TLP updates: Tangu kuanzishwa kwa Vyama vingi, chama cha upinzani kinamuunga Mkono Mgombea Urais kutoka chama tawala

HUU SI UBINADAMU KABISA,
Wewe unaona mnayoyafanya ni ya mtu hai? Mwenye roho hai? Nyinyi ni opposition party , kazi yenu ni kuikosoa/kuielekeza serikali wapi wamekosea then later mshike nchi! Mnajinadi mtazunguka nchi nzima kumnadi "mpinzani" wenu! Mnaishi kweli na roho? au ni maiti isiyokuwa na fahamu! Ndiyo maana nimeweka ".." (inverted commas!
 
Tangu mkutano mkuu Wa Chama chetu Wa tarehe 09/05/2020 umpitishe kwa Sauti moja Mhe. Dk John Pombe Joseph Magufuli kuwa Mgombea Wa TLP kwa nafasi ya Urais Wa JMT,

Kwa mara ya kwanza Mkt Wa Chama chetu Mhe. Dk Augustino Lyatonga Mrema atakutana ana kwa ana na Mhe. Dk John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano Mkuu Wa Chama chake baada ya Kuitikia Mwaliko wake kuhudhuria mkutano huu utakaofanyika Jiji Dodoma,

Mhe.Dk Lyatonga Mrema ameambana na Katibu Mkuu wake Bw Lymo pamoja na Makamu Mkt Wa Chama Bi.Dominatha Rwechengula,

Tangu kuanzishwa kwa Vyama vingi mwaka 1992 kwa mara ya kwanza Chama cha Upinzani kinamuunga Mkono Mgombea Wa Urais toka chama tawala kwa Vikao ili kutafsiri Uzalendo kwa Vitendo,

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu mbariki Rais Magufuli,
Mungu Ibariki TLP,

____________
TLP njaa ya mwenyekiti wenu ndiyo shida yenu kubwa!
 
Ule ni ugonjwa tu ambao hata wewe au mimi tunaweza kuupata hivyo tuchunge kauli zetu.
Unakuwa na ugonjwa halafu msaliti wa upinzani! Lazima ukanyagwe! Pumbavu zake mrema, yaani akina Ben, azory anaona swa badala ya kulaani yanayotokea tangu serikali iingie madarakani!!
 
Unakuwa na ugonjwa halafu msaliti wa upinzani! Lazima ukanyagwe! Pumbavu zake mrema, yaani akina Ben, azory anaona swa badala ya kulaani yanayotokea tangu serikali iingie madarakani!!
Kwa hivyo ukiwa na ugonjwa unakosa haki ya kuchagua utakacho ambacho ni halali kisheria?
Mrema ni ugonjwa na kesi za hao wengine si ugonjwa na hatuwezi kusema kwa 100% wamekutwa na nini, nani anahusika, au chanzo ni nini.

Tunalinganisha matufaa na machungwa (comparing apples and oranges), what a stroke of a genius!!!
 
nadhani wote ni wajinga! Ikitokea mageuzi ndiyo utaona kuwa mlihusika!
 
Back
Top Bottom