana. Wasomi kama AG, CAG na wengine wooote wamegeuzwa mazwazwa wa kutupwa na kila wanapoitwa Ikulu wanaenda washajipanga kukubali kila wanachoambiwa maana Jiwe halikawii kuagiza lolote.
Kama anavyocontrol bunge yaani kama north Korea
 
Bunge Ni Chama? TLS Ni Chama. Wabunge Wanachaguliwa Na Umma. Mawakili Hawachaguliwi Na Umma. Hayo Mambo Mawili Ni Ushahidi Tosha TLS Sio Ya Umma Kama Ilivyo Bunge, Serikali Na Mahakama.

TLS Is A Professional Society Not A Public Society.

Kimajukumu Inagusa Umma Wa Tanzania. Hapa Sikatai.
Kama ni chama cha hinafsi,je kwa nini Bunge ambayo ni taasisi umma/wananchi ilitunga sheria inayounda TLS? Je tuseme bunge lilijipendekeza kwa mawakili? Kwa nini mawakili wasingeunda chama chao kwa kutengeneza katiba ya chama?Bunge linatunga sheria kwaajili ya matumizi ya umma.TLS ilianzishwa na Binge kama taasisi ya umma.
 
vp bodi ya wahasibu NBAA Ambayo rais huunda bodi ya wakurugenzi je ni mali ya umma? pale husajiriwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu nayo sio mali ya umma?

TLS husevu matakwa ya umma, ndio maana mali ya umma, wachana na mafunzo ya mkemia zero brain unless u want to be in wining side and not the truth
 
Sheria inayounda chama cha mawakili Tanganyika/TLS imetungwa na Bunge. Bunge ni mali ya wananchi/umma. Wakili Kambole anajiongoza vibaya kusema TLS siyo mali ya umma. Labda anachanganya kati ya serikali na umma. Hivi ni vitu viwili tofauti.

From legal point of view TLS ni mali ya umma. Kwamba eti serikali haihusiki kwenye administration ya TLS.

Hii ni mipango tu ambayo inaongeleka.Hii hoja haiondoi ukweli kuwa TLS ni mali umma/wananchi.
Wewe jamaa wa ajabu sana. Unataka kumaanisha kila kilichotungiwa sheria na Bunge ni Mali ya umma? Kwa maana unayoisemea hata makampuni binafsi ni Mali ya umma au hata NGOs!
 
Kama ni chama cha hinafsi,je kwa nini Bunge ambayo ni taasisi umma/wananchi ilitunga sheria inayounda TLS? Je tuseme bunge lilijipendekeza kwa mawakili? Kwa nini mawakili wasingeunda chama chao kwa kutengeneza katiba ya chama?Bunge linatunga sheria kwaajili ya matumizi ya umma.TLS ilianzishwa na Binge kama taasisi ya umma.
Wapi Nimesema Ni Chama Binafsi?
Tafadhali Usiniwekee Maneno.
Bunge Halitungi Sheria Za Mashirika Binafsi Pamoja Na Sekta Binafsi ?
Hoja Zako Ni Za Kitoto Sana.
 
Back
Top Bottom