TLP: Tunampongeza Rais Samia kwa kupaisha bei ya mbaazi kwa 3200%. Hongera sana tuko nyuma yako

aisee! ndugu ondoa chuki na wivu moyoni, vitakuweka huru na kukuepusha na uongo. bei ya mbaazi ilishushwa kwa siasa za mwendazake na pm wake, majaliwa kassimu 2017 huko. hivi korona ilishafika kaka mwaka 2017?!!!! duuuu!

hata kama tunachukia, kwa nguvu zote, baadhi ya viongozi kwa sababu zetu za kurithi, kuambiwa (kushawishiwa), kuhisi n.k. bado kutokana na nguvu zao za kikatiba wataendelea tu kufanya mambo mema hata awe na mapungufu kiasi gani. mama samia, pamoja na mapungufu yake (kama binadamu) yapo ambayo ameshayafanya tayari na anaendelea kuyafanya;

1. mbaazi ndo hivyo bei inaongezeka tu
2. sgr ya kisaka-mwanza, twende kazi
3. kusini kuna mpango wa kuijenga reli
4. vituo vipya 90 vya afya njiani kujengwa
5. madaraja wamepanda % kubwa ya watumishi
6. kiwanda cha kukoboa mpunga cha bilioni 3, km sikosei, kinajengwa huko mwanzana kinamalizika hivi punde (october) n.k

chukieni na endeleeni kuomba mabaya tu lakini mdogo mdogo na kimya kimya mama anajivuta.......na ataeleweka tu.
Ungenisaidia kaongezaje mama hizo Bei?
 
Kama namuona Nape na wapigakura wake wanavyofurahia bei mpya ya Pamba,

Najua kwa hili Nape amemaliza Uchaguzi wa 2025.
 
NAPE NA NDUGU ZAKO MSIACHE KUMSHUKURU MUNGU KWAAJILI YA MAMA SAMIA | MBAAZI IMEPAA TOKA TZS 50 FY2017|2020-TZS 1,600 FY2021|22 KWA KILO

Bei ya mbaazi Tanzania chini ya Rais Samia imeongezeka karibu ( X3200 ) kutoka Shilingi Hamsini za Kitanzania hadi kufikia Tshs 1,600 mwaka huu,Mtakumbuka ni trh 19|3|2021 ndio siku ambayo Mama Samia alikabidhiwa nchi hii kama Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT wa awamu 6,huku bei ya mbaazi ikiwa ni chini ya Tshs 200|50.Kwalugha rahisi Fuso la Tani 7 lilijazwa mbaazi za watoto wa masikini kwa Tshs 350k Tu,Leo baada ya Rais Samia Fuso hilohilo linajazwa Mbaazi hizohizo kwa Tshs 11.2M,Mama Samia ameiongeza bei hii kwa zaidi ya 3,200%,Ukifungua hizo link utawasikia wakulima hao wakilalama,Mbaazi kutoka kuwa zao la Kibiashara hadi kuwa Chakula cha Ng'ombe na Nguruwe huku baadhi yao wakizisusa mbaazi hizo Shambani bila ya kuzivuna,Inaumiza.

Nape Nauye|Zitto Kawe kwenye bunge la 10 ndio vijana miongoni Mwawabunge wachache waliopaza sauti zao juu ya mporomoko mkali wa bei ya mbaazi Tanzania,Wakati flani Nape akishauriwa na Naibu Waziri wa kilimo wa wakati huo kama soko hakuna ni bora kuwahimiza Wapigakura wake Wale Mbaazi kwa wingi kwakuwa mbaazi zina Protini nyingi, majibu yaliyoonesha kama ni kejeli mbele ya Mhe Nape Mbunge wa Mtama na kwawalima mbaazi wote nchini,Ujio wa Rais Samia umeshusha neema|faraja tena na tena kwa wakulima|Wasambazaji na Wauzaji wa Mbaazi wa nje na ndani ya Tanzania,Kwenye hili Rais Samia anastahili pongezi toka kwa Watanzania wote na hasahasa Wale walioambiwa Wale mbaazi ili wanenepe badala ya kupata Pesa ambayo leo Wanaifurahia,

Mtakumbuka,Mwaka wa fedha 2015/16 bei ya Tani ya Mbaazi ilikuwa US$ 715.11,Tanzania tulijipatia kiasi cha US$ 113,760 ikiwa ni sawa fedha ya kuuza Mbaazi nje jumla ya Tani 160 tu ,Dollar hizi ni sawa na Tshs 264M,Gafla Mauzo hayo yaliporomoka mpaka kufikia US$ 5,112 sawa na Tshs 11.3M Tu,FY2018|19|20 ambazo ni sawa na mauzo ya Tani 5 tu za Mbaazi,Mapato haya ni sawa na anguko la 95.7% nadhani hii haijawahi kutokea popote pale dunia wakati huu bei ikiwa ni US$ 0.023 kutoka US$ 1.14 FY 2015|16|17.Bila shaka haya ndio yaliwaliza wakati wote akina Nape pale Bungeni kwenye bunge la 10.Leo Mama amepandisha bei ya Mbaazi mpaka kufikia US$ 0.73 kutoka US$ 0.023 ikiwa ni sawa Tshs 1,600 kutoka Tshs 50/Lakini pia Kahawa imepaa kutoka 1,000 ya mkopo hadi kufikia Tshs 1,500/= Cash, Mwenye Masikio na asikie sasa,






...Kazi iendelee...








" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
 
Rais Samia ni mpango halisi wa Mungu,Mungu wetu hakawii wala hawai ni huyuhuyu tumepewa tumlinde,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom