TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Hongereni TLS.
Nahisi ndio maana mh Rais alisita kidogo kumtaja majaliwa kama waziri mkuu wa Tz wakati anatoa heshima zake kwa viongozi wengine kabla ya hotuba yake kwa wananchi.
Kumbe na wewe uliona.

Mama Samia alisita kidogo kutamka kama Waziri Mkuu.
 
Mjadala huu mtamu sana watu wanauliza vifungu kwenye katiba vinavyosema kuhusu waziri mkuu Rais aliye madarakani anapo fariki!

TLS hoja zao zinazua maswali sana na ni assumptions tuu!
Maana kuna maana kubwa kama kwenye muktadha husika katiba inaponyamaza kuhusu waziri mkuu!

Mbona kwa Vice iko wazi kabisa? Hata kama katiba yetu ina mapungufu wasingeliweza sahau swala la PM kama kweli linahitaji kwenye muktadha tulionao!

Kuna maana kubwa sana katiba kutosema chochote kuhusu PM!

Mimi niko hapa nafatilia uzi huu nipewe vifungu.
 
TLS kwa mara ya kwanza nimeona mmetekeleza wajibu wenu wa kisheria kwenye nchi hii. Mawaziri wote ikiwemo waziri Mkuu inabidi waambiwe, na wasiendelee kutokea kwenye nafasi zao kwani kwa sasa hakuna baraza la mawaziri. Nimemuona Majaliwa akiendelea kutambulishwa kama waziri Mkuu, wakati kikatiba hana uhalali huo. Tungekuwa na vyombo vya habari vinavyotekeleza wajibu wao walipaswa kulitangaza hili wazi wazi kuwa kwa sasa hakuna baraza la mawaziri, na waziri yoyote aliyekuwa kwenye baraza lililopita asiendelee kuingia ofisini au kutumia mali za ofisi kama gari nk, wakati hana uhalali huo.
Kwenye mazishi ya viongozi wa juu serikalini waziri mkuu ndiye mwenyekiti wa kamati ya mazishi katibu wake ndiye katibu wa mazishi wajumbe ni waziri wa fedha wa bara na visiwani na baadhi ya mawaziri, hivyo kama katiba haiwatambui kama mawaziri na katiba hiyohiyo inawapa hayo majukumu ya kushughulika na maziko basi kwa upande huo katiba inahitaji marekebisho.
 
Law interpretation ya ajabu kabisa hii. Utasemaje hakuna Baraza la Mawaziri wakati halijavunjwa? Halafu kifungu mlichoquote kina husiana na kuunda Baraza likiwa limevunjwa. Someni vizuri Katiba na kuitafasiri vizuri.
 
Labda uwaziri utakoma baada ya kupata makamu wa Rais make kiti cha Rais bila makamu hakijatimia hivyo serikali ya mama SSH Haijakamilika.
 
Asante TLS kwa kutoa ufafanuzi huu. Kama nimeelewa vizuri andiko hili, Ina maana kikao Cha leo alichoendesha Mh. Madame President na Baraza la mawaziri baada ya Kula kiapo Ni batili? Yaani null and Void. TLS please fafanua hili.
 
Back
Top Bottom