Uchaguzi 2020 TLP Updates: Fahamu Mambo matano (5) kati ya ishirini na moja (21) yanayoisukuma zaidi TLP kumuunga Mkono Mhe Dkt. John Magufuli kuelekea Okt 2020

Ze Bulldozer

JF-Expert Member
Jun 12, 2020
998
520
" HAYA NDIO MAMBO MATANO( 5 ) KATI YA ISHIRINI NA MOJA ( 21 ) YANAYOISUKUSUMA ZAIDI LABOUR PARTY YA TANZANIA KUMUUNGA MKONO MHE DK JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KUELEKEA OCT 2020 "

1. Watumishi 32,555 wenye dosari serikalini,
Nyote Mtakumbuka March 2016 Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli aliwaondoa watumishi wenye dosari wapatao 32,555 sawa 5% ya watumishi wote serikalini na hivyo kuokoa pesa za serikali kiasi cha Tshs 19.8bln katika kila mwezi hii ni sawa na Tshs 237.6bln kwa mwaka,Mpaka mwezi huu ( kwa miezi 51 ) Taifa kupitia yeye litakuwa limeokoa jumla ya Tshs 1.01trl zilizotafunwa bila huruma ambazo ni sawa na bajeti ya dawa kwa miaka 33 mfululizo kwenye Serikali ya awamu ya nne iliyofikia Tshs 31bln mwaka 2014/15,kiasi hiki cha fedha kilichookolewa ni sawa na kile kilichotoa elimu bila malipo kwa miaka yote mitano ( 5 ) yaani Tshs 1.01trl

Ndugu Watanzania wenzetu, Hizi Tshs 1.01trl kupitia yeye zimetusaidia kuajiri vijana wetu 74,173 na kuongeza mishahara kwa njia ya kupandisha madaraja( Promotion ) watumishi wapatao 306,917 sawa na 44% ya watumishi wote na ile hoja kwamba Mhe Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli hajaongeza mishahara kwa miaka 5 mfululizo kwa muktadha huu “ Si ya kweli ” kwani mfumo huu wa kuongeza mishahara kwa njia ya kupandisha madaraja ni bora zaidi ya ule wa ongezeko la lazima la mshahara ( statutory annual salary increment) ambapo kimataifa ( ILO ) ni kati ya 1-3.1% tu kwa mwaka ukilinganisha na huu wa kukua/kupanda kwa TGS.

Ndugu Watanzania wenzetu,Hizi Tshs 1.01trl kupitia yeye zimetusaidia kulipa madeni ya watumishi yaliyohakikiwa yasiyo ya kimishahara na yakimishahara yenye thamani ya Tshs 472.6bln,Sisi Labour Party,katika vikao vyetu hivyo tulitafakari sana juu ya jambo hili,Kama mtu anaweza kuokoa pesa ya serikali inayofikia Tshs 1.01trl iliyokuwa inatafunwa bila huruma hivi Sisi ni nani hata tusimuunge mkono mtu wa aina hii! Na ninyi wengine mnasubiri nini kumuunga mkono Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli kuelekea oct 2020 ili kushuhudia maajabu zaidi?

2. Usambazaji wa Umeme vijijini (REA)
Ndugu Watanzania wenzetu,Wakati Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015 palikuwa na vijijini 2,018 tu vyenye umeme nchi nzima,kwa lugha rahisi tangu Tanzania iumbwe ni vijiji 2,018 tu kati ya vijiji 12,268 sawa 17% ndio vilikuwa na umeme kabla ya ujio wa Mhe Dk John Pombe Magufuli kama Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Nov 2015.

Ndugu Watanzania wenzetu,Mpaka tarehe 09/05/2020 tunatangaza kumuunga mkono Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli bei ya kuunganisha umeme ilifikia Tshs 27,000/= tu toka Tshs 177,000/= mwaka 2015,Kwa bei na miaka hii minne na nusu jumla ya vijiji 9,112 sawa na 74.3% sawa na ongezeko la vijiji 7,094 vilikuwa vinawaka umeme,Mpaka tunatoa tamko hili ni vijiji 3,156 tu sawa na 25.73% ndio bado havijafikiwa na umeme ili kufanya Tanzania yote kumeremeta kwa Umeme wa uhakika

Ndugu Watanzania wenzetu,Mfahamu pia uzalishaji wa Umeme umeongezeka toka 1,038MW mwaka 2015 hadi 1,602MW mwaka huu sawa na ongezeko la 564MW sawa na 54.34% wakati huohuo Umeme toka maporomoko ya Rufiji ( SG ) wenye kuzalisha karibu 2,115MW ukisubiriwa ili kuifanya Tanzania kuwa na vyanzo vya umeme vinavyofikia 3,717MW Umeme utakaotulazimu pia kuwauzia majirani zetu,Mpaka sasa watumiaji wa umeme nchini wamefikia 85% toka 35% mwaka 2015 sawa na ongezeko la 50%, kwa haya yote,hivi Sisi Labour party ni nani hata tusimuunge mkono mtu wa aina hii na ninyi wengine mnasubiri nini kumuunga mkono Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli kuelekea oct 2020?

3. Ujenzi wa miundombinu ( infrastructure)
Ndugu Watanzania wenzetu,Kabla ya kumuunga mkono Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli tulipitia ripoti ya “ The Africa Construction trend report 2019 ” ya Deloitte Consultancy Firm,Tanzania na Kenya walisajiri miradi mikubwa 51 kila moja isipokuwa thamani ya miradi ilitofautiana baina yao,Miradi 51 toka nchi ya Kenya ilikuwa na thamani ya $ 36bln sawa na 24.6% ya thamani ya miradi yote 182 ambayo ni $146bln na miradi 51 ya Tanzania ilikuwa na thamani ya $60.3bln sawa na 41.2% au Tshs 140trl ya thamani ya miradi yote.

Ndugu Watanzania wenzetu,Sisi TLP tulishangaa sana Kwa miaka zaidi 35 ni Kenya na Ethiopia pekee ndio zimekuwa nchi zinazoongoza kwa kurekodi miradi mingi na mikubwa yenye thamani kubwa katika Ukanda wa nchi za Africa ya Mashariki,Tanzania pamoja na rasilimali zetu lukuki hatukuwahi kufikiriwa kuwa ipo siku tutaongozi kwa miradi ya thamani kubwa Ukanda mzima wa Africa Mashariki wenye nchi za Kenya,Ethiopia,Uganda,Rwanda,Burudi,Shelisheli,Djibout,Somalia,Comoro na Elitrea.

Ndugu Watanzania wenzetu,Nibaada ya karibu nusu karne ni kwa mara ya kwanza Tanzania inarekodi miradi yenye thamani kubwa zaidi ya Ethiopia & Kenya vinara wa miradi mikubwa na yenye thamani kubwa kwa miaka 35 na hili linafanyika chini ya Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli huku jumla ya thamani ya miradi yetu ikifikia 41.2% ya miradi yote ambayo ni karibu sawa na nusu ya thamani ya miradi yote 182 yenye jumla ya $146bln kwa lugha rahisi kazi inayofanywa na Rais mmoja wa Tanzania ni karibu sawa na nusu ya kazi yote inayofanywa na marais wote kumi ( 10 ) toka nchi za Kenya,Ethiopia,Elitrea,Uganda,Rwanda,Burundi,Comoro,Somalia,Shelisheli na Djibou ti,hapa yupo pia Uhuru Kenyatta wa Kenya.

4.Ukuaji wa Sekta ya Elimu nchini,
Ndugu Watanzania wenzetu, Mfahamu kuwa sisi pia tunawatoto wanaosoma katika shule zetu za Awali,Msingi na Sekondari,Baada ya Tangazo la Elimu bila Malipo mapema mwaka 2016 kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto kujiunga na shule zetu katika ngazi mbalimbali,Hadi tunatangaza kumuunga mkono Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli tarehe 09/05/2020 watoto wetu na watoto wa masikini wenzetu wastani wa wanafunzi1.6M wamejiunga mwaka huu tofauti na wale 1.0M waliojiunga mwaka 2015,Kwa lugha rahisi elimu bila malipo ya Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli imekuja na wastani wa watoto 600K zaidi kila mwaka au wastani wa watoto 3M kwa miaka hii mitano ya kwanza,Kwa matokeo haya,Sisi Chama cha Labour ni nani hata tusimuunge mkono Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli na mnaosema tumenunuliwa ninyi Uzalendo wenu uko wapi kwa Taifa lenu?

Ndugu Watanzania wenzetu, Jumla ya shule mpya za msingi 905 zimejengwa kwa miaka hii minne na nusu na kufikia jumla ya shule 17,804 mwaka huu toka shule 16,899 mwaka 2015,Huku shule zingine mpya 622 za Sekondari pia zikijengwa na kufikia jumla ya shule 5,330 kutoka shule 4,708 mwaka 2015,Na Shule zote kongwe 89 zimekarabatiwa isipokuwa 16 tu sawa na 18%,Mabweni 253 na vyumba vya maabara 227 pia vilijengwa,kwa lugha rahisi jumla ya majengo mapya 2,007 yakujifunzia yamejengwa na Mhe Dk John Joseph Pombe Magufuli kwa muda huu mfupi wa awamu yake ya kwanza,Tutafakari kwa pamoja ni nini kitatufanya tusimuunge mkono mtu huyu kwa kazi hizi na iweje mtu anayeunga mkono haya tuseme kanunuliwa!?tuendelee kutafakari na kujitafakari kizalendo tena na tena

Ndugu Watanzania wenzetu, Mikopo ya Elimu ya Juu imepandwa kwa Tshs 101.3bln yaani kutoka Tshs 348.7bln mwaka 2015 hadi Tshs 450bln mwaka 2020,Jumla ya wanafunzi wapya 32,583 wameongezwa na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wanaopata mkopo kufikia130,883 mwaka 2020 toka wanafunzi 98,300 mwaka 2015 huku wanafunzi wa Sekondari ( I-IV ) wastani wa wanafunzi 537,000 wakiongezeka na kufika wanafunzi 2.185M mwaka 2020 ukulinganisha na wanafunzi 1.648M haya yote yakiwa ni matokeo ya Tshs 1.01trl fedha za elimu bila malipo toka kwa Mhe Dk John Joseph Pombe Magufuli haya ndio yanatufanya sisi chama makini cha Labour Tanzania,

5.Kuimarika kwa Huduma za Afya nchini,
Ndugu Watanzania wenzetu,Upatikanaji wa damu salama umeongezeka na kufikia lita 309,376 kwa mwaka 2020 toka lita 104,632 mwaka 2015 sawa na ongezeko la lita 204,744 ikiwa ni sawa na 196%, ndio sababu vifo vya watoto wachanga vimepungua na kufikia vifo 7 kutoka 25 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2015,Wakati huohuo WHO wanasema mwaka 2019 maambuzi ya Malaria yalipungua kutoka 14% mpaka 7% ( Single digit ) maana yake Tanzania sasa Chini ya Mhe Dk John Joseph Pombe Magufuli malaria imeshuka kwa 50%,Huku Bajeti ya dawa nayo ikifikia Tshs 270bln toka Tshs 31bln mwaka 2015 ikiwa ni sawa na ongezeko la Tshs 239bln mwaka 2020 sawa na 771%,Watanzania wenzetu,Hivi kwa haya yanayofanyika sasa TLP ni nani hata tusiyaone haya, na iweje tukiunga mkono iwe ni nongwa kwenu,?Ninyi Uzalendo maana yake nini kama si huu wa kusimama nanchi yetu!?

Ndugu Watanzania wenzetu,Mmeona na kushudia Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli akijenga hospitali tatu ( 3 ) za rufaa,za mikoa kumi ( 10 ), za wilaya sabini na moja ( 71 ),vituo vya Afya 487,Zahanati 1,198 na kufanya Jumla ya Vituo vipya vya kutolea huduma vilivyojengwa awamu ya kwanza pekee kufikia 1,769 na hii inafanya jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya Tanzania kufikia 8,783 mwaka 2020 toka vituo 7,014 mwaka 2015,

Ndugu watanzania wenzetu,Ukitafuta uwiano wa Vituo hivi dhidi ya Idadi ya Watanzania ambao tunakadiriwa kufikia 55M, yaani 0.009M : 55M hii ni sawa na 1: 6,111 yenye maana kila Kituo kimoja cha kutolea huduma ya Afya Tanzania kitahudumia wangonjwa 6,111 kwa mwaka mmoja, Hii ni sawa na wagonjwa 6,111/366 kwa siku,ambao ni sawa na 1:17, maana yake Kila Kituo kimoja cha kutolea huduma za Afya kitahudumia Wagonjwa Kumi na saba (17) tu kwa siku na hili ni kama Watanzania wote 55 wataugua kwa siku moja,Hili limewezekana tu wakati huu chini ya Uongozi madhubuti wa Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli,

Ndugu Watanzania wenzetu, Sisi Labour Party baada ya kuona haya yote yakitokea Chini yake Rais wetu makini na Mpenda watu hasa Wanyonge na wanaodharaulika tumekubaliana kuungana na chama chochote cha Siasa nchini kwa Sharti la kwanza kumuunga mkono Mhe Dk John Joseph Pombe Magufuli kwa kutangaza hadharani kama tunavyofanya sisi. Pili, sisi Chama cha Labour Tanzania tutazunguka nchi nzima kumnadi Mgombea wetu Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli na kwa Unyenyekevu mkubwa tuwaombe kila anayedhani kuwa ni Mzalendo wa kweli wa Taifa letu asimame na Rais Magufuli kufa au kupona kwa jasho au kwa damu kuhakikisha mzalendo wetu huyu anasalia madarakani.

" TLP-Uhai Wa Mtanzania "🇹🇿

_________
 
Hujui kama siasa za ugali watu wanazijua huwa wanapenda majanga ili chama/mtu/cheo/kada fulani ipendwe kuliko wengine...

Baada ya watumishi hewa kuondolewa na wanajua kazi za utumishi wa umma sijui wanatuandalia makao gani huko tukistaafu.... Ulikuwa ujanja kucheza na kuwatengenezea dharau kwa jamii.

Kazi hiyo ya kukubali maagizo ya mitego kwa kwenda mbele sijui itaisha lini!? Wengine tunaangalia tu bora sekta ya UONGO iendelee kutafuta ZILIPENDWA

http://kilosadc.go.tz/storage/app/media/uploaded-files/346750078-Public-Service-Halmashauri.pdf
 
Basi kumbe sikua nalifahamu hili, kuna ajira 74 elfu? Nyongeza za mishahara kwa kuwapandishia watu madaraja, sijui mlimaanisha statutory increment au nini? Maana madaraja ni madaraja na hio statutory increment ni sheria. Haya mengine yote naona no hadithi tu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom