TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Oct 15, 2018
17
153
Mnamo tarehe 19 Machi 2021, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kufuatia kifo cha Raisi Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Kuapishwa kwake kunaibua suala la msingi la kikatiba juu ya kuendelea au kutoendelea kuwapo kwa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Hayati Raisi John Magufuli.

Baraza la Uongozi la TLS, kwa kutambua wajibu wake wa kisheria chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Tanganyika Law Society Act Sura ya Namba 307 wa kutoa ushauri kwa Serikali, Bunge, Mahakama, na Umma linapenda kutoa mwongozo wa nini kinatakiwa kufanywa kutokana na tukio kubwa la kihistoria ya nchi yetu la kupata Raisi mpya baada ya Raisi wa nchi kufariki.

Katika kutoa Mwongozo huu Baraza la Uongozi lilijiuliza swali lifuatalo:

Je, Katiba inalazimisha au inamtaka Raisi aunde na aapishe Baraza la Mawaziri pindi anapotwaa madaraka baada ya Raisi kufariki?


Kujibu swali hili mtu analazimika apitie ibara mbali mbali za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa ili kuweza kupata mtiririko wa kisheria na kimantiki. Ibara moja haitakiwi kusomwa peke yake bali moja baada ya nyingine ambazo zinawiana. Hivyo kanuni ya uwianishaji/ulinganishaji (harmonization) lazima itumike.

1. Kwa mujibu wa ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pindi Raisi:
a. anapofariki;au
b. kujiuzulu; au
c. kupoteza sifa za uchaguzi; au
d. kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili; au
e. kushindwa kutekelezwa kazi na shughuli za uraisi;

basi Makamu wa Raisi ataapishwa na atakuwa Raisi kwa muda uliobaki wa kipindi cha miaka mitano.

2. Makamu wa Raisi hawi Raisi kutokana na kiapo chake cha kwanza alichoapa wakati anaapishwa kuwa Makamu wa Raisi bali pale anapoapishwa kutwaa madaraka baada ya kutokea kwa moja kati ya mambo matano yaliyoanishwa hapo juu.

3. Baada ya hapo Raisi mpya (aliyekuwa Makamu) ana jukumu la kumteua mtu mwingine baada ya kushauriana na chama chake kuwa Makamu. Mteule huyu lazima athibitishwe na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia 50 ya wabunge wote wa Bunge hilo.

4. Makamu wa Raisi mteuliwa kwa mujibu wa Ibara ya 30(5) naye anatakiwa kuapishwa na Jaji Mkuu, kama ilivyo kwa Makamu wa Raisi aliyechaguliwa kuwa Makamu pamoja na Raisi wakati wa uchaguzi mkuu kwa mujibu wa ibara za 42(5) na 49; au aliyeteuliwa na kuthibitishwa kuwa Makamu wa Raisi kwa mujibu wa Ibara ya 50(4).

Baraza la Mawaziri

5. Sehemu ya Tatu ya Sura ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inazungumzia Baraza la Mawaziri. Ibara ya 51(2) inatamka ifuatavyo:

Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuuungwa mkono na Wabunge walio wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na wabunge walio wengi. (Mkazo umeongezwa)

Hivyo ni wazi kabisa kuwa Raisi wa nchi yetu awe wa kuchaguliwa ama wa kuapishwa kutokana na ibara ya 37(5) anatakiwa kumteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14 baada ya yeye kuwa Raisi.


6. Ibara ya 51(1) ya Katiba inataka Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Raisi kabla ya kushika madaraka yake kuapa mbele ya Raisi kiapo kilichowekwa na Bunge.

7. Aidha, Raisi baada ya kumteua Waziri Mkuu, na Waziri Mkuu huyo kuthibitishwa na Bunge na kumuapisha, ndipo anatakiwa kuteua mawaziri wengine na manaibu mawaziri kwa mujibu wa Ibara ya 55(1).

8. Ibara ya 56 ya Katiba inatamka:

Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. (Mkazo umeongezwa)

9. Ielew.eke kiapo hicho lazima kifanywe kwa Raisi aliyepo na si yule aliyeondoka madarakani kwani kiapo kwa Raisi mmoja hakimishwi kwa Raisi mwingine. Ndiyo maana hata aliyekuwa Waziri chini ya Raisi huyo huyo pindi akiteuliwa kuwa Waziri wa wizara nyingine tofauti na ile ya kwanza ni lazima aape upya.

10. Ibara ya 57(2) inazungumzia uwazi wa nafasi ya Waziri au Naibu Waziri kitu ambacho chaweza kutokea ikiwa mojawapo ya mambo yafuatayo:

a. Kujiuzulu au kufariki;
b. Kukoma kuwa mbunge;
c. Raisi atafuta uteuzi wake na kumuondoa kazini;
d. Akichaguliwa kuwa Spika;
e. Waziri Mkuu akijiuzulu au kiti cha Waziri Mkuu kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;
f. Unapowadia muda wa Raisi mteule kutwaa madaraka yake;
g. Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi wa yeye kukiuka maadili; (Mkazo umeongezwa)

11. Usomaji wa pamoja wa ibara ya 51(2) na ibara ya 57(2)(e) unatufanya tuseme, kwa kujiamini kabisa, kuwa mara tu baada ya Raisi kuapishwa kuwa Raisi anatakiwa kumteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14 tokea kuwa kwake Raisi. Waziri Mkuu aliyepo wadhifani anahesabika kutokuwa Waziri Mkuu na hivyo Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjika kutokana na Waziri Mkuu kutokuwepo “kwa sababu nyingine yoyote”. Sababu nyingine yoyote ni “kufariki kwa Raisi aliyemteua na kusimikwa Raisi mpya ambaye siye aliyemchagua.”

Baraza la Uongozi la TLS linaamini kuwa Mwongozo huu utaiwezesha nchi yetu kuweza kusonga mbele huku ikiwa imefuata kwa usahihi na uaminifu mkubwa misingi na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hivyo kuhakikisha kuwa Baraza la Mawaziri na uongozi wa nchi yetu una uhalali wa kikatiba na kisheria.



Umetolewa leo tarehe 19 Machi 2021 Jijini Dar es Salaam kwa Amri na Mamlaka ya Baraza la Uongozi la TLS.

Dkt. Rugemeleza A.K. Nshala

Raisi

[/CENTER]
 

Attachments

  • Mwongozo wa TLS juu uundwaji wa Baraza Jipya la Mawaziri la JMT-Final.pdf
    190 KB · Views: 29
Mwongozo wa TLS juu ya uundwaji wa serikali mpya kufuatia mama Samia Suluhu Hassan kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Source : wakili tv

N.B
Hivi ndivyo inatakiwa wadau, wananchi wenye uzoefu au vyama vya kitaaluma n.k kuchangia mawazo na ushauri wao kwa uwazi ili serikali iliyopo madarakani iweze kuwajibika na kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Ni mwanzo mzuri. Tunaanza vizuri kwa kutoa ushauri ni mategemeo serikali itakuwa sikivu na shirikishi kwa kukubali ushauri murua kama huu.

Photo: H.E Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania.

Tutakuwa tunaipima serikali hii mpya kwa kulinganisha na Bandiko hili zuri linalotoa muongozo kwa viongozi.

Na pia kubwa ni kuwa limetufungua macho kwa kutufahamisha wananchi wa kawaida serikali iendeshwe vipi baada ya kutokea msiba wa mkuu wa nchi kufariki akiwa ofisini yaani bado anatumikia muhula wake wa uongozi.

Tumechoka kuona masuala haya yanajadiliwa, kuchambuliwa kwa ufasaha kwa niaba yetu nje ya mipaka ya nchi yetu mama Tanzania, mfano vyombo vya media, vyama vya kitaaluma na wananchi wenye uzoefu Kenya wamekuwa mstari wa mbele kutuchambulia hali iliyopo Tanzania kufuatia msiba huu mkubwa huku kumbe ndani ya Tanzania kuna wadau wazalendo kabisa wanaweza kutoa mchango tena kwa lugha adhimu ya kiSwahili safi kila mtanzania akaelewa.

Inaleta simanzi kwanini wataalamu wetu hawahojiwi wala kujitokeza kuelezea hali halisi ya nchi yetu na badala yake ulimwengu unafahamishwa yanayoendelea au katiba yetu toka miji ya Johannesburg, Nairobi, Abuja badala ya dunia kupata hali halisi toka Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, University of Dar es Salaam, Tanganyika Law Society au ITV , AZAM n.k
Advocate Sipho Mantula from Unisa's Thabo Mbeki African School on Public and International Affairs speaks
 
Mnamo tarehe 19 Machi 2021, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kufuatia kifo cha Raisi Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Kuapishwa kwake kunaibua suala la msingi la kikatiba juu ya kuendelea au kutoendelea kuwapo kwa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Hayati Raisi John Magufuli....
Ccm hujiamulia tuu hawajui katiba. Bunge lenyewe linalo tajwa ni nani aliwacgagua. Hata mwenda zake alikuwa akiwaambia hawakuchaguliwa na wananchi. Hilo ni bunge la tume ya uchaguzi na baadhi ya vyombo vya dola.

Usishangae wakamwambia Mh Mama Samia aendelee na mawaziri ambao hawaja apa mbele yake
 
Kama nimeelewa vizuri kana kwamba kwa sasa hatuna Waziri Mkuu wala Baraza la Mawaziri! Naomba kusahihishwa tafadhali
Kwa mujibu wa muongozo wa TLS upo sahihi, waziri mkuu na baraza lote la mawaziri wanatakiwa kuteuliwa na kula kiapo mbele ya rais (aliye wateua).

Hivyo kwa sasa hakuna cha PM, waziri wala naibu waziri yoyote yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TLS kwa mara ya kwanza nimeona mmetekeleza wajibu wenu wa kisheria kwenye nchi hii. Mawaziri wote ikiwemo waziri Mkuu inabidi waambiwe, na wasiendelee kutokea kwenye nafasi zao kwani kwa sasa hakuna baraza la mawaziri.

Nimemuona Majaliwa akiendelea kutambulishwa kama waziri Mkuu, wakati kikatiba hana uhalali huo. Tungekuwa na vyombo vya habari vinavyotekeleza wajibu wao walipaswa kulitangaza hili wazi wazi kuwa kwa sasa hakuna baraza la mawaziri, na waziri yoyote aliyekuwa kwenye baraza lililopita asiendelee kuingia ofisini au kutumia mali za ofisi kama gari nk, wakati hana uhalali huo.
 
Mnamo tarehe 19 Machi 2021, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kufuatia kifo cha Raisi Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Kuapishwa kwake kunaibua suala la msingi la kikatiba juu ya kuendelea au kutoendelea kuwapo kwa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Hayati Raisi John Magufuli...
TLS ni kiungo muhimu sana kwa ustawi wa Taifa letu, haswa ukizingatia kwa nyakati kama hizi ambapo bunge letu limekuwa 'bubu'.

Nawaombea afya njema na baraka tele kutoka kwa Mungu Mwenye Enzi, daima msitetereke.
 
Yule mama Ni mwelewa Sana..naimani atafata katiba

Nimeona pia leo amerekebisha muda wa maombolezo kuwa siku 21 kwa mujibu wa katiba, baada ya kufanya makosa kwenye ile taarifa ya awali kuea ni siku 14. Rais aliyepita alikuwa sio mfuataji wa katiba, na TLS wakawa waoga kusema katiba inasema nini. Mfano rais alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha, wakati jeshi limetengwa kikatiba na jeshi/vyombo vya dola.
 
Back
Top Bottom